kitukuupinde
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 210
- 168
NI vema nianze makala hii kwa kurudia kidogo jambo ambalo kwa muda mrefu nimekuwa nikiliamini kwa dhati: kwamba zaidi ya miaka 20 ya demokrasia ya vyama vingi haijamnufaisha sana Mtanzania wa kawaida.
Zaidi tumeshuhudia demokrasia ndani ya vyama vya siasa ya kusuasua na kelele nying tu. Pamoja na hayo, hakuna ubishi kwamba Mwenyekiti Mwanzilishi wa CHADEMA, mzee Edwin Mtei, ni mtu ambaye alikuwa tofauti na viongozi wenzake wengi kwenye kambi ya upinzani. Mtei ni mtu ambaye alikuwa kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu na aliacha rekodi nzuri. Na alifanya kazi nzuri pia nje ya nchi.
Jambo ambalo najiuliza tu ni kama Mtei hakuona kwamba pengine kungekuwa na uwezekano mzuri zaidi wa kuwa na demokrasia ya maana nchini kama angeungana na wenzake wachache ndani ya CCM kupigania kwa dhati. Kukimbilia kuanzisha chama wakati mwingine si dawa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kitabu cha maisha ya Mtei, walipokubaliana juu ya jina Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lengo lilikuwa kuwa na chama ambacho kitaakisi demokrasia ya ndani pamoja na nchini kwa sababu kuu za maendeleo.
Chama hicho pia kilipaswa kuwa kinaamini kwa dhati juu ya dhana ya "uzawa" pamoja na mambo mengine yanayoambatana na uchumi wa soko huria. Vilevile CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kupaswa kuendelea kuwa kuamini katika falsafa ya mrengo wa kulia na ndio maana chama hicho kimo katika taasisi ya International Democratic Union, IDU, inayokutanisha chama kikongwe cha Uingereza cha Conservative na vingine vingi duniani.
Sasa tukienda kwenye Uchaguzi Mkuu wa 1995, ambao Mzee Mtei aliandika "kulikuwa mtihani wa kwanza wa kweli kwa demokrasia ya vyama vingi", pengine lugha sahihi zaidi ingekuwa ni "mtihani hasa kwa CHADEMA" maana ndiyo mwaka ambao tulishuhudia Augustine Mrema akijiuzulu kutoka CCM.
Na CHADEMA kilionyesha kama vyama vingine kuwa tayari kumkaribisha na kumteua kuwa mgombea urais wao. Tatizo lilikuwa tu shinikizo la Mrema kutaka kuwa pia Mwenyekiti wa Taifa. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ilibidi kuitisha Mkutano Mkuu ili kumchagua Mrema.
Hata hivyo, CHADEMA kilishirikiana na NCCR-Mageuzi kwenye kampeni kwa maelewano kwamba wangeunda serikali ya mseto endapo wangeshinda. Ushirikiano huo ulizaa kila aina ya matatizo na kwa maneno ya Mtei, mtu mmoja mkubwa ndani ya CCM alimwambia miaka michache baadaye kwamba tangu siku yeye Mtei alipotangaza kwamba CHADEMA kingemuunga mkono Mrema, alipoteza imani kwake.
Na Mtei anasema akitazama nyuma, anakiri hilo lilikuwa kosa moja kubwa katika maisha. Anaendelea kusema kwamba yalikuwa ni maoni ya wengi ndani ya chama chake ambayo alikuwa anajaribu kuheshimu lakini anasema alipaswa kuwa na nguvu kuupinga. Haya si ndwele, tugange yajayo. Pia tunaambiwa kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!
Cha ajabu, mwaka 2000, chini ya Marehemu Bob Makani, ni kama CHADEMA hakikujifunza vya kutosha kutokana na yaliyotokea mwaka 1995 maana tuliona ushirikiano kati ya CHADEMA na CUF kwa kumuunga mkono Profesa Lipumba. Kwa jinsi ambavyo tuliona baadaye vyama hivyo vikitupiana vijembe mara kwa mara, huwezi kuamini vilikuwa pamoja hapo nyuma.
Tukienda mwaka 2005, chini ya Mwenyekiti mpya Freeman Mbowe, chama hicho angalau kilionyesha dalili ya kutoa changamoto ya aina yake kwa CCM. Kwa kweli ni jambo la kusifia sana baada ya kusoma kitabu cha Mtei, kwamba CHADEMA kiliamua kuwa na uwazi wa hali ya juu wa kidemokrasia kumpata mgombea urais kwa mara ya kwanza. Iliamuliwa kwamba mwanachama yeyote ataweza kugombea urais na walifika sita.
