Kwenye Maswala ya mapenzi Wazungu ni Noumar!

Kwenye Maswala ya mapenzi Wazungu ni Noumar!

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,437
Reaction score
17,916
Kwenye hili jukwaa huu utakuwa ni uzi wangu wa 3 kama nitakuwa sijakosea.

Niende 1 kwa 1 kwenye mada. Linapokuja swali la mapenzi, Wazungu ni noma, hawa jamaa hawana wivu kabisa.

Kuna Mzungu m1 Dr yupo hapa nchini kwa muda sasa. Huyu kwa uraia anatokea Finland. Ni mtu wa makamo kwa sasa 50+. Kwa maelezo yake ana watoto wa3. M1 kwa sasa yupo Frankfurt huko ujerumani naye ni Dr pia. Wawili wapo Norway ni maDr watarajiwa.

Huyu bwana yupo kwenye Mahusiano na dada m1 hivi, ambaye alimkuta na mtoto m1. Huyu mdada ana umri kama 30 hivi. Kajengewa nyumba, anasomeshewa mtoto wake, na gharama zote za maisha anaendeshewa na huyu Dr.
Huyu Dr Mungu amefuata taratibu zote na huyu dada ni mke wake kabisa. Yaani kalipa mpaka mahari. Huwa wanaenda naye kwao huko Finland pamoja na mtoto aliyemkuta naye. Kila mwaka lazima waende, haswa baada ya majira ya baridi kuisha.
Kimbembe kipo hapa, huyu dada amejaribu kila njia kuzaa na huyu mzungu lakini imeshindikana. Kwani jamaa hayupo tayari. Kwa maelezo kuwa kwa sasa haitaji kuwa na mtoto. Mdada wa watu kapewa ruksa kutafuta mtu atakayeona anamfaa amzalie mtoto. Hivi navyo andika kuna msela kashamaliza kazi, kabandika mimba ina miezi 7 sasa na Dr wa watu hana habari.

Wanaenda wote Clinic, wamepima wote HIV, mzee wa watu anagharamia. Yaani kwake ni jambo la kawaida. Kaanza maandalizi kwa ajili ya mtoto mtarajiwa.

Nimewaza sana nikaona hawa jamaa Wivu wameacha wapi? Ingekuwa ni sisi ngozi nyeusi sijui ingekuwaje. Hii kitu kwa sisi haitakaa itokee.
 
We umejauje kama hiyo mimba siyo ya mzungu?
Huyo mdada ni mshkali wangu. Na alikuja kuomba ushauri. Msela aliyembandika mimba alikuwa mtu wake kabla ya kuzaa huyo mtoto ambaye anaye.

Kwa kifupi namjua nje ndani.
 
Wazungu mtoto si jambo Dogo. Sie tunazaa kama mbwa akiacha kunyonya akajitafutie jalalani. Huoni hapo umesema watoto alio nao wengine nima doctor. Ndicho anacho hofia Huyo babu ni muda wa kula maisha wenzetu wana mipango
 
Hahaha duuh aisee kweli huyo ni mzungu tatizo exposure, kwa wazungu mtoto ni issue kubwa sana
 
Damu zitaruka kila kona wewe,,huo upuuzi wafanye hao hao wazungu hicho kitu kwangu au kwetu wa africa hakuna na haitotokea
 
Back
Top Bottom