Kwq mtazamo wa Kaunga

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Baada ya kutafakari kwa kina na kwa muda mrefu na hasa baada ya tuhuma nyingi na za mara kwa mara kwamba wanawake tuna roho mbaya ndio maana tunapokuwa mama wa kambo twawatesa au hatuwatreat sawa watoto wetu wa kambo; nimekuja na vitu hivi.
wanaume hawana bond kubwa na watoto kwakuwa hawajabeba mimba wala kuwanyonyesha hao watoto tofauti na wamama.
Mwanaume anatambulishwa mtoto tofauti na mwanamke ambaye anamjua mwanaye.
Kitokana na hali hizo, ndio maana:-
1. Mwanaume anaweza mtunza vizuri mtoto wa mkewe alomkuta naye, kwani hakuna tofauti kubwa sana na yule ambaye amemshuhudia akizaliwa maana bado anaweza asiwe wake pamoja amelea mimba.
2. Mwanaume anaweza telekeza watoto wake na asipate shida sana (ingawa kuna wamama wachache sana nao hutelekeza watoto)

NB: lengo langu si kutetea au kusupport ouvu wa baadhi ya wamama watesao watoto wa kambo, ninajaribu kuwaelewa au kuielewa tofauti ya wamama na wababa ili kuboresha tu.
 
Last edited by a moderator:
Juzi nilikuwa msibani Marangu Moshi, wakati wa kutoa salamu mbalimbali Mwanamke mmoja(nadhani ni mwanaharakati) alisimama mbele ya umati na kusema kuwa wanawake wamechoka kuendelea na majina ya marehemu-waume zao, wanataka sasa mke arudie jina lake la awali mara baada ya mumewe kufariki, maana hakuna ndoa tena!
Mimi pamoja na watu wengine ambao ni sensitive tuliachwa midomo wazi!

Hapo nilikuwa najaribu tu kuonyesha jinsi wanawake walivyo na hisia kali za ndani kwa ndani juu ya vitu ambavyo mwanaume waweza kuona vya kawaida!

Nimalizie kwa kusema wanawake hawana strong bond na watoto wao, wanalazimika kuwa karibu na watoto kutokana na natural cause ya wao kuwa ndio wanaozaa. Nasema hivi kwasababu wanaongoza kutupa watoto WAO WENYEWE majalalani, vyooni na mitaroni kwa kukosa upendo...worse huwa wanatupa mtoto wake wa kuzaa, na si wa kambo...strong bond ya wapi hiyo?!
 
ni kweli dada Kaunga ukisemacho ila labda ilitakiwa maelezo yako yabase kwenye ukweli wa kwamba wababa mara nyingi hawana ukaribu na watoto wao au hwapati presha kama wamama wanavyopata presha watoto wao wanapopatwa na matatizo kama aksidenti,kuchelewa kurudi nyumbani au hata kuumwa kwa sababu ulizozianosha hapo juu,kwa sababu kwa maelezo yako yaliyotangulia ni kama vile unajaribu kutetea utesaji japo hapa mwishoni umekiri kuwa hilo si lengo lako.
 
Last edited by a moderator:
Mi hata sijaelewa nini kinaongelewa hapa..... Bond, mtoto, wanaume, wanawake... Wai!!
 

Unajua nini, hiyo natural cause ndio yasababisha hiyo bond.
Halafu kingine ni nini, baba kutelekeza watoto kwa kisingizio chochote haimake headlines kama vile mama kutupa mtoto; hivyo usihadaike na unachosikia kwa sana maana kungekuwa na takwimu na l hope watu wa sociolojia wanaweza fanya tafiti kulinganisha idadi ya wamama waliotupa watoto na wababa waliotelekeza watoto.
 
Dada Kaunga, hapa panahitaji busara kidogo kujadili hili. Labda niwaombe wanaJF hebu hii thread itazame kwa jicho la tatu.
 

Sitetei kabisa utesaji na ninauchukia kwa kila cell yangu mwilini na ndio maana swali la WHY limekuwa likirindima kichwani mwangu, nilichofanya pia ni kujiuliza WHY kina baba hawana hiyo tuhuma au hiyo shida sana; of course you are right kwakuwa muda mwingi hawako na watoto lkn mbona na wamama wengi siku hizi wameajiriwa au kujiajiri hivyo kutokuwa nyumbani.
Najua issue complex kama hii haiwezi sababishwa na sababu moja au mbili ndio maana nimejaribu kuzama zaidi. Imagine wababa wangapi wanakataa mimba kwa kusema ataaminije kama ni wake, pia angalia wangapi wanawatunza watoto wa wake zao as if na sometimes (kama mtoto ana adabu kuliko wa kwake) kuliko wa kwake? Lkn sisi wamama hata mwanao akiwa mkorofi, bangi etc utahangaika naye na pengine kuzidi kumspoil na kumnyima au kumpunja support kijana mzuri na mstaarabu wa mumeo?
 
Last edited by a moderator:
Dada Kaunga, hapa panahitaji busara kidogo kujadili hili. Labda niwaombe wanaJF hebu hii thread itazame kwa jicho la tatu.

I hope wanaJF hawatadhani nasupport unyanyasaji in anyway.
Mimi nina amini ili utatue tatizo lazima ulichimbe kiundani kuufukua mzizi wa tatizo na sio kudeal na dalili tu au matawi ukitumia mfano wa mti.
 
Point.......umemaliza mkuu sina nyongeza!
 

nadhan tusitoke nje ya mada tukianza kulinganisha habari ya ukatili kwa watoto sijui nani anaongoza hatutafika matokeo yake tutajikuta tunajadili kiushabiki tu......lakini nadhan mada hii ni nzuri na inalengo nzuri ya kutaka kujenga so tusiitie najisi mapema ...
 
Mi hata sijaelewa nini kinaongelewa hapa..... Bond, mtoto, wanaume, wanawake... Wai!!

Aiseee kumbe na wewe tupo pamoja mkuu

Mimi sielewi kabisa hapa
Hebu Kaunga njoo hapa utueleweshe ni kitu gani umelenga hapa!!
 
Last edited by a moderator:
kwani na ww mama yako alikutupa?
Jamaa kama umemuelewa kwamba bond ya mama kwa mtoto ni kwa sababu amemzaa tu ndo maana kama hakumzaa kwa hiari yake atamtupa
 
Eiyer kapate lunch kwanza halafu nishati ikipanda upstairs utanielewa naongelea nini.
 
Last edited by a moderator:


Bond baina ya mama na mtoto si ndio ingesababisha akina mama wawapende watoto zaidi au??
 
Eiyer kapate lunch kwanza halafu nishati ikipanda upstairs utanielewa naongelea nini.

Sijakuelewa bana

Kama wakina mama ndio wanaopata uchungu,si ndio wanapaswa kuwa na uchungu zaidi na watoto?
Inakuwaje watu ambao hata hawajui uchungu wa kujifungua ndio wawe rahisi kulea bila tatizo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…