Rais Samia ashiriki Kongamano la Pili la Kumuenzi Hayati Benjamin Mkapa, ahimiza ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
FXmwdoQXoAI_hds.jpg




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kongamano la Pili la kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa leo tarehe 14 Julai, 2022 katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar.
JOAQUIM ALBERTO CHISSANO, RAIS MSTAAFU - MSUMBIJI

- Siwezi kuzungumza Kiswahili vizuri

Ahsante sana kwa kukumbusha watu kuwa nilizungumza kwa Kiswahili kule Umoja wa Afrika, na ile ilikuwa tu kuwakumbusha watu kwamba Kiswahili ilikuwa ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika kipindi kile na watu wakaamini kuwa nilikuwa nafahamu Kiswahili vizuri. Lakini si kweli kwamba nafahamu Kiswahili kwa kiasi hicho, na kwahiyo siwezi kutoa hoyuba yangu kwa Kiswahili. Niruhusu nizungumze Kiswahili.

Naweza kuzungumza Kiswahili cha Mtaani lakini si kwa kiasi hicho.

- Urafiki wa Chissano na Mkapa
Najua mpo mnaojiuliza kuwa likuwaje watu hawa wawili (Chissano na Hayati Mkapa) walikuwa marafiki. Ningependa nitumie dakika mlizonipa nieleze namna tulivyokuwa marafiki.

Nilikuwa namuita “Ben” na yeye alikuwa akiniita Joachim, kwakuwa alikuwa hawezi kutamka Joaquim kama inavyotamkwa kwa Kireno.

Mara ya kwanza ya urafiki wetu ilikuwa mwaka ambao matatizo yaliyokuwa yakionekana ni ya ndani chama cha Ukombozi cha Msumbiji ambapo tulianza kujikita na kuwaunganisha watu wa Msumbiji na wa Tanzania.

- Mchango wa Mkapa Ukombozi wa Msumbiji
Tulitaka ndugu zetu Watanzania watuunge mkono katika mapambano yetu. Tulikuwa na migawanyiko mbalimbali ndani ya nchi yetu na tulitaka kuiondoa. Tuliueleza uongozi wa TANU na Afro-Shirazy Party (ASP) ili watusaidie kueleza katika taasisi zao mbalimbali na kwa wananchi wote wa Tanzania.

Wakati ule vyombo vya habari vilikuwa ni muhimu sana. Benjamin Mkapa wakati ule alikuwa ni Mhariri mkuu wa magazeti mawili ya TANU – The Nationalist na Uhuru.

Uwezo wake wa kusikiliza na kufanya uchambuzi wa kina wa matukio ambayo aliyafahamu moja kwa moja au kupitia wanahabari wake kama vile Ferdinand Luhinda, John Tesha na wengine, ulifanya magazeti yake yatoe taarifa kwa viongozi kuhusu mapambano yetu. Kazi yake ya uanahabari iliendelea kutetea ukombozi wa Afrika.

Tukiangalia magazeti mawili chini ya uhariri wake yalikuwa ya viwango na ubora wa juu sana. Mapambano ya vita kule Msumbiji tulikuwa tukifanikiwa sana na ilipofika 1996 tukafikia kuwa na maeneo au kanda mbalimbali za nchi yetu ambazo tulikuwa tumeshazikomboa.

Huu ulikuwa ni ukombozi muhimu lakini adui akataka kuendelea kutugawanya na kuchukuwa baadhi ya wapiganaji wetu ili kuharibu mapambano. Hiyo ilikuwa ni vita iliyoletwa kutoka nje, lakini yeye Mkapa pamoja na wanahabari wake wakatusaidia sisi katika mapambano hayo.

Kwahiyo, mbali na vipawa vyake binafsi alikuwa na hisia za Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamini kwamba Tanzania haitaweza kuwa huru kama taifa lingine la Afrika lipo chini ya Ukoloni.

