Kyaka, Kagera: Rais awapiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi kulima kandokando ya mito

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113

Nukuu ya Rais Magufuli => ''Ole wake mtu aende akawazuie hawa vijana wanaolima ndipo ataona ''obwato bufa amagoba''

Tafsiri: obwato bufa amagoba - Mtumbwi uharibika unapofika

Rais Magufuli akiwa Kyaka Jimbo la Nkenge amepiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi wanaolima. Ataka vijana hao waungwe mkono. Ni baada ya kupokea kero ya kijana Rosh Omary amabaye amelalamika kuwa afisa mifugo amefyeka mazao yake kando ya mto Nkenge Kyaka.

Rais Magufuli katika ziara yake Nkenge Kyaka Mkoani Kagera baada ya kusikiliza kero za vijana rais ametoa maagizo haya;

"Mimi najua mkuu wa wilaya yuko wapi? Kasimimie hili. Hakuna kufukuza vijana hawa wanaofanyakazi. Waache walime, wakilima mpaka kwenye mto ili maji yakija yatachukua mazao yao, wao waache walime. Waache wafanye biashara watengeneze mali zao."

Habari zaidi, soma=>Pwani: Serikali yafyeka mazao yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu ndani ya Mita 60 - JamiiForums
 
View attachment 625921
Rais Magufuli akiwa na mkulima aliyeharibiwa mazao yake
Rais Magufuli akiwa Kyaka Jimbo la Nkenge amepiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi wanaolima. Ataka vijana hao waungwe mkono. Ni baada ya kupokea kero ya kijana Rosh Omary aliyefyekewa mazao yake kando ya mto Nkenge Kyaka Mkoani Kagera
Amsaidie na mbowe aliyefyekewa mazao yake
 
Wakisha haribu vyanzo vya maji na ukame ukatamalaki anaanza kuwaambia kuwa serikali haijazuia mvua.

Na pia hapo ameonyesha kuwa tukio la mbowe ni mwendo wa visasi, siyo makosa ya kulima kando ya mto.
 
Rais Magufuli akiwa Kyaka Jimbo la Nkenge amepiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi wanaolima. Ataka vijana hao waungwe mkono. Ni baada ya kupokea kero ya kijana Rosh Omary aliyefyekewa mazao yake kando ya mto Nkenge Kyaka Mkoani Kagera

Hayo maagizo ni kwa nchi nzima au kwenye jimbo hilo tu?
 
Hapo hapo ndio anavyokuza double standard.....tamko lake linatawala Tanzania nzima....NEMC wajipange!!! Ole wao....na kilugha tuta copy.....ole wao!!! Awamu hiii.....mihemko haswaa
 
Rais Magufuli katika ziara yake Nkenge Kyaka Mkoani Kagera baada ya kusikiliza kero za vijana rais ametoa maagizo haya;

"Mimi najua mkuu wa wilaya yuko wapi? Kasimimie hili. Hakuna kufukuza vijana hawa wanaofanyakazi. Waache walime, wakilima mpaka kwenye mto ili maji yakija yatachukua mazao yao, wao waache walime. Waache wafanye biashara watengeneze mali zao."
 
Jamani hi kauli ya rais huko Bukoba naona kama alikuwa inamlenga mtu...ina maana hakujutia ?

"unamtafuta nyoka unamgonga kichwa akikimbia bahati yake we unaendelea na kulima"- Mwisho wa kunukuu
aliongea katika context ipi, tuwekee maana si rahisi hapo kufanya any speculation, itakuwa wrong with no base.. linkage si rahisi hapo kuipata
 
Huyo nyoka hana madhara tena kwake lakini ipo siku atajichanya na ndio itakuwa mwisho wa maisha yake!
 
Back
Top Bottom