JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,327
- 17,915
kutoka Kahama,kwenda kakola,mpaka Geita,barabara ni mbaya sana,migodi hii,ingekuwa kilimanjaro,hizi barabara zingekuwa na taa kabisaHabari za muda huu wadau..?
Napenda kuwaleteen japo kidogo taarifa fupi kuhusu maendeleo katika wilaya yetu ya msalala na kijiji cha kakola.
Licha ya kuwa ni wilaya yenye uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini namaanisha uwepo wa kampuni kubwa ya uchimbaji wa dhahabu inayomiliki mgodi wa bulyanhulu.maendeleo katika maeneo haya hasa kijiji cha kakola ni masikitiko makubwa,kwamba mpaka leo miaka takriban 19 ya uwekezaji bado hali si shwari.
Leo sitazungumzia yote hayo nataka kugusia kidogo swala zima la miundombinu ya barabara zinazoingia nakutoka hapa kakola ambapo ndo hasa mgodi huu mkubwa upo.kijiji hiki kinapakana na mkoa wa geita kwa upande mmoja na wilaya ya kahama kwa upande mwingine.kutoka pande zote hizo mbili kuja hapa hazizidi kilomita 78.
Barabara zote hizi zina hali mbaya kwakweli ikilinganishwa na thamani ya rasilimali za madini zilizopo eneo hili.aibu zaidi ni kuwa tuna wabunge wetu wawili(mbunge wa jimbo la msalala na mbunge wa nyang'wale) ambao kimsingi ndio wawakilishi wetu lakini hatuoni msaada wao katika hili.hasa huyu mbunge wa msalala hatumuoni kabisa akitembelea jimboni kwake mpaka siku za kampeni zikisogea ndio huonekana.
Juzi nilipata kutembelea wilayani msalala nikitokea hapa kakola,hali niliyoikuta ilikua mbaya na aibu sana katika barabara hii.
Na hizi ni picha ambazo zmetoka katika maeneo kadhaa ya barabara hii.
Tusaidiane kuwakumbusha hawa ndugu zetu kuwa hayo madaraka ni dhamana na mungu atawauliza siku ya mwisho.

.... Nakumbuka kilifungashwa na mmoja wa wakubwa wa kitengo cha ulinzi kwa jina la John Bwana, na kisha aliibeba zawadi ile kwenye sanduku madhubuti (safe box)...... Haooooo wakalipeleka kwenye uwanja wa ndege pale Bulyanhulu, tena zawadi ile ikiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.