Utaratibu ulikuwa kwamba wagombea hao wote waliokuwa wamejitokeza kugombea urais watembelee kanda sita na kuhutubia mikutano mikuu ambako watajieleza namna gani watatekeleza ilani ya chama endapo watachaguliwa. Walikuwemo pia wanawake wawili.
Wagombea watatu wanaume walijitoa kabla ya mkutano wa mwisho na kuachia wanawake wawili, Anna Komu na Chiku Abwao, pamoja na Mbowe ambaye alipata zaidi ya asilimia 80 ya kura. Mgombea Mwenza naye alipatikana siku hiyo.
Kipindi hicho nakumbuka jambo jema alilokuwa anafanya Mbowe kama kiongozi wa chama ambacho kilistahili pongezi kubwa. Mbowe alikuwa amejenga tabia ya kuandika makala mara kwa mara juu ya masuala ya kitaifa na kwa kweli alinitia nguvu kiasi cha mimi kujenga mawasiliano naye katika kuendeleza fikra mpya nchini.
Ni jambo la kusikitisha kwamba kwa muda mrefu sasa ameacha kabisa kuandika - jambo ambalo lilikuwa linamtofautisha na viongozi wengi wa CCM ambao uwezo wa kuandika na hata kusoma maandiko ya maana ni mdogo sana.
Kwa kweli hili la kusoma na kuandika ni janga la kitaifa.
Sina budi niseme pia kwamba ni jambo la kusikitisha kuona hatua nzuri iliyofanyika ya kumpata mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2005, ni kama ulisahaulika baada ya hapo.
Mchakato wa kumpata mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2010 ambao Dk. Wilbrod Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisimamishwa ulikuwa umegubikwa na usiri wa hali ya juu. Hata Dk Slaa mwenyewe alionekana kuwa gizani juu ya kinachoendela. Ni jambo la kushangaza chama kilishindwa kuuendeleza msingi mzuri wa mwaka 2005.
Hapo kwa kweli mwelekeo uliokuwa wa CHADEMA ulianza kuwa shakani kwa namna fulani. Na nadiriki kusema pia kwamba kwa nafasi yake Dk Slaa, ilibidi yeye awe mstari wa mbele tangu mapema kusisitiza umuhimu wa demokrasia kwa ustawi wa chama chochote.
Maana tuliona yeye mwenyewe alivyokuja kuonja joto la jiwe mwaka 2015, alipowekwa kando na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kama mgombea urais wa CHADEMA. Kwa muda mrefu Dk Slaa alikuwa anatueleza kwamba suala la yeye kugombea au la si lake binafsi bali chama chake. Sasa sijui ni chama gani hicho ambacho kinashindwa kuweka uwazi mapema kwa suala zito la urais wa nchi. Ni watu wa kuwashtukizia tu wananchi.
Huwa naamini kipimo kizuri cha kiongozi ni kama anafikiria madhara ya jambo fulani hata kama kwa wakati fulani inamnufaisha kwa namna yoyote. Binafsi, nikimfikiria sana Dk Slaa, nachanganyikiwa kidogo kwamba angeweza kweli kuwa Rais wa nchi.
Ni kweli kabisa kwamba alijitahidi bungeni kufichua mambo mengi ya oyvo yaliyokuwepo serikalini na alipogombea urais mwaka 2010, aliwagusa Watanzania wengi japo pia mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, alikuwa amepoteza mvuto aliokuwa nao kwenye uchaguzi wa mwaka 2005.
Ila amenichefua kwa namna anavyomsifia kwa muda sasa Rais Magufuli, ambaye baada tu ya kupitishwa na CCM, Dk. Slaa alimkebehi. Yaani kutokana na Lowassa kuchukua nafasi yake ndiyo amegeuka sasa kuwa mpiga debe wa Magufuli? Hiyo ni siasa gani jamani? Kuna mambo mazito ambayo angeweza kuyarejea kuonyesha jinsi Magufuli anavyovurunda. Mfano, kwenye mahojiano na gazeti moja la kila wiki mwezi Novemba 2014, Dk Slaa, alilaani vikali tukio la kufanyiwa vurugu, Jaji Joseph Warioba, na Paul Makonda na wenzake.
