Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Mimi ni baba wa mtoto mmoja, sina uzoefu na kulea watoto aidha nasaidiwa sana na wanaJF katika kujua baadhi ya mambo yanayomhusu mtoto.

Nakili nilienda clinic katika moja maeneo ninayoishi niliona saver was interested na maswali niliyokuwa nammuliza aidha pangine aliona nampotezea muda au nae hajui.

Mwanangu kwa sasa anasumbuliwa na kwikwi ya mara kwa mara.

Je, kwikwi husababishwa na nini?

Nimepewa njia za kuweza kuzuia ikiwemo kukilowesha kinyuzi cha nguo kwa mate na kukiweka katika paji lake la uso na kumpaka wanja, yote nimefanya lakini bado naona tatizo linaendelea.

Msaada...

2.
Mke wangu amejifungua siku 16 zilizopita na mtoto anaendelea vizuri tu,hana tatizo kubwa zaidi ya hili linalonipa maswali.Anapata kwikwi mara kwa mara,ambayo hudumu kwa takribani dakika 10-15 then inaisha.

Swali langu ni kwamba hii hali na kawaida?

Je, is it necessary for a kid kupata kwikwi yaani hawezi kuishi bila hii kitu? na kama anaweza, what should be done ili niiondoe kabisa?

Naomba msaada.

--------------MICHANGO-----------------

Kwikwi huwapata watoto hata kabla hawajazaliwa wakiwa matumboni mwa mama zao!

Hutokana na mfumo mzima wa kupumua kwa mtoto.Ni kitu cha kawaida katika ukuaji wa mtoto.

Cha kufanya ni kumfanaya mtoto apitishe muda katika hali ya raha ( comfort) kwa kumnyonyesha au kumbembeleza.BTW mtoto hubembelezeka kwa urahisi zaidi kwa kunyonya.

Imani nyingine kama kumwekea uzi kwenye paji la uso haziondoi kwikwi.

Njia pekee ni kuvuta subira na muda unapita na kwikwi kusha yenyewe.

Pole sana,ni suala common kwa watoto wachanga hasa wa kwanza(usiniulize takwimu)
Inasemekana sababu kubwa ni kunyonya 'hewa'.

Hii huchangiwa na position ya mtoto wakati wa kunyonya kuacha nafasi ya kuingiza 'hewa' kinywani.

Pia wengine wanasema overfeeding inaweza kupelekea hali hii.

Cha kufanya...
Muone daktari/mkunga aliyebobea kwenye maswala ya watoto wachanga/unyonyeshaji anaweza kukusaidia.
 
Pole Kichwa Ngumu....usitishike, kwikwi (hiccup) ni kitu cha kawaida kwa watoto wadogo, especially wachanga..ni kama 'reflexes' (sijui kiswahili chake samahani) zinazotokea sababu ya kutokomaa kwa viuongo vya ndani vya mtoto. Kwa hiyo mtoto anapokuwa na kukomaa, basi kwikwi zinapungua pia. Inaweza zikadumu kwa kuanzia dakika chache mpaka masaa kadhaa.

Kitabibu, hakuna tiba ya moja kwa moja ya kwikwi kwa mtoto...kuna vitu vingi watu huwa wanafanya (baadhi ndio ulivyofanya wewe) lakini huwa havisaidii. Lakini kujaribu kum'distract' mtoto wakati ana kwikwi kwa kumvutia na kitu kingine mfano chenye rangi za kuvutia au kinachotoa sauti flani hivi kupata attantion ya mtoto inaweza saidia.

NB: Mara nyingi mtoto anapopata kwikwi ni wazazi/walezi ndio wanaosumbuka...lakini si mtoto, kwani kwikwi haimsumbui mtoto!
 
Riwa hata mimi nakubaliana na wewe and I have taken that one
 
Oooh! your very helpfull thnx a lot
 
Binafsi sijui tiba permanent lakini mtoto wangu anapo pata tatizo la kwikwi, wife huwa anakata kipande cha uzi, analowesha na mate kisha anambandika mtoto usoni.
Amazing!! kwikwi inaisha.
 
