Kwenye kupanga bei ya Sukari kuna Suala nadhani haliko sawa. Tutafakari Upya

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,459
2,829
Watanzania kuna kila mara sukari huwa inapanda baada ya "kupotea/kuadimika" kwa sababu yoyote ile. Hii sio mara ya kwanza kutokea.

Ila baada ya serikali kuingilia kati napata taabu kidogo hasa kwenye upangaji wa bei. Sukari inzalishwa Mtibwa na Kilombelo. Kwanini bei ya moro iwe 2,700 na Dar ambako hakuna kiwanda bei inakuwa 2,600? Ni kigezo kipi kimetumika ku-justify hili.

Kwanini Kagera sugar ipo kagera, halafu bei iwe 3,000.

TPC kiwanda kipo Moshi. Kwanini bei ya Kilimanjaro isiwe afforable zaidi kiliko Dar ambako hakuna kiwanda??

Katika taarifa ya Waziri Hasunga na Waziri Bashungwa, sijaona kama tumezingatia sukari inazalishwa wapi na kwanini alie karibu na kiwanda anakuwa beneficiary wa kwanza kupata bei ya chini kwa kuwa gharama za logistics ziko chini kuliko Dar.

Au kwa sasa viwanda havizalishi na Dar imekuwa point ya kusambaza?? Kama ndiyo hivi, uzalishaji ukirejea, je bei itashuka au ndiyo wenye viwanda wata-take advantage na kupiga hapo hapo.

Wastani wa bei ya sukari Uganda ni 2,300 kwa TZS; Kenya 2,200 kwa TZS.

Nchi ya Uganda tumewasaidia kumwomwondoa Nduli na baadae kijana tuliemsomesha UDSM akaingia madarakani 1986;
Sisi hapa tunakosea wapi?

Kwa nyakati hizi ambapo baadhi ya watu wanapoteza kazi kutokana na waajiri kuacha kutoa mishahara (tumesikia taarifa kwa baadhi ya mashule binafsi);
Then bei ya sukari inapanda. Inaleta maudhi. Hongereni mawaziri kwa kuchukua hatua, japo we have to do more than that.

BOT, huu ni wakati wa kuwapa dhamana visionaries wenye kuja na solution ya kuzalisha sukari kwa soko la ndani. Please, fungueni milango, Watanzania tupo tayari kufanya biashara ya sukari pia kwa kikidhi soko la ndani na nje ambao kutakuwa na upungufu. Mimi niko tayari, je mtafungua milango tushirikiane kutatua uzalishaji wa sukari, huku tukizalisha ajira, huku tupunguza imports za sukari, huku tukinunua umeme Tanesco wa kuzalisha sukari, huku tukiongeza wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa wanafanya kazi Kiwandani.

Huu sio wakati wa kusubiri wajomba toka Ulaya; huu ni wakati wa kushirikiana kukidhi soko la sukari kwa kuwa ni fursa ipo na soko lipo. Tusiendelee kuona sifa ya ku-import kitu ambacho tuna capacity ya kuzalisha locally.

Takwimu na tafiti toka kwa mtani wetu jirani zinaonesha, nae pia ana upungufu wa sukari japo bei yake ya soko ni nafuu kuliko hapa kwetu.

Ila, hapa chini, kuna taarifa toka kwa mmoja wa watafiti kuwa zao aina ya beet sugar inaweza kutoa mazao mara 2 kwa mwaka tofauti na miwi kuvunwa kwa miezi 9 mpaka miaka 2. Sugarbeet unapata tani zaidi ya 15 kwa hekta (2.5 acres) wakati miwa inatoa tani takribani 7 kwa hekta (2.5 acres)



Bado nina imani, kuwa BOT inaweza kuweka bank guarantee kwenye small and medium scale industry ya dhahabu; kwanini tusitoa guarantee tuzalishe sukari kwa soko la ndani na majirani kama Kenya na Mozambique?

Takwimu zaonesha Kenya anatumia metric Ton 870,000. Uwezo wa Kenya kuzalisha ni metric tons 400,000. Ina maana tuna soko la jirani ambae anategemea mahindi na mchele unaoingia Kenya.
Kwanini tusiwekeze hapa???