Alisema: "Siku mbili kabla ya tukio la vurugu nikiwa na viongozi na watu kadhaa wa heshima nilikutana na Paul Makonda. Nilimwambia siku damu ya Watanzania ikimwagika laana yake itakuwa juu ya kichwa chako kwa sababu wewe ni mnafiki.
“Mnaliangamiza taifa kwa ajili ya ushabiki, mnaparanganyisha taifa hili kwa sababu ya ushabiki, mnaliua taifa kwa sababu ya maslahi binafsi. Makonda haya mnayoyafanya ni kwa ajili ya maslahi yenu na si kwa sababu ya Katiba, nilimwambia hivyo, baada ya siku mbili zikatokea vurugu katika mdahalo ule."
Leo hii angewasaidia Watanzania kwa kurudia kwa ukali maneno yake kufuatia uteuzi wa Makonda huyohuyo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Na vilevile sasa naweza kuelewa vizuri kwanini alikuwa hataki kurudisha kadi yake ya CCM. Kwenye mahojiano hayohayo alitetea kuendelea kumiliki kadi ya CCM huku akiifananisha na cheti cha ndoa. Kwa maoni yangu, haiwezekani kweli mtu uendelee kumiliki kadi ya chama cha siasa kama moyoni huna mapenzi na kile chama.
Kinachojitokeza hapo ni uCCM B au kama ilivyokuwa nchini Kenya wakati wa Rais wa zamani, Daniel Arap Moi, CCM ni Baba na Mama. Na pengine isishangaze sana maana alihamia CHADEMA baada tu ya kufanyiwa mizengwe na CCM jimboni Karatu 1995.
Kama taifa hatuna budi kutazama upya suala la vyama vyetu vya siasa maana mfano Dk Slaa baada ya kuingia CHADEMA mwaka 1995, endapo angekuta hicho chama hakitimizi matarajio yake, angehama tena na tena? Au hata kwenye uamuzi mzito wa CHADEMA kumuunga mkono Mrema na baadaye Lipumba, yeye Dr Slaa alikubaliana kweli?
Niende sasa kwenye tukio kubwa kabisa la kumpokea Lowassa. Tofauti ya kwanza na Mrema ni kwamba Lowassa alikuwa Waziri Mkuu wakati Mrema alikuwa Naibu Waziri Mkuu. Angalau yeye Mrema hakusubiri jina lake kukatwa ndani ya CCM. Bila shaka Mrema alisoma alama za nyakati na kuona bora atimkie zake upinzani mapema. Yeye Lowassa alijifanya CCM damu damu kumbe shida yake ilikuwa kwenda Ikulu.
Kabla ya kumzungumzia Lowassa, sina budi niwakumbushe wasomaji jinsi miaka miwili mitatu kabla ya uchaguzi mkuu, Mbowe, alitangaza kwamba wamejifunza kutokana na kuchukua watu kadhaa kugombea vyeo fulani dakika za mwisho na kuleta usumbufu baadaye. Aliweka wazi safari ijayo hawataki 'makapi' ya CCM. Heko kabisa!
Sasa cha ajabu kabisa ni maneno aliyotamka juu ya Lowassa kuelekea mchakato wa urais kuanza ndani ya CCM: "CCM wanajidanganya, Lowassa ni dhaifu sana, amekaa serikalini zaidi ya miaka 30 na hakuna maendeleo yanayoonekana ndani ya serikali zaidi ya kila siku wizi na ubadhirifu kuongezeka.
“Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua watanufaika binafsi akipita kwenye urais, lakini kimsingi huyu jamaa ni dhaifu sana na hafai kuongoza Tanzania ya sasa yenye changamoto lukuki. Wapambe wake wanasema Lowassa si msemaji bali mtendaji, hivi nani atakubali porojo hizo wakati tunajua akiwa Waziri Mkuu hakufanya lolote kukemea wizi, ubadhirifu na ufisadi? Richmond ilikuja akiwa wapi?
"Sina ugomvi wala simchukii Lowassa binafsi, lakini ni vema hawa wanaosema ni mtu wa maamuzi magumu wakaueleza umma wakati watendaji wa serikali wakitafuna mabilioni ya fedha, CCM wakipitisha Katiba Inayopendekezwa ya ovyo pale Dodoma, yeye alisema au kufanya nini?"
