Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 8,400
- 6,366
Hili zoezi ni kipimo tosha kwamba sera zetu hazina tija, nizile zinazo badilika badilika(uncertainity policies). CCM hawana mfumo wezeshi wa kufanya biashara kisheria ,kwakinyakyusa tunasema :Business enabling environment (BEE) which will follow regurations and rules of the stateMheshimiwa rais,
Unabeba lawama za moja kwa dhulma na manyanyaso na uonevu waliofanyiwa na wanaoendelea kufanyiwa wamachinga katika zoezi hili onevu na kandamizi linaloendelea nchini dhidi yao nitaeleza.
1. Serikali yenu wewe na Hayati Magufuli mliwatengenezea wamachinga utaratibu wa sasa
Mheshimuwa rais, huwezi kujifanya hujui suala la wamachinga toka mwaka 2015 mlipochaguliwa wewe na hayati Magufuli kuingia madarakani, unajua mlichukua hatua gani katika suala hili la wamachinga, na upo ushahidi wa video Mheshimiwa Hayati Magufuli akitoa maagizo kwako na Mheshimuwa Jaffo kutowaondoa wamachinga mpaka muwe mmewapatia maeneo mengine ya biashara. Na katika video hiyo, umesikika ukikubaliana na raisi Magufuli ukisema kuwa "hizo ndo ajira zenyewe hizo"
Sasa mheshimiwa rais naomba kukuuliza maswali yafuatayo:
a) Kipi ulichokubaliana na rais Magufuli wakati huo ukiwa makamu wake ambacho leo unadhani wakati huo mlikosea?
b) Je, hayo mazingira mazuri na mbadala ya wamachinga kufanya shughuli zao wewe kama raisi umejiridhisha kuwa mamlaka za chini zimeyaandaa?
2. Mheshimiwa rais kumbuka mlitunga sheria ya wamachinga kulipa 20000 kwa mwaka ili wafanye biashara zao wasibughudhiwe
Je, mheshimiwa rais, hii sheria mmeifuta lini?, na je mtawarudishia lini pesa zao?
3. Mheshimiwa rais, umevunja ahadi ya kampeni iliyowapeni kura
Mheshimiwa rais, ahadi ya muungwana anapoahidi jambo hutekeleza. Wewe na rais Magufuli mlizunguuka sehemu kubwa ya nchi hii kuomba kura, na mliwaahidi wamachinga kutowabughudi, na mkasema wakilipa elfu ishirini zao watafanya biashara zao bila kubughudhiwa. Leo hii Wamachinga sehemu zao zinavamiwa usiku, watu wsnavunja mali zao, nyingine zinachukuliwa, Hii mheshimiwa rais unaiona ni sawasawa?
Unaona ni sawasawa uonevu mkubwa kabisa na dhulma kubwa wanayofanyiwa hawa wananchi wa Jsmhuri ya Muungano wa Tanzania?. Ukweli wa ahadi yenu wa kampeni uko wapi? Tuseme basi mmeamua bila soni kuvunja ahadi yenu ya kampeni. Je, mmeshindwa kulifanya hili zoezi kwa uso wa utu?
4. Hili zoezi linawatia wananchi umasikini zaidi na linatweza utu wao
Hawa wamachinga ni watu wanaopata ajira zao halali kwa kujituma, ni watu wanaolisha familia zao kwa kazi hizihizi ambazo baadhi ya watu wanaziita "kuchafua miji", kwa nini angalau tusiheshimu hilo?
Mheshimiwa rais wewe unajua shida ya ajira katika nchi hii, leo hii hili jeshi la vijana lisilo na ajira utalipeleka wapi kama hata jitihada zao za kujitafutia riziki badala ya kuzipangia utaratibu mzuri sisi tunaona tufukuzefukuze, tubomoebomoe tu, Tunaipeleka nchi wapi kwa aina ya maamuzi kama haya?
5. Mheshimiwa rais, lawama zote zinakushukia wewe, THE BUCK STOPS WITH YOU
Mheshimiwa rais, hili zogo, unyanyasaji na uendeshaji wa zoezi lisilozingatia utu, lawama zibakuangia wewe mhedhimiwa rais. Ulikuwa na nguvu za kimaamuzi na kibajeti za kuamuru hili zoezi lizingatie haki zotw za binadamu na sheria na taratibu na busara lakini unawaacha wasaidizi wako wafanye uharibifu wa mali wa hawa wananchi wa kipato cha chini. Mheshimiwa Rais Tunataka uzuie zoezi hili mara moja mpaka utaratibu mzuri uwekwe! Leo hii wanaamka watu wanavunja msli za wananchi usiku wa manane, na wewe ndiye rais unaawacha wafanye udhalimu huu maana yake nini?
6. Mheshimiwa rais, kukitokea uvunjifu wa amani, sababu ya zoezi hili wewe na chama chako cha Mapinduzi mtabeba lawama zote
Hawa wanachinga mliwageuza mtaji wa kura, mkawaahidi ahadi ambayo leo hii mnawageuka, sasa kama kukitokea uvunjifu wa amani kwa nini wewe na CCM msibebe lawama.
Mheshimiwa rais huwezi kujitoa, na kujitenga na maamuzi ya rais Magufuli katika hili suala, wewe ulikuwa ni. msaidizi wake mkuu na mgombea mwenza. Kura za Magufuli ni kura zako, Ahadi za Magufuli ni zako. Ile ilikuwa ni serikali yenu, huwezi kukwepa hili. Tueleze sisi wananchi leo kunani unakwenda nyuzi 180 tofauti katika hili suala?
7. Mheshimiwa rais, pamoja na sheria lakini nchi hii inapaswa iongozwe kwa Busara, hekima, mila nzuri na tamaduni nzuri za Mtanzania
Watanzania tulishakataa masuala ya ukandamizaji wa wananchi, Watanzania tulishasema kuwa sheria ni zetu lakini sisi hatumilikiwi na sheria hususan linapokuja suala la masilahi mapana ya wananchi. Ndiyo masna kwa mujibu wa sheria za usafiri kusimamisha watu kwenye vyombo vya usafiri vya umma haikubaliki, lakini mazingira yetu ya hali halisi yanapelekea hivyo. Ni kinyume cha sheria ndiyo lakini tunafumba macho. Sasa leo hii linapokuja suala kuhusu kula na Shibe ya watu, tunakwenda tu kutumia miguvu bila kujali social economic situation ya watu wetu?
Na kama mnasema eti mnadimamia sheria, kwani sheria ngapi mnazivunja kila siku?, Vifungu vingapi mnavivunja kila siku? —Leo hii mnavizuia vyama vya siada kufanya shughuli zao halali za kisiasa kinyume cha sheria na katiba lakini sijawahi kuona mkijutia leo, sasa eti ndo mje mtwambie kuwa mko serious na sheria za mipango miji linapokuja suala la wamachinga, Hizo sheria nyingine je mnataka kutwambia kuwa hamzioni?
Mheshimwa rais onyesha Leadership katika hili suala la wamachinga yanayoendelea nchini si sawa na hayakubaliki!
Tazama hii video usikie jinsi zoezi hili linavyoendeshwa kinyama
View attachment 1991704