HUSSEIN ALI MWINYI, RAIS – ZANZIBAR

Kumbukizi hii ya pili ina nafasi adhimu kwangu. Kwanza, ni mara ya kwanza nakuwa mwenyeji kwenye shughuli hii na pili, ni mara ya kwanza kuhudhuria kumbukizi hii nikiwa kama Msarifu – yaani settler wa Taasisi ya Mkapa Foundation.

- Kijiti cha Usarifu wa Taasisi ya Mkapa
Leo napenda nihadithie kwamba wakati nilipofuatwa kuombwa kuwa Msarifu nilikuwa kigugumizi kukubali. Uzito wangu ulikuwa ni kwa mashaka kuwa viatu ninavyovyaa ni vikubwa ukizingatia kwamba Msarifu wa kwanza alikuwa ni yeye mwenyewe Mzee Mkapa. Sikuwa na njia wala uthubutu wa kukataa dhima ya jukumu la kuwa Msarifu.

Nilipata nguvu zaidi ya kukubali kuongoza Taasisi hii nikitambua kuwa matunda ya kazi zinazofanywa na taasisi hii yanalenga kuleta ustawi wa taifa letu, na kazi njema lazima iendelezwe. Kazi bora na njema inaendelezwa ikiwa pia ni njia bora ya kumuenzi Mzee Mkapa.

Kwa kutambua ukubwa na dhima wa jukumu nimejizatiti kadiri ya uwezo wangu kuongoza taasisi hii kuhakikisha kwamba dira na dhamira ya kuanzishwa kwake inafikiwa.

- Mashirikiano na Sekta Binafsi
Serikali ya Zanzibar imeweka kipaumbele cha kuendeleza mashirikiano na sekta binafsi pamoja na sasasi za kiraia. Vilevile suala la ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi limehimizwa katika dira ya maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050; Ilani ya CCM mwaka 2020/25 pamoja na mipango mingine ya maendeleo ya kitaifa.

Naendelea kufarijika kwa namna ambavyo sekta binafsi pamoja na asasi za kiraia zinavyoendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo.

Taasisi ya Mkapa, kwa upande wa Zanzibar, inafanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma, mafunzo na hivi sasa katika kutelkeleza mipango itakayotuwezesha kuanzia Bima ya Afya hapa Zanzibar. Ni vema asasi nyingine za kiraia zikaiga mfano huo.

Ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi umesaidia sana katika mapambano yetu dhidi ya UVIKO-19. Taasisi mbalimbali zinaendelea kushirikiana na Serikali katika upatikanaji wa vipimo, vifaa tiba, utoaji wa chanjo, pamoja na ukusanyaji wa takwimu na katika maeneo mengine mengi.

Mafanikio haya yameongeza imani kwa wananchi juu ya mashirikiano ya Serikali na sekta binafsi, si tu katika uwekezaji lakini pia katika utoaji wa huduma za jamii.

- Ujasiri na Changamoto za Mageuzi
Wakati tukimkumbuka Mzee Mkapa, nachukuwa fursa hii kugusia wosia na falsafa aliyotuachia kuhusu ujasiri na changamoto za kufanya mageuzi. Katika kitabu chake: My Life, My Purpose; A Tanzanian President Remembers, akizungumzia ugumu aliokutana nao akifanya mageuzi ya Ubinafsishaji Hayati Mzee Mkapa ameandika ya fuatayo na ninaomba kunukuu:

“Kuwa kiongozi kunahitaji kuwa tayari kubadilika kuendana na mawazo mapya na kuwa na ujasiri wa kutekeleza yale yaliyo sahihi.”

Mwisho wa kunukuu.

Ushpavu huu wa uongozi unajidhihirisha pia katika uongozi wa waasisi wetu wa Mapinduzi ya Zanzibar wa Mzee Abeid Aman Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar aliyesema, naomba nimnukuu:

“Ni heri kugombana na mtu katika jambo tutakalokuja kupatana baadaye.” Mwisho wa kunukuu.

Kwa kawaida, mageuzi kama yalivyo mapinduzi, huja na mafanikikio na changamoto zake. Ni hulka ya binadamu kupenda kushikilia jambo alilolizoea hata kama linamgharimu. Ndiyo maana wahenga wakasema, mazoea yana tabu.

