Kwq mtazamo wa Kaunga

Kwq mtazamo wa Kaunga

Kumbe ndugu yangu tuna experience inayofanana , hata nami nimeishi na hawa wamama tofauti tofauti mziki wao naujua asikwambie mtu . Lkn kupitia maisha yale yamenisaidia kujifunza mambo mengi kuhusu wanawake, huko nyuma nilikua nawalaumu sana . Ninapoandika hapa sina kinyongo kabisa na wale wamama nilishawaachilia manake niliwabeba moyoni mwangu. Nilijifunza kuangalia mazuri yao hata kama machache yanatosha kunipa faraja.

Na huku ndiko kukua ...!!!!!!!!!
 
Hapa tatizo kubwa linaanzia kwenye malezi

Kitendo cha mama kumchukia mtoto wa kambo sijui ni wivu kwa mumewe au ni kitu gani maana akina mama hugeuka wanyama kwa hawa watoto

Labda huenda kuna siku tunaweza kujua sababu lakini hili ni janga kubwa...!!!!
Tumuombe Mungu huenda kuna siku tutajua kwanini wanawake wako hivi. Point ya kwanza hapo juu nafikiri ndio ya msingi kwani malezi yanachangia kwa kiasi kikubwa tabia ya mtu. Kwa mfano tunaona kama mama haelewani na mama mkwe wake basi hata binti aweza asielewane na mkwewe pindi atakapoolewa. Sasa malezi yana nafasi kubwa kwenye maisha yetu.

Hili ni janga.
 
Da Kaunga hii ni mada nzuri sana. Ninaomba niivutie kasi nitarudi. Kaka PakaJimmy umenigusa sana kwa post yako hapo pa mwanamke anayedai kubadilisha majina baada ya mume kufariki (Hii ni mada ya peke yake wapendwa) na hapo pa kutupa watoto natamani kama tungekuwa tunao uwezo wa kuassess na conscious ya huyo mama atupaye mtoto wake kutokana na kukosa mwelekeo ................. huwa anajisikiaje, je akishamtupa huwa anasahau na kufurahi au huwa anabaki na guilty daima? (Najua wapo wale ambao wanadhamiria kutupa - mie siwazungumzii hao) Nway hii ni mada nyingine ambayo ningefurahi sana kama ingepata mtu wa kuitengeneza vizuri na kuipost.
 
Last edited by a moderator:

Usiache kurudi, mada hii ilipata wachangiaji wachache nafikiri wengi hawakuielewa maana nina poor presentation skills; lkn pia ni ngumu na inahitaji kutulia na kuwa mkweli (si mnafiki hasa kwa wamama).
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom