Kwenye Utawala wa awamu ya 5, Viongozi wa Chadema walikamatwa, walitekwa, walifungwa jela, walipotezwa, walijeruhiwa na wengine waliuawa

actually, hatutakiwi kuja kuruhusu kuwa na utawala wa aina ile tena nchini kwetu. utawala usio na sheria, watu waliishi bila kujua watatekwa au la, na watekaji walikula hela sana za uporaji na kutishia watu aidha kuwapoteza au kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi, Mungu hafurahishwi na maisha ya aina ile, machozi ya waliomwagwa damu yataendelea kulia hadi haki itendeke.
 
Lakini Bado hamtoi shukrani Kwa Samia kukomesha hayo.
Niliona video Moja Sugu anayembelea Tanganyika jeki nilicheka sana 🤪🤪🤪🤪

..Samia na Husseni wanapaswa kuunda TUME za Uchunguzi ili kupata ukweli wa yaliyotokea ktk awamu ya 5 na kabla ya hapo.

..Maridhiano yanapaswa kutambua dhuluma aliyotendeka, nani walihusika, na wahanga kuombwa radhi na kulipwa fidia.
 
Matusi ya Mdude_Nyagali alitamka pale Tabata Baracuda mwezi Juni mwaka 2021 alipotoka gerezani kwa msukumo wa Samia.

Lissu alisema maamuzi ya Rais Samia ni akili au matope baada ya mkataba wa DP WORLD mwaka 2023 Agosti

..hapo ni swali limeulizwa.

..kama maamuzi ya mkataba wa Dp yana manufaa, au hayana manufaa yaani matope, uchafu, ujinga, no.

..kusema viongozi wametukanwa ni kulazimisha mtizamo fulani.
 
? Hiyo character inamaanisha Swali...., Mbowe alikamatwa Awamu ya 5 ? Au ya Awamu ya 6 Tutayazungumzia awamu ya 7?
Ukijua tarehe ambayo aliuawa akwilina utaelewa ninachomaanisha , hapa hatuzungumzii ile kesi ya Ugaidi , hebu fungua ubongo wako
 
Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi huu wa 3, ambao ni Mwezi wa Mungu.

Kwenye utawala wa Awamu ya 5, ulioongozwa na Dkt. John Magufuli, Karibu viongozi wote wa Chadema wa ngazi zote walitekwa, walikamatwa, walijeruhiwa, waliuawa na walirundikwa selo ama walifungwa jela, kwa kesi za uongo ili kuwakomoa.

Wanaouliza kwanini tunayaleta haya leo , jibu lake ni hili , ni kwa sababu hatutaki uchafu huu urudiwe tena kwenye Nchi yetu nzuri, Never and Never again.

Alphonce Mawazo alikuwa kiongozi wa mwanzo kabisa kuuliwa baada ya awamu ya 5 kutwaa madaraka, huyu alipigwa mashoka kuliko hata yale wanayopigwa ng'ombe wa nyama machinjioni.

View attachment 2936409

Alphonce Mawazo ni miongoni mwa watu walioua CCM Kanda ya Ziwa, hii ndio sababu kubwa ya kuuawa kwake , serikali ya Jiwe ikazuia mazishi yake kwa siku kadhaa , yaani wamemuua lakini hawataki azikwe , Mawazo anaingia kwenye historia ya Taifa kuwa mwanasiasa wa kwanza kuzikwa kwa Hati ya Mahakama .

Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba anayekula nyama ya mtu haachi, hakika ndivyo ilivyokuwa, baada ya Mawazo mambo ya kukamata viongozi wa Chadema yakashika kasi, Godbless Lema akakamatwa na kupewa kesi na kisha kunyimwa dhamana kwa tuhuma za kutoa unabii hadharani , hata hivyo unabii huo ulikuja kutimia bila hata kupunja .

View attachment 2936423View attachment 2936426

Kama haitoshi viongozi wa Chadema wakaanza kuwindwa na kukamatwa kama kuku wa Pasaka, Tundu Lissu akapigwa risasi zisizo na idadi kwa lengo la kumuua, ikaelekezwa azikwe haraka na hotuba ya kusomwa kwenye mazishi yake ikaandaliwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu akakamatwa na kufungwa jela kwa kesi ya uongo, Hakimu aliyemfunga jela Michael Mteite akapandishwa cheo.