Nilikuwa makini kupata uwelewa kidogo hapo kwa sababu natarajia kupata mtoto hivi karibuni uenda hayo pia yaweza nikuta.
 
Kwiki ni tatizo linalowapata sana watoto wachanga ingawaje na watu wazima pia. Nimeona link hii ambayo ukifungua unaweza kuona njia mbali mbali za kutibu/kuzuwia bila ya kumwona daktari.
Waswahili tumezowea kumwekea mtoto mchanga uzi uliloweshwa kwa mate, lakini kipande kidogo cha barafu kinasaidia pia, na kina uwezo kuliko uzi. Jengine tunachofanya ni kumshitua mtoto lakini sikushauri, hujui atashituka kiasi gani, usije ukaongeza tatizo jengine.
Lakini tatizo likizidi, muone daktari.
Kwenye link bonyeza kwenye kila moja ya viunganishi vikuu: Introduction, Causes, Diagnosis na Treatment:
Hiccup - NHS Choices
Kwa mtu mzima, ziko njia rahisi:
1. Bugia kijiko cha chai cha sukari nyeupe
2. Kunywa maji baadae.
3. Tafuna kipande cha mkate
4. Chukua mfuko wa karatasi, weka mdomoni na puliza na vuta pumzi mara kadhaa.
Ikiwa bado kwikwi itaendelea rejea hatua hizo mara mbili tatu na itaisha.
Pole sana na matatizo Mkuu.
 
Kunywa maji pia hua kunaondoa kwikwi!Kwa mtoto mdogo dumbukiza kidole chako kwenye maji alafu umdondoshee matone kama bado hajafikia umri wa kuhitaji maji ya ziada!Kama ameanza mchotee na kijiko!Nimewahi kujaribu kwa mtoto na inafanya kazi!
 
mimi ni baba wa mtoto mmoja sina uzoefu na kulea watoto aidha nasaidiwa sana na wana JF katika kujua baadhi ya mambo yanayomhusu mtoto.
nakili nilienda clinic katika moja maeneo ninayo ishi niliona saver was interested na maswali niliyokuwa nammuliza aidha pangine aliona nampotezea muda au nae hajui.
mwanangu kwa sasa anasumbuliwa na kwiki ya mara kwa mara.
je, kwiki husababishwa na nini? nimepewa njia za kuweza kuzuia ikiwemo kukilowesha kinyuzi cha nguo kwa mate na kukiweka katika paji lake la uso na kumpaka wanja yote nimefanya lakini bado naona tatizo linaendelea.
msaada plz

Hapo kwenye nyekundu nimeshaona wazazi wengi wakiitumia sana hiyo kwa watoto waliobanwa na kwikwi na wengine huwa wanawapa matone ya maji kama bado ni wachanga sana labda matatu au manne hivi ili kuwasaidia.
 
Kwiki ni tatizo linalowapata sana watoto wachanga ingawaje na watu wazima pia. Nimeona link hii ambayo ukifungua unaweza kuona njia mbali mbali za kutibu/kuzuwia bila ya kumwona daktari.
Waswahili tumezowea kumwekea mtoto mchanga uzi uliloweshwa kwa mate, lakini kipande kidogo cha barafu kinasaidia pia, na kina uwezo kuliko uzi. Jengine tunachofanya ni kumshitua mtoto lakini sikushauri, hujui atashituka kiasi gani, usije ukaongeza tatizo jengine.
Lakini tatizo likizidi, muone daktari.
Kwenye link bonyeza kwenye kila moja ya viunganishi vikuu: Introduction, Causes, Diagnosis na Treatment:
Hiccup - NHS Choices
Kwa mtu mzima, ziko njia rahisi:
1. Bugia kijiko cha chai cha sukari nyeupe
2. Kunywa maji baadae.
3. Tafuna kipande cha mkate
4. Chukua mfuko wa karatasi, weka mdomoni na puliza na vuta pumzi mara kadhaa.
Ikiwa bado kwikwi itaendelea rejea hatua hizo mara mbili tatu na itaisha.
Pole sana na matatizo Mkuu.

