Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,467
- 2,861
Watanzania kuna kila mara sukari huwa inapanda baada ya "kupotea/kuadimika" kwa sababu yoyote ile. Hii sio mara ya kwanza kutokea.
Ila baada ya serikali kuingilia kati napata taabu kidogo hasa kwenye upangaji wa bei. Sukari inzalishwa Mtibwa na Kilombelo. Kwanini bei ya moro iwe 2,700 na Dar ambako hakuna kiwanda bei inakuwa 2,600? Ni kigezo kipi kimetumika ku-justify hili.
Kwanini Kagera sugar ipo kagera, halafu bei iwe 3,000.
TPC kiwanda kipo Moshi. Kwanini bei ya Kilimanjaro isiwe afforable zaidi kiliko Dar ambako hakuna kiwanda??
Katika taarifa ya Waziri Hasunga na Waziri Bashungwa, sijaona kama tumezingatia sukari inazalishwa wapi na kwanini alie karibu na kiwanda anakuwa beneficiary wa kwanza kupata bei ya chini kwa kuwa gharama za logistics ziko chini kuliko Dar.
Au kwa sasa viwanda havizalishi na Dar imekuwa point ya kusambaza?? Kama ndiyo hivi, uzalishaji ukirejea, je bei itashuka au ndiyo wenye viwanda wata-take advantage na kupiga hapo hapo.
Wastani wa bei ya sukari Uganda ni 2,300 kwa TZS; Kenya 2,200 kwa TZS.
Nchi ya Uganda tumewasaidia kumwomwondoa Nduli na baadae kijana tuliemsomesha UDSM akaingia madarakani 1986;
Sisi hapa tunakosea wapi?
Kwa nyakati hizi ambapo baadhi ya watu wanapoteza kazi kutokana na waajiri kuacha kutoa mishahara (tumesikia taarifa kwa baadhi ya mashule binafsi);
Then bei ya sukari inapanda. Inaleta maudhi. Hongereni mawaziri kwa kuchukua hatua, japo we have to do more than that.
BOT, huu ni wakati wa kuwapa dhamana visionaries wenye kuja na solution ya kuzalisha sukari kwa soko la ndani. Please, fungueni milango, Watanzania tupo tayari kufanya biashara ya sukari pia kwa kikidhi soko la ndani na nje ambao kutakuwa na upungufu. Mimi niko tayari, je mtafungua milango tushirikiane kutatua uzalishaji wa sukari, huku tukizalisha ajira, huku tupunguza imports za sukari, huku tukinunua umeme Tanesco wa kuzalisha sukari, huku tukiongeza wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa wanafanya kazi Kiwandani.
Huu sio wakati wa kusubiri wajomba toka Ulaya; huu ni wakati wa kushirikiana kukidhi soko la sukari kwa kuwa ni fursa ipo na soko lipo. Tusiendelee kuona sifa ya ku-import kitu ambacho tuna capacity ya kuzalisha locally.
Takwimu na tafiti toka kwa mtani wetu jirani zinaonesha, nae pia ana upungufu wa sukari japo bei yake ya soko ni nafuu kuliko hapa kwetu.
Ila, hapa chini, kuna taarifa toka kwa mmoja wa watafiti kuwa zao aina ya beet sugar inaweza kutoa mazao mara 2 kwa mwaka tofauti na miwi kuvunwa kwa miezi 9 mpaka miaka 2. Sugarbeet unapata tani zaidi ya 15 kwa hekta (2.5 acres) wakati miwa inatoa tani takribani 7 kwa hekta (2.5 acres)
Bado nina imani, kuwa BOT inaweza kuweka bank guarantee kwenye small and medium scale industry ya dhahabu; kwanini tusitoa guarantee tuzalishe sukari kwa soko la ndani na majirani kama Kenya na Mozambique?
Takwimu zaonesha Kenya anatumia metric Ton 870,000. Uwezo wa Kenya kuzalisha ni metric tons 400,000. Ina maana tuna soko la jirani ambae anategemea mahindi na mchele unaoingia Kenya.
Kwanini tusiwekeze hapa???
Amkeni wakubwa, we join force and produce sugar for local and African Regional Market