mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Nukuu ya Rais Magufuli => ''Ole wake mtu aende akawazuie hawa vijana wanaolima ndipo ataona ''obwato bufa amagoba''
Tafsiri: obwato bufa amagoba - Mtumbwi uharibika unapofika
Rais Magufuli akiwa Kyaka Jimbo la Nkenge amepiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi wanaolima. Ataka vijana hao waungwe mkono. Ni baada ya kupokea kero ya kijana Rosh Omary amabaye amelalamika kuwa afisa mifugo amefyeka mazao yake kando ya mto Nkenge Kyaka.
Rais Magufuli katika ziara yake Nkenge Kyaka Mkoani Kagera baada ya kusikiliza kero za vijana rais ametoa maagizo haya;
"Mimi najua mkuu wa wilaya yuko wapi? Kasimimie hili. Hakuna kufukuza vijana hawa wanaofanyakazi. Waache walime, wakilima mpaka kwenye mto ili maji yakija yatachukua mazao yao, wao waache walime. Waache wafanye biashara watengeneze mali zao."
Habari zaidi, soma=>Pwani: Serikali yafyeka mazao yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu ndani ya Mita 60 - JamiiForums