Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 672
Nimechoshwa na barua za ngono-Lowassa
2007-12-16 10:13:40
Na Lulu George, PST Tanga
Waziri mkuu, Bw. Edward Lowassa, amesema amechoshwa na kupokea barua zinazotumwa ofisini kwake zikihusisha malalamiko ya kuwepo kwa vitendo vya ngono kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Bw. Lowassa alisema hayo kwenye kikao cha Watendaji Wakuu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, hapa.
Alisema kwa ujumla mkoa wa Tanga una Halmashauri mbili ambazo hazimfurahishi kiutendaji kutokana na kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa, uzorotaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.
``Jamani kuna baadhi ya Halmashauri mkoani hapa hazinifurahishi hata kidogo, kila siku ni malumbano...kama Muheza napokea barua kila mara ofisini kwangu, shutuma zinazotolewa ni za ngono tu...hivi mna matatizo gani...hii hali inatisha na tayari nimeshamkabidhi Waziri wa TAMISEMI alishughulikie suala hili,`` alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa amepata taarifa kwamba kuna baadhi ya Madiwani katika Halmshauri za mkoani humo wamekuwa na tabia ya kuwadanganya wananchi wasichangie shughuli mbalimbali za maendeleo na badala yake waiachie Serikali kutekeleza majukumu hayo, jambo ambalo alilisema kuwa ni kinyume na taratibu za uongozi.
``Mchana mnapita changieni ujenzi wa shule wananchi...,lakini usiku, ninyi ninyi mnawaambia tena wananchi, acheni Serikali itafanya; hivi mpo hapa kwa maslahi ya nani...? yenu au ya wananchi, nawaambia hivi baada ya miaka mitano, hao hao ndio watakaowageuka kwani wameshawatambua kuwa mnawafanya wajinga...,tabia hii ni mbaya viongozi wenzangu,? alisisitiza.
Aidha, alikemea tabia ya baadhi ya Maofisa Watendaji wa Kata kujifanya ni miungu watu na kwamba wamekuwa wakitumia nguvu kwa kuwakamata wananchi bila kufuata sheria zilizopo kwa kuwatuhumu kuwa hawataki kutoa michango ya maendeleo. [/B]``Hii tabia ya kamatakamata si nzuri na siipendi kabisa kwanini hamtumii hamasa sana kuliko kukimbilia kutumia nguvu...zipo sheria ndogondogo katika maeneo yenu zitumieni sio kujifanya wababe tu kwa kila kitu...maendeleo yanakuja kwa kushawishiwa sio kutumia nguvu..tabia hii ife mara moja``,alisema.
Bw. Lowassa aliwataka Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasimamia vizuri kama walivyoahidi kwa wananchi katika utekelezaji ya ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2005 katika nyanja ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
``Kumbukeni katika uchaguzi tuliwaambia wananchi kuwa tutahakikisha katika kila kata kuwe na shule moja ya Sekondari...sasa hii habari ya ninyi kuwa wakusanyaji wa pesa naomba muwaachie watendaji na jukumu lenu ninyi liwe ni usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi sio kung?ang?ania kushika risiti tu``,alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema ni dhahiri kuwa Halmashauri ya Jiji la Tanga ina vyanzo vingi vya Mapato iwapo itajipanga vizuri badala ya kubaki na visingizio kuwa inakabiliwa na umaskini jambo ambalo limechangia katika suala zima uzoroteshajia kwenye ujenzi wa madarasa na hivyo kutofikia lengo lililopangwa na Serikali kwa asilimia angalau 80 ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na masomo ya sekondari hapo mwakani.
``Nimekuja Tanga kuzungumza na ninyi leo kwa sababu dalili za elimu haziendi vizuri...hata asilimia iliyopangwa hamtaifikia jamani sikusudiii kuita mtu Dar es Salaam ila ikinilazimu nitafanya hivyo...mko nyuma sana kielimu na inanisikitisha,`` alisema.
SOURCE: Nipashe