Isitoshe sasa. Kufuatia kukatwa kwa Lowassa, katika kile kilichoonekana kwangu kama kumsafishia njia Lowassa kuingia CHADEMA, Mwenyekiti wa chama hicho alitamka maneno ya hatari mno tarehe 21 Julai 2015: "CHADEMA haimzuii mtu kujiunga kwani CHADEMA kuna kila aina ya wanachama - kuna vibaka, majambazi, wezi, wachawi, wala rushwa, mafisadi na wengineo.
“Hiki ni chama cha siasa, kina jumuisha watu wengi, siwezi kusimama na kusema wanachama wa CHADEMA wote ni wasafi, itakuwa si kweli, hivyo anayetaka kujiunga na chama chetu anakaribishwa ila lazima kuzingatia kanuni na maadili ya chama."
Na siku ya kumpokea Lowassa CHADEMA, Mbowe alitafuta kila aina ya maneno kuonyesha kwamba alichokisema juu ya Lowassa akiwa ndani ya CCM ilikuwa ni kucheza na akili ya viongozi wa CCM.
Binafsi kama mtu ambaye nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuisaidia CHADEMA kwa hali na mali kupitia wanachama wake wachache makini, nimelazimika kutamka walichokifanya viongozi wa CHADEMA kwa wananchi ni kosa la jinai la kisiasa ambalo pengine halisameheki. Kwa wale wapenzi wa mpira wanaweza kumbuka jinsi ambavyo timu mmoja wa mpira wa miguu kwenye Ligu Kuu ya Uingereza ilivyokuwa inaelekea kuchukua ubingwa baada ya zaidi ya miaka ishirini kama isingekuwa uzembe wa hali ya juu kwa upande wa mabeki wa timu hiyo.
Kocha mkuu alifikia kuuita uzembe huo jinai. Haiwezekani kuchezea maisha ya wananchi waliowachoka CCM kwa kuwapelekea watu walewale ambao hawakuwahi kutetea maslahi yao, mfano rasimu ya Katiba iliyobeba maoni yao. Kama si jinai la kisiasa sijui ni nini tena? Ni huyohuyo Lowassa aliyechelewesha upatikanaji wa Katiba bora kutokana na yeye kutumia ushawishi wake ndani ya bunge kuzuia mabadiliko makubwa.
Na ndio maana hata leo akizungumzia kwa mbali suala la Katiba, kwake ni kwa ajili tu ya kupata tume mpya ya uchaguzi na si uhai wa taifa. Hata kutetea suala la mgombea binafsi hawezi.
Na hapohapo viongozi wa CHADEMA walikuwa mstari wa mbele kumnukuu Nyerere kila uchao kwamba "upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM". Mara wanakimbilia kutoa mifano ya nchi nyingine kama Kenya walivyofanikiwa kuing'oa chama tawala. Si rahisi hata kidogo wanavyofikiri wao. Niwaeleze kidogo historia ilivyokuwa kwa jirani zetu.
Ukiangalia kwa haraka, Mzee Mwai Kibaki ni mtu ambaye historia yake ni ya kutukuka tangu anasoma Chuo Kikuu cha Makerere. Yaani ni mtu ambaye alionekana kama asingeingia kwenye siasa ambayo ilikuwa wito wakati huo, basi kwenye taaluma yake ya uchumi angefika mbali sana, mfano kuwa hata Rais wa Benki ya Dunia.
Na si mwingine bali Robert McNamara aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, aliyetamka takriban miaka arobaini iliyopita kwamba "Kibaki alikuwa miongoni mwa watu wachache sana mwenye upeo wa juu sana kuhusu masuala ya uchumi barani Afrika".
Mara jarida maarufu duniani la Time, lilimtaja zamani sana miongoni mwa watu 100 duniani ambao wangefika mbali kwenye uongozi. Vilevile huyu ni mtu ambaye alitumikia nchi yake kama Makamu wa Rais vizuri na bila doa. Na alifikia mahali alijitoa KANU na kuanzisha chama chake cha DP.
Na kutokana na ushindani mkali nchini Kenya, ilimchukua mara tatu hadi anafanikiwa kuwa Rais. Wakati wote huo hakuyumba na alizidi kujijenga miongoni mwa makundi mbalimbali ya kuheshimika.
