HOJA Kwenye umeme na mafuta....

HOJA Kwenye umeme na mafuta....

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

YASIYOSEMWA

Member
Joined
Jun 1, 2026
Posts
68
Reaction score
149
Tuambizeni ukweli hizo tozo na Makato hasa kwenye umeme yamezidi...
Unanua umeme wa 5000/=
Unapata unit za 3800/=
Kuna Makato kibao rea,Vat,ewura Kwa sitaili hii kujiajiri Ni ndoto TUWENI TU MAWINGA....
UMEME WA BWAWA LA NYERERE
Ulisafirishwa kwenda wapi mbona Bei YA umeme haishuki kama supply imeongezeka
 
Kodi/tozo mbalimbali ni muhimu kwa maendeleo.

Tatizo kubwa linakuwa kutozitumia kihalali kwa ustawi na usalama wa walipa kodi wote.
 
Yaani huyu mama sijui ana ng'ang'ania nini hapo, kiukweli anatuumiza siku hizi umeme wa elf kumi hautoshi kabisa baada ya wiki umeisha
 
Tuambizeni ukweli hizo tozo na Makato hasa kwenye umeme yamezidi...
Unanua umeme wa 5000/=
Unapata unit za 3800/=
Kuna Makato kibao rea,Vat,ewura Kwa sitaili hii kujiajiri Ni ndoto TUWENI TU MAWINGA....
UMEME WA BWAWA LA NYERERE
Ulisafirishwa kwenda wapi mbona Bei YA umeme haishuki kama supply imeongezeka
Habari,Asante kwa kuwasiliana nasi
Makato yote uliyotaja yapo kwa mjibu wa taaribu na Sheria,Mfano VAT kila mtu anatakiwa kulipia Kodi kwenye manunuzi au huduma unayopata ndiyo maana utakuta kwenye manunuzi ya umeme pia ipo.

Aidha, uwepo wa bwawa la Julius Nyerere limeongeza upatikanaji wa huduma ya umeme nchini ambayo ni muhimu kwenye uwekezaji na ujasiliamali wa aina zote. Hata hivyo kuhusu bei kushuka mamlaka husika (Ewura) wanawajibika kuangalia gharama za umeme na kupendekeza kupunguza au kuongeza kulingana na uhalisia.^CM
 
Washaurini sasa EWURA washushe bei. Maana mkishusha zaidi ya ilivyo sasa mtachochea uwekezaji mkubwa na kukuza uchumi kwa ujumla.
 
Habari, Ndugu Mteja.

Asante sana kwa ushauri wako. Tumeupokea kwa shukrani na tutauwasilisha kwa taasisi husika ili uweze kuzingatiwa katika mikakati yao.

Tunathamini mchango wako na tunakushukuru kwa kutenga muda wa kutushirikisha maoni yako.

Asante sana. ^GK
 
Back
Top Bottom