View attachment 2936433View attachment 2936434

Viongozi wote wa Chadema Tunduma walikamatwa akiwemo Meya wa Mji huo Ally Mwafongo na kupewa kesi ya uzushi ya mauaji, yaani viongozi 57 wote wanadaiwa kuua mtu mmoja tu wa CCM haya ndio mambo ya awamu ya 5.

Mdude akatekwa na kuteswa nusu ya kufa, shukrani ziwaendee Wazungu walioingilia kati hadi akapatikana.

Karibu viongozi wote wa Kamati Kuu ya Chadema akiwemo Freeman Mbowe walikamatwa na kuswekwa gerezani kwa tuhuma za uongo za kusababisha mauaji ya Akwilina, Ambaye alipigwa risasi na Polisi chini ya Lazaro Mambosasa aliyekuwa RPC, viongozi wa Chadema wakahukumiwa kifungo au kulipa faini ya Mamilioni ya hela za kitanzania, unaweza kushangaa walioua ni Polisi, lakini waliohukumiwa ni Chadema!

Hivyo ndivyo Hakimu Thomas Simba alivyoona, Shukrani sana kwa Watanzania walioamua kuchanga fedha zao ili viongozi hao wa Chadema wasiozee jela

Wanachadema waliopotea, kuteswa na kufungwa ni wengi, akiwemo Bernard Saa Nane ambaye hadi leo hajulikani aliko

Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko
Hata uandike nini lakini kiongozi kipenzi atabaki kuwa yeye ni shujaa mmoja tu John pombe magufuli huwezi kubadilisha hilo
 
Hata uandike nini lakini kiongozi kipenzi atabaki kuwa yeye ni shujaa mmoja tu John pombe magufuli huwezi kubadilisha hilo
Lengo la uzi huu si kuondoa umaarufu wa mtu yeyote , hii ni kwa sababu hata shetani ni maarufu kuliko mtume Petro
 
Ukiona unajua sana mabaya ya wenzako basi inawezekana wewe ndo muovu zaidi kuliko hao unaowasema. Ila kwa vile wewe huna umaarufu wowote na haujatoa mchango wowote wenye manufaa kwa jamii utaonekana mwema na watu wasiokufahamu watakusifia sana.
Tangu 2017 ndio unarudi leo !
 
Mkuu usijitoe ufahamu. Najua unaifahamu fika nguvu ya jiwe katika kuamua mambo. Samia na wenzie walikuwa pale wakiwa ceremonial tu, asiweze kukosoa wala kushauri kwachochote alichokiamua bwana yule. Yeye mwenyewe aliweka wazi kuwa hashauriki, na ukimshauri ndo umeharibu kabisa.

Alichokifanya alitafuta kikosi cha majambazi wenzie wachache ndo akaanza kuwatumia kutekeleza ukatili wake huku wengine wakitulia na kushuhudia show inavyokwenda, bila kukosoa kwa hofu ya kufikiwa. Wa kujikomba zaidi walifikia hadi hatua ya kupongeza ule ushetani uliokuwa ukiendelea.

Lakini naamini pamoja na mapungufu kibao kule ccm, ni mashetani wachache walipendezwa na hali ile. Ndo maana pamoja na kuwa safu nzima ilibaki, lakini huo upuuzi ulipungua sana kama si kukoma.

Awamu ya mama ina mapungufu makubwa, hatupendezwi nayo hata kidogo, lakini at least katika hili mabadiliko ya ghafla yalionekana. Kwa sasa at least tunaweza hata kuikosoa serikali na tukabaki salama. Kipindi kile hata kuandika huku tu kwenye ID fake ilikuwa ni unaandika huku ukimwombea Maxence Melo ashinde balaa atakaloletewa kesho kwa comment yako, na zaidi maji yasimzidie unga akaweka taarifa zako hadharani.
Mkuu hakika Maxence Melo ni shujaa, aliwaokoa wengi! Apewe maua yake! 💐🛡️🎖️👑
 
Back
Top Bottom