Binadamu angependa yale mabadiliko tu ambayo hayaji na changamoto, ama hayatibui mazoea yake. Bahati mbaya mawili haya hayawezi kutenganishwa.

Kwa kutambua hilo Serikali imamua kushirikisha Sekta Binafsi katika Nyanja zote za maendeleo sababu ni sahihi kufanya hivyo. Tutaendelea kuwaelimisha wale wote wenye mashaka wakati tukiendelea kuzishirikisha Sekta Binafsi. Ni imani yetu tutakuja kuelewana baadaye.

Wale watakaopata ugumu kuelewa fikra na matendo yetu, watakuja kuyaelewa matokeo watakapoyaona. Huo ndiyo ustahimilivu na ushupavu wa ungozi aliouzungumzia Hayati Benjamin William Mkapa na viongozi wtu wengine waliotangulia.

Nakuhakikishieni kuwa mimi na wenzangu tunao ustahimilivu na ushupavu wa kufanya hayo. Na wale ambao utashindwa kabisa kuendana nao, basi tutawaombea du’a.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS - TANZANIA

Nimefurahishwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa kushirikiana na Serikali kulinda utamaduni wetu huu wa kumuenzi mpendwa wetu Hayati Benjamin William Mkapa. Kufanyika kwa kumbukizi hii ni Ushahidi kuwa tumedhamiria kuuenzi mchango wake katika maendeleo aliyoyachangia katika taifa letu, Afrika na Dunia.

- Taasisi Ipo Kwenye Mikono Salama
Msarifu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, tunaamini viatu ulivyovivyaa vitakutosha. Nina hakika unamtendea haki Mzee wet una sina shaka anafurahia na kujivunia kazi yako. Na sisi inatupa amani sana kuwa taasisi ipo katika mikono salama mno na kwamba utaendelea kuleta matunda ambayo yamekusudiwa.

- Urafiki wa Mbeki, Chissano na Mkapa
Nimefurahi pia kuwaona Marais wetu wastaafu Joaquim Chissano na Thabo Mbeki. Wazee hawa walikuwa marafiki wa karibu sana wa Hayati Mzee Mkapa. Walipatana kifikra na walikuwa na urafiki uliojikita vyema katika udugu na umoja wa nchi zetu tatu kama wenyewe walivyoeleza hapa.

Misimamo yao aghalabu haikutofautiana. Akiwepo mmoja kwenye mkutano hakukuwa na shaka kuwa maslahi ya ukanda wetu yatawakilishwa vyema. Fikra zao zilikuwa zinaenda pamoja.

- Mzee Mbeki na Chissano Mmmetufuta Machozi
Umoja wenu, kuwepo kwenu na sisi hapa leo unadhihirisha katika maneno yenu mazuri mliyoyatoa hapa ya kumwelezea Rafiki yenu Mzee Mkapa. Mmetufuta machozi na kutufutia upweke. Tukiwaona tunafarijika na kuona kwamba Mzee Mkapa yupo katikati yenu. Leo hayupo tena lakini tukiwaona ninyi tunajihisi tupo naye.

Nimevutiwa sana na kaulimbiu ya mwaka huu inayosema: “Uongozi Shupavu ni Kichocheo cha Kuleta Mabadiliko kwa Manufaa ya Wote”

Binafsi nilitamani sana kuwa sehemu ya mjadala uliofanyika jana uliofunguliwa na Mh. Othman Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, uliojikita katika kujadili nafasi ya sekta binafsi katika kuondosha changamoto za afya tulizo nazo na hatimaye kuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea katika kulinda afya za Watanzania.

- Ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi
Matamanio yangu hayo yanatokana na imani kuwa ikiwa tunataka kwenda kwa kasi na kufikia lengo letu la 2030 la afya bora kwa wote basi hatuna budi kubadili mtazamo wetu kuwa tunaweza kulifanya hilo peke yetu. Zile enzi za kwamba serikali itafanya yenyewe kila kitu, nadhani inabidi tubadilike.

