Kwetu Kakola na Msalala

al abry

Senior Member
Feb 5, 2017
161
102
Habari za muda huu wadau?

Napenda kuwaleteen japo kidogo taarifa fupi kuhusu maendeleo katika wilaya yetu ya msalala na kijiji cha kakola.

Licha ya kuwa ni wilaya yenye uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini namaanisha uwepo wa kampuni kubwa ya uchimbaji wa dhahabu inayomiliki mgodi wa bulyanhulu.maendeleo katika maeneo haya hasa kijiji cha kakola ni masikitiko makubwa,kwamba mpaka leo miaka takriban 19 ya uwekezaji bado hali si shwari.

Leo sitazungumzia yote hayo nataka kugusia kidogo swala zima la miundombinu ya barabara zinazoingia nakutoka hapa kakola ambapo ndo hasa mgodi huu mkubwa upo.

Kijiji hiki kinapakana na mkoa wa geita kwa upande mmoja na wilaya ya kahama kwa upande mwingine. Kutoka pande zote hizo mbili kuja hapa hazizidi kilomita 78.

Barabara zote hizi zina hali mbaya kwakweli ikilinganishwa na thamani ya rasilimali za madini zilizopo eneo hili.aibu zaidi ni kuwa tuna wabunge wetu wawili(mbunge wa jimbo la msalala na mbunge wa nyang'wale) ambao kimsingi ndio wawakilishi wetu lakini hatuoni msaada wao katika hili. Hasa huyu mbunge wa msalala hatumuoni kabisa akitembelea jimboni kwake mpaka siku za kampeni zikisogea ndio huonekana.

Juzi nilipata kutembelea wilayani msalala nikitokea hapa kakola,hali niliyoikuta ilikua mbaya na aibu sana katika barabara hii.

Na hizi ni picha ambazo zmetoka katika maeneo kadhaa ya barabara hii.

Tusaidiane kuwakumbusha hawa ndugu zetu kuwa hayo madaraka ni dhamana na mungu atawauliza siku ya mwisho.
 
437ecd15edf457c6881393d8cd7582f5.jpg
 
Picha, nmesoma shule ya Kakola darasa la kwanza na nilipanda mti mwaka 98,vp kampuni ya Tanzoro bado ipo?
Weka picha
 
Nimefika Chela kijiji ambacho ndo nyumbani kwa mbunge nikatembea tembea mpaka kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo karibia na kijiji cha Nundu tatizo kubwa la Msalala ni miundombinu ni mibovu
 
Nakuna migodi midogomidogo ya wachimbaji wadogo kama vile nyangalata,usulwangili,nyakagwe,kaloe n.k kodi selikali wanachukua tena mtu akihila ndo wanabana sana eti kuna asilimia wanachukua lakini hamna maendeleo yeyote
 
Back
Top Bottom