Kwenye maisha usiruhusu kila mtu akuzoee ni KOSA kubwa mno pia weka muda maalum wa watu kukupigia simu

Life has no single formulas for us to rely on, yamkini mtoa mada Kuna wanajamii wamekutenda hivyo usihalalishe kuwa hiyo ni acceptable life style to everyone.
 
nyieeee,maisha hayako serious namna hiyo.
nyinyi ndio mnabandika ratiba za misosi kwenye kuta za jikoni.

mtu akikudharau unatoboka!!!si ni upuuzi wake unamsumbua??

mimi kanuni yangu katika maisha huwa sichagui wa kumzoea,sitarajii maajabu kwa binaadam maana nawajua wana visa,wajeuri,wana roho za kwanini,hivyo hata ninapokuzoea nimebeba matokeo yote.

kuna nyumba nilipanga na mama mmoja yeye alikuwa anaishi na watoto wake wa kiume 3,mkubwa ni mlevi mbwa,akija kalewa anaingia ndani kwangu full misele na kuyumba,anakomaa amabebe mtoto nakuwa naye makini tu,siku moja akakojoa ndani kwangu imagine,sijui alitarajia ningesemaje!!!nilikaa kimya tu maana ndio hawa viumbe waliomfanya Mungu akajificha,ni wakorofi sana.
We nae sasa uache ufala.
Ndo haya haha tunasema mazoea yakisenge, we mtu anakojoa ndani kwako unabaki kusema ndo binadamu.

Ebu Wacha ujinga uko

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa unaingilika ingilika kirahisi utajishushia heshima weka limits za watu kukuzoea. Wengine salamu tu inatosha wasikuzoee sana

Kawaida ya mbongo akikuzoea anakushusha thamani ndo maana hata wasanii somo lao kubwa kwenye kazi zao za sanaa ni kujiweka mbali na mazoea yani kutojichanganya changanya hovyo na watu.

Maana utasikia yule jamaa msanii atakuwa yule mbana deile tupo naye hapa tunapiga naye stori ni wa kawaida mno.

Kingine usipende kuchati chati ovyo kwenye groups mtu akiwa interested kuchati na wewe akufate inbox

Kingine weka muda wa watu kukupigia simu ukiona unapigiwa simu mpaka usiku wa manane hiyo ni dharau na wamekuchukulia cheap
Inategemea na shughuli unayofanya
 
Inategemea na maisha unayoishi kama huna connection yoyote we hata ukipachua sim card hutaulozwa kitu ila kama ni ntu wa dili walahi hata chaji hutamani iishe
 
We nae sasa uache ufala.
Ndo haya haha tunasema mazoea yakisenge, we mtu anakojoa ndani kwako unabaki kusema ndo binadamu.

Ebu Wacha ujinga uko

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
nilitakiwa nimuue,embu tia neno mkuu.

ndio nyinyi mnaua au kujeruhi halafu unapelekwa jela kwa kitodhibiti hasira.
 
Pana watu mna akili sana aisee...pana jamaangu mmoja alikua akitoka kazini anazima simu anawasha usiku muda anaojisikia yeye nilimwambia hiyo sio nzuri hakunielewa kuna siku Mzee wake aliumwa ghafra jioni wanampigia simu yeye hapatikani watu wamempeleka hospital bahati mbaya Mzee akafariki huyo jamaa anakuja kuwasha simu saa nne usiku ndio anaona idadi ya missed call na meseji hapo yupo Tanga muda huo atafanyeje ili asafiri ilibidi aondoke asubuhi toka hapo huyo jamaa anaona simu na mtu yeyote anaempigia simu wakati wowote anapokea tuu...wengine wanajifunza kwa matukio na wengine ubinafsi upo kwenye damu wataishi hivyo milele..
Absolutely true, we pokea simu muda wotewote mana uwezi kujua simu ipi ni ya dharura na simu ipi ni ya salamu! Na hakuna mtu anayekupigia usiku halafu akuambie namalizia dakika zangu huyo atakuwa amekuzoea sana! Binafsi nilishapokea simu usiku sana kumbe kuna mzazi yupo hatua za mwisho ilibidi kuwasha gari fasta. Dharura zipo jamani pokeani simu
 
chakula kinakwenda na mood ya kila siku,kuna siku ratiba inasoma makande halafu unahisi kabisa hayapandi labda mchicha na ugali tu,ratiba iko pale juu ifatwe.
sijui kama una familia, kama ni bachela sawa unashauriana tu na halmashauri ya kichwa chako lkn hamna kitu kinachosha kama kupanga menu ya chakula asubuh mchana jioni, inafika point
watu wenyewe hawapendi kuulizwa wanataka kula nn au wanasema we pika chochote, so ratiba inasaidia, kama siku ya makande hamtamani makande si mnabadisha tu
 
Hii ya kupokea simu inategemea mzunguko wako wa watu ukoje, kama ni mwanafunzi, huna kazi/mishe, familia haikutegemei unaweza usione umuhimu wa kupokea maana unajua hamna cha maana, hapo ushapokea simu mara kadhaa nyuma hakukuwa na cha maana
 
Mtu wa kunipigia sim mda wowote Ni mmangati wangu tu anaenipa utamu .
Wengine napokea pale inapobid lakin sio lazima.

Afu sitabiriki mda wowote nabadilika
 
Ukiwa unaingilika ingilika kirahisi utajishushia heshima weka limits za watu kukuzoea. Wengine salamu tu inatosha wasikuzoee sana

Kawaida ya mbongo akikuzoea anakushusha thamani ndo maana hata wasanii somo lao kubwa kwenye kazi zao za sanaa ni kujiweka mbali na mazoea yani kutojichanganya changanya hovyo na watu.

Maana utasikia yule jamaa msanii atakuwa yule mbana deile tupo naye hapa tunapiga naye stori ni wa kawaida mno.

Kingine usipende kuchati chati ovyo kwenye groups mtu akiwa interested kuchati na wewe akufate inbox

Kingine weka muda wa watu kukupigia simu ukiona unapigiwa simu mpaka usiku wa manane hiyo ni dharau na wamekuchukulia cheap
Maisha ni mafupi sana - jitahidi kuyafurahia bila kujiwekea vikwazo na vizuizi vingi. Wote safari yetu ni moja na siku ya mwisho unasafiri mwenyewe kama vile unavyotaka kujiwekea mipaka wakati upo hai. Wewe unatakiwa kupunguza msongo wa mawazo siyo kujiongezea na visheria sheria vingi visivyokuwa na sababu- eti unatafuta heshima.
 
Tafuta pesa,,
Mambo ya ratiba za simu zitajipanga zenyewe.

Hivi ukiwa huna chochote wala lolote hizo ratiba zitakusaidiaje?
Kama sio kujuzidishia umaskini.
 
Hautakiwi kutabirika,mi kuna siku unaweza nipigia simu hata usiku kama niko macho napokea fresh tuu,ila kama nimechoka sitapokea simu ya mtu labda awe wa muhimu sana.
 
Back
Top Bottom