Haya tukienda nchini Zambia, Frederick Chiluba katika miaka yake 17 ya uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Zambia (ZCTU), alikuwa mtetezi mkubwa wa wafanyakazi kiasi cha kuwekwa kizuizini na serikali ya Rais Kenneth Kaunda mwaka 1981, akituhumiwa kuchochea madai ya hali bora ya wafanyakazi.
Si chini ya mara mbili serikali ya Kaunda ilijaribu sana kumpatia nafasi serikalini bila mafanikio. Kwa kweli alijitahidi mno kuonyesha msimamo thabiti kwenye masuala ya msingi. Haishangazi basi kwamba Waziri maarufu wa zamani, Vernon Mwaanga, anamwelezea vizuri sana Chiluba kwenye kitabu chake walipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 1974, mjini New York, kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Anaeleza jinsi alivyovutiwa mno na uelewa wake wa masuala ya msingi. Anasema vilevile kwamba alikuwa mtu aliyesimamia nidhamu, kanuni na utekelezaji wa ratiba juu ya mambo ya umma. Niongeze kwamba kufuatia kuruhusiwa kwa vyama vyingi mwishoni mwa 1990, chama cha MMD kilichagua Halmashauri Kuu ya Kwanza, kikiongozwa na Chiluba kama Rais na Marehemu Levy Mwanawasa, Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa Taifa alikuwa Elias Chipimo na Katibu Mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Godfrey Miyanda, kutaja tu majina machache maarufu. Ni vizuri kusema kwamba kwenye nafasi ya Makamu wa Rais, Mwanawasa aliwashinda washindani wake wawili, Luteni Jenerali Christon Tembo na Baldwin Nkumbula.
Zaidi ya hilo, lilipofika suala la mgombea Urais, wanachama wazito walichuana kama Arthur Wina, aliyekuwa Waziri wa kwanza wa Fedha na Humphrey Mulemba ambaye pia aliwahi kuwa Makamu wa Rais na Chiluba mwenyewe ambaye aliibuka mshindi.
Kwa kweli jinsi walivyochuana ilikuwa hatua ya kupongeza. Kilichofuata kilikuwa ushindi wa kishindo kwa MMD dhidi ya chama tawala cha UNIP.
Safari ya Ikulu si rahisi hata kidogo. Hata Rais Barack Obama pamoja na kutokuwa na uzoefu mkubwa kwenye siasa, alikuwa amejipambanua kiasi cha kuwa mtu wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Jarida la Sheria kwenye chuo chake mashuhuri cha Havard.
Kuhitimisha, uchaguzi uliopita wa kuingia Ikulu kwa gharama yoyote ulijaa joto bila mwanga. Sijapata kuona mgombea urais wa upinzani duniani akikwepa mdahalo, wala hata mahojiano ya maana juu ya masuala mazito ya nchi.
Na matokeo yake, Magufuli ameweza kupata umaarufu ndani na nje ya nchi usiokuwa wa maana kabisa. Kuna masuala mengi kabisa ambayo mwanasiasa yeyote wa kawaida tu hapa Afrika angemshugulikia kikamilifu Magufuli tangu wakati wa kampeni.
Mifano ni suala la Zanzibar; nyumba za Serikali zilizouzwa wakati yeye akiwa Waziri; akisema kwamba Watanzania wote wanamuunga mkono Odinga na ambayo viongozi wa CHADEMA wangenisikiliza vizuri tangu zamani ilibidi Magufuli ajiuzulu.
Pia, kufutilia mbali sherehe muhimu za siku ya Uhuru bila hata kushauriana na baraza la mawaziri; mali za viongozi wa umma kujulikana pamoja na mishahara; uteuzi wa Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kihistoria cha Dar es Salaam;
Masuala ni mengi mno.
Kwa miaka mingi nchi yetu imelilia sana kuwa na upinzani wa kweli na kama ambavyo alivyopenda kusema mwanasiasa mmoja nchini Uingereza, marehemu Charles Kennedy, "British Politics is up for grabs". Hivyo hivyo "Tanzanian Politics is up for grabs". Who are the takers? (Nani wa kuchukua nafasi?)
Makundi yote tuungane angalau kupata chama kinachoweza kusimamia demokrasia ya kweli na pia Katiba Mpya ili tuingie kwenye Jamhuri ya Pili! -
Raia Mwema