Lazima tushirikishe sekta binafsi ili twende kwa kasi na kupata matokeo tunayoyataka.

Mzee Chissano amemsifia vema Mzee Mkapa kwa kuleta mageuzi wakati wa globalization, liberal economy au market economy. Mzee Mkapa alikuwa muumini thabiti wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi katika kutatua changamoto zinazotukabili.

Alihubiri sana juu ya hili na alitangulia wakati kwasababu wakati ule bado nchi yetu ilikuwa ina imani ya kijamaa isiyoamini kushirikiana na private sector. Lakini yeye alikuwa na uthubutu wa kutushawishi kufanya kazi na private sector. Yumkini wakati ule hatukumuelewa sana lakini sasa tunaendelea kumuelewa.

- Ushupavu Katika Uongozi
Muhimu zaidi, alikuwa na ushupavu wa uongozi katika mabadiliko hayo pamoja nay eye kuwa muumini thabiti wa ujamaa ila kwa wakati ule kama nilivyosema, nchi ikiwa na imani ya Ujamaa isiyoamini sekta binafsi.

Nakumbuka katika hotuba yake aliyoitoa katika Halmashauri Kuu ya CCM tarehe 5 Agosti, 2004 kule Dodoma alizungumzia ushupavu wa uongozi unaohitajika katika Karne ya 21. Katika hotuba ile, pamoja na mambo mengine mengi, Mzee Mkapa alituasa kuwa, na hapa naomba ninukuu:

“Uongozi shupavu hauogopi kubadili mkakati iwapo ni lazima kufanya hivyo. Tukishaamua sera tujadili mkakati wa kutenda, na si wa maneno. Ukiwepo ubishi, uwe wa kasi na ubora wa utendaji na siyo ubishi wa sera ambayo tulikwishaiamua.”

Mwisho wa kunukuu.

Kwahiyo ukisoma kwenye mistari ya maneno hayo, Mzee Mkapa aliusoma wakati tulionao leo. Bado tunaendelea kubishana na sera badala ya kubishana na ubora wa utendaji wetu. Lakini tukiikumbatia sekta binafsi. Bado hatujaamini kwamba sekta binafsi ni mshirika muhimu katika kuleta maendeleo ya Tanzania.

Hakuogopa kutueleza kuwa uchumi wa dunia wa sasa ni uchumi wa soko na kwamba ubia na sekta binafsi ni jambo lisiloepukika. Sasa tumelitambua hilo na kuliainisha katika mikakati yetu ya maendeleo ya kitaifa ndani ya nchi yetu ikiwamo pia katika Mpango Mkakati wa Tano wa Sekta ya Afya, au Health Sector Strategic Plan -HSSP5.

Kwa upande wa Sekta Binafsi natarajia watapokea wito wetu na kutoa ushirikiano na kwamba watazingatia kuwa Afya ni stahili ya Umma na sio biashara, hivyo lazima mzingatie urari kati ya kupata faida kiasi na kuwekeza katika kutoa huduma endelevu za Afya kwa Wananchi na kuwekeza pale kwenye mahitaji makubwa zaidi kwa maslahi ya Umma
 
Mama kwa matamasha na mitoko hajambo.

Wacha sisi kila kitu kipande bei huku. Watu walambe asali na kamba zao zizidi kuwa ndefu.
 
Miaka 200 mbele hafla za kuwaenzi marais waliopita zitawashughulisha sana marais watakaokuwa madarakani.
 
Siyo chini ya 6B
Kweli kabisa kwa watu ambao wamewahi kushiriki katika halfa za kiserikali wanaelewa mfuko lazima ujae pesa ndefu unaingia.

Mfano mimi ningekuwa Rais ningefuta mikutano na halfa zisizo na umuhimu na hata zikiwepo chache zitakuwa simple hakuna wakutumbuiza, maonyesho, watu wengi nk ni kutoa taarifa kuhusu mambo muhimu na kuondoka ili kuokoa pesa zitakazoteketea na kupigwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom