Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba

Discussion in 'JF Doctor' started by Kichwa Ngumu, Mar 16, 2011.

 1. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi ni baba wa mtoto mmoja, sina uzoefu na kulea watoto aidha nasaidiwa sana na wanaJF katika kujua baadhi ya mambo yanayomhusu mtoto.

  Nakili nilienda clinic katika moja maeneo ninayoishi niliona saver was interested na maswali niliyokuwa nammuliza aidha pangine aliona nampotezea muda au nae hajui.

  Mwanangu kwa sasa anasumbuliwa na kwikwi ya mara kwa mara.

  Je, kwikwi husababishwa na nini?

  Nimepewa njia za kuweza kuzuia ikiwemo kukilowesha kinyuzi cha nguo kwa mate na kukiweka katika paji lake la uso na kumpaka wanja, yote nimefanya lakini bado naona tatizo linaendelea.

  Msaada...

  2.

  --------------MICHANGO-----------------

   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Pole Kichwa Ngumu....usitishike, kwikwi (hiccup) ni kitu cha kawaida kwa watoto wadogo, especially wachanga..ni kama 'reflexes' (sijui kiswahili chake samahani) zinazotokea sababu ya kutokomaa kwa viuongo vya ndani vya mtoto. Kwa hiyo mtoto anapokuwa na kukomaa, basi kwikwi zinapungua pia. Inaweza zikadumu kwa kuanzia dakika chache mpaka masaa kadhaa.

  Kitabibu, hakuna tiba ya moja kwa moja ya kwikwi kwa mtoto...kuna vitu vingi watu huwa wanafanya (baadhi ndio ulivyofanya wewe) lakini huwa havisaidii. Lakini kujaribu kum'distract' mtoto wakati ana kwikwi kwa kumvutia na kitu kingine mfano chenye rangi za kuvutia au kinachotoa sauti flani hivi kupata attantion ya mtoto inaweza saidia.

  NB: Mara nyingi mtoto anapopata kwikwi ni wazazi/walezi ndio wanaosumbuka...lakini si mtoto, kwani kwikwi haimsumbui mtoto!
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Riwa hata mimi nakubaliana na wewe and I have taken that one
   
 4. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Oooh! your very helpfull thnx a lot
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Binafsi sijui tiba permanent lakini mtoto wangu anapo pata tatizo la kwikwi, wife huwa anakata kipande cha uzi, analowesha na mate kisha anambandika mtoto usoni.
  Amazing!! kwikwi inaisha.
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa makini kupata uwelewa kidogo hapo kwa sababu natarajia kupata mtoto hivi karibuni uenda hayo pia yaweza nikuta.
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kwiki ni tatizo linalowapata sana watoto wachanga ingawaje na watu wazima pia. Nimeona link hii ambayo ukifungua unaweza kuona njia mbali mbali za kutibu/kuzuwia bila ya kumwona daktari.
  Waswahili tumezowea kumwekea mtoto mchanga uzi uliloweshwa kwa mate, lakini kipande kidogo cha barafu kinasaidia pia, na kina uwezo kuliko uzi. Jengine tunachofanya ni kumshitua mtoto lakini sikushauri, hujui atashituka kiasi gani, usije ukaongeza tatizo jengine.
  Lakini tatizo likizidi, muone daktari.
  Kwenye link bonyeza kwenye kila moja ya viunganishi vikuu: Introduction, Causes, Diagnosis na Treatment:
  Hiccup - NHS Choices
  Kwa mtu mzima, ziko njia rahisi:
  1. Bugia kijiko cha chai cha sukari nyeupe
  2. Kunywa maji baadae.
  3. Tafuna kipande cha mkate
  4. Chukua mfuko wa karatasi, weka mdomoni na puliza na vuta pumzi mara kadhaa.
  Ikiwa bado kwikwi itaendelea rejea hatua hizo mara mbili tatu na itaisha.
  Pole sana na matatizo Mkuu.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kunywa maji pia hua kunaondoa kwikwi!Kwa mtoto mdogo dumbukiza kidole chako kwenye maji alafu umdondoshee matone kama bado hajafikia umri wa kuhitaji maji ya ziada!Kama ameanza mchotee na kijiko!Nimewahi kujaribu kwa mtoto na inafanya kazi!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,105
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye nyekundu nimeshaona wazazi wengi wakiitumia sana hiyo kwa watoto waliobanwa na kwikwi na wengine huwa wanawapa matone ya maji kama bado ni wachanga sana labda matatu au manne hivi ili kuwasaidia.
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Hiyo kwa watu wazima tunafanya hayo yote au mojawapo?
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Samahani Mkuu nilikosea kufafanua. Hatua ya kwanza mpaka ya tatu (1-3) zinafuatana, hatua ya 4 inafanyika ama peke yake au baada ya hizo tatu kutofanya kazi. Kwa kwikwi ya muda tu, hatua 1-3 ni nzuri sana, lakini kwikwi ikiendelea, inawezekana mhusika anasumbuliwa na pumu pia kwa hivyo hatua ya 4 ni lazima.
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Elimu ya afya kwa hisani ya watu wa JF. Safi sana wadau.
   
 13. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii hata mimi naijua, na inafanya kazi kabisaa..
   
 14. majany

  majany JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mke wangu amejifungua siku 16 zilizopita na mtoto anaendelea vizuri tu,hana tatizo kubwa zaidi ya hili linalonipa maswali.Anapata kwikwi mara kwa mara,ambayo hudumu kwa takribani dakika 10-15 then inaisha.

  Swali langu ni kwamba hii hali na kawaida?

  Je, is it necessary for a kid kupata kwikwi yaani hawezi kuishi bila hii kitu? na kama anaweza, what should be done ili niiondoe kabisa?

  Naomba msaada.
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Duh pole sana for ur kid..ila usihofu hii kitu ni kawaida kwa watoto wengi wachanga, ni kawaida sana, mara nyingine huwa anastukastuka na kwikwi huanza! Sidhani kama ni tatizo kubwa, hapa sista angu mtoto akianza kwikwi anachukua uzi wa nguo kuna maji anapaka(hata ukipaka mate ni pouwa tu) halafu anamwekea kwenye paji ya uso katikati kwikwi inakwisha within short time!! Try that ukisubiri ushauri wa wengine!!
   
 16. majany

  majany JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Thanx man..its my first experience,so i have to ask everything...noted
   
 17. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Nilimwona ma wife akifanyaga hivyo,nilidhani ni imani tu,kumbe wengi wanafanya hivyo!
   
 18. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpe maji au mama amnyonyeshe.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwikwi huwapata watoto hata kabla hawajazaliwa wakiwa matumboni mwa mama zao!

  Hutokana na mfumo mzima wa kupumua kwa mtoto.Ni kitu cha kawaida katika ukuaji wa mtoto.

  Cha kufanya ni kumfanaya mtoto apitishe muda katika hali ya raha ( comfort) kwa kumnyonyesha au kumbembeleza.BTW mtoto hubembelezeka kwa urahisi zaidi kwa kunyonya.

  Imani nyingine kama kumwekea uzi kwenye paji la uso haziondoi kwikwi.

  Njia pekee ni kuvuta subira na muda unapita na kwikwi kusha yenyewe.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii myth ya uzi nadhani ipo kwa jamii nyingi saana niliwahi kuwasikia watu kutoka west Africa pia wakizungumza hili.

  Kwikwi kwa watoto wadogo mara nyingi husababishwa na kushiba. Huenda anakuwa ameshiba saana. Kwahiyo hupaswi kuogopa.

  Lakini ukiona inakuwa kero saana kwake, kanyonyeshwe hako ka-uncle mambo yanakuwa sawa.

  Au kama kanatumia bottle, apewe hayo. Unaweza pia kuisearch kwenye net inaitwa hiccup kwa kidhungu.
   
Loading...