Hiyo kwa watu wazima tunafanya hayo yote au mojawapo?
 
Samahani Mkuu nilikosea kufafanua. Hatua ya kwanza mpaka ya tatu (1-3) zinafuatana, hatua ya 4 inafanyika ama peke yake au baada ya hizo tatu kutofanya kazi. Kwa kwikwi ya muda tu, hatua 1-3 ni nzuri sana, lakini kwikwi ikiendelea, inawezekana mhusika anasumbuliwa na pumu pia kwa hivyo hatua ya 4 ni lazima.
 
Binafsi sijui tiba permanent lakini mtoto wangu anapo pata tatizo la kwikwi, wife huwa anakata kipande cha uzi, analowesha na mate kisha anambandika mtoto usoni.
Amazing!! kwikwi inaisha.

Hii hata mimi naijua, na inafanya kazi kabisaa..
 
Mke wangu amejifungua siku 16 zilizopita na mtoto anaendelea vizuri tu,hana tatizo kubwa zaidi ya hili linalonipa maswali.Anapata kwikwi mara kwa mara,ambayo hudumu kwa takribani dakika 10-15 then inaisha.

Swali langu ni kwamba hii hali na kawaida?

Je, is it necessary for a kid kupata kwikwi yaani hawezi kuishi bila hii kitu? na kama anaweza, what should be done ili niiondoe kabisa?

Naomba msaada.
 
Duh pole sana for ur kid..ila usihofu hii kitu ni kawaida kwa watoto wengi wachanga, ni kawaida sana, mara nyingine huwa anastukastuka na kwikwi huanza! Sidhani kama ni tatizo kubwa, hapa sista angu mtoto akianza kwikwi anachukua uzi wa nguo kuna maji anapaka(hata ukipaka mate ni pouwa tu) halafu anamwekea kwenye paji ya uso katikati kwikwi inakwisha within short time!! Try that ukisubiri ushauri wa wengine!!
 
Thanx man..its my first experience,so i have to ask everything...noted
 
Duh pole sana for ur kid..ila usihofu hii kitu ni kawaida kwa watoto wengi wachanga, ni kawaida sana, mara nyingine huwa anastukastuka na kwikwi huanza! Sidhani kama ni tatizo kubwa, hapa sista angu mtoto akianza kwikwi anachukua uzi wa nguo kuna maji anapaka(hata ukipaka mate ni pouwa tu) halafu anamwekea kwenye paji ya uso katikati kwikwi inakwisha within short time!! Try that ukisubiri ushauri wa wengine!!
Nilimwona ma wife akifanyaga hivyo,nilidhani ni imani tu,kumbe wengi wanafanya hivyo!
 
Kwikwi huwapata watoto hata kabla hawajazaliwa wakiwa matumboni mwa mama zao!

Hutokana na mfumo mzima wa kupumua kwa mtoto.Ni kitu cha kawaida katika ukuaji wa mtoto.

Cha kufanya ni kumfanaya mtoto apitishe muda katika hali ya raha ( comfort) kwa kumnyonyesha au kumbembeleza.BTW mtoto hubembelezeka kwa urahisi zaidi kwa kunyonya.

Imani nyingine kama kumwekea uzi kwenye paji la uso haziondoi kwikwi.

Njia pekee ni kuvuta subira na muda unapita na kwikwi kusha yenyewe.
 
Hii myth ya uzi nadhani ipo kwa jamii nyingi saana niliwahi kuwasikia watu kutoka west Africa pia wakizungumza hili.

Kwikwi kwa watoto wadogo mara nyingi husababishwa na kushiba. Huenda anakuwa ameshiba saana. Kwahiyo hupaswi kuogopa.

Lakini ukiona inakuwa kero saana kwake, kanyonyeshwe hako ka-uncle mambo yanakuwa sawa.

Au kama kanatumia bottle, apewe hayo. Unaweza pia kuisearch kwenye net inaitwa hiccup kwa kidhungu.
 
Back
Top Bottom