Amkeni wakubwa, we join force and produce sugar for local and African Regional Market
 
kwani hujui pia sukari ya bei rahisi zaidi inatoka nje na lango kuu ni Dar es salaam serikali huwa inatoa vibali kuagiza sukari nje ya nchi pia apart from hivyo viwanda.
 
Hivi viwanda visingeruhusiwa kuagiza sukari vingebaki na kazi ya kuzalisha Zanzibar bei ya sukari haizidi 1800 sasa hiyo bei elekezi imepatikanaje
 
Hivi viwanda visingeruhusiwa kuagiza sukari vingebaki na kazi ya kuzalisha Zanzibar bei ya sukari haizidi 1800 sasa hiyo bei elekezi imepatikanaje
Zenji 1,800 just few hours mpaka Dar au Tanga. Hii inakuwaje.

Ujerumani ambae alikuwa mkoloni wa Tanganyika ukubwa wa nchi yake ni 357,386 km²; wakati nchi yetu 945,087 km²;
Tunawezaje kutumia ardhi na maji yaliyo nchini hapa ku-bridge the gap? Tunahitaji kununua technology (machinery) ili kulima miwa au sugar beet mingi na kuichakata sukari.

Sio sawa, kuwategemea mabilionea wale wale ambao wanauza mpaka barafu tu kitu ambacho kingeweza kufanywa na wengine ili pia nao wapate ukwasi.

Tunahitaji mizania sawa ili mabilionea wengine waingie. Vinginevyo, hawa mabilionea ndo watatengeneza vifungashio vya 500 kama "fulani".
 
The issue is demand and supply. The higher demand the higher price, The lower supply the higher price. The lower price the lower demand. Wanauchumi. Nimemjibu au nimekosea

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kanuni haifanyi kazi kwenye mfumo ambao uko regulated.

Kwa kuvipa viwanda 4 (TPC, Mtibwa, Kagera na Kilimbero) kazi ya kuzalisha na jukumu la kuagiza sukari ili kufidia deficit, kama wakiungana na kuficha au kuchelewesha kuleta, right away inatengeneza watu kugombania. Tumeweza kudhubiti bei kwa mafuta ya petroli na diezel kwa kutumia EWURA ambao pia wanahusika na maji na umeme ambayo watuaji wake (Tanzania) ni wachache, tuna wajibu wa kufanya zaidi kwenye sukari ambayo walaji wake ni wengi kuliko mafuta.

Kwa taarifa kutocha chanzo kimoja, kuna mhindi yuko Mwanza ndiye ananunua sukari yote ya moja ya kiwanda kama wholesaler na kusambaza kwa wauzaji wengine. Sasa mtu kama huyu, akiungana na kiwanda kuchelewesha tu kusambaza hata kwa week moja effect yake ni mbaya sana.

Okay, tuweke dhana, kanuni hiyo iko applicable, njia pekee ni kuzalisha kwa wingi ili bei ishuke. na ndiyo moja ya hoja iliyo kwenye andiko hili.
 
The issue is demand and supply. The higher demand the higher price, The lower supply the higher price. The lower price the lower demand. Wanauchumi. Nimemjibu au nimekosea

Sent using Jamii Forums mobile app
Usisahau hzo theory zina apply under Ceteris Paribus,

Ila Government intervention kwenye masuala haya hua siielewi, yaan mara nyingi naona serikali inawatisha wafanya biashara tu ila sioni technical solutions za kiuchumi..

Ile market equilibrium inayotakiwa kufanywa na serikali sioni ikifanyika zaidi ya vitisho tu vya wanasiasa, na mwisho wa siku sisi walaji ndio tunabeba mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamefanya makosa makubwa,unaweza ukafikiri labda tumekuwa kama marekani ambako kila jimbo huwa na mambo yake,kutoka Dar to Moro ndo muweke tofauti hiyo.Kagera imeumizwa,mpaka sasa wafanyabiashara wengi walikuwa hawazid sh.3,000 mpaka hukoo vijijini ndan leo unajidai umereglate kwa kuipaisha eti 32,00/- Serikali yangu kuwa makini japo kwa mambo madogo kama haya!

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
Muda sio mrefu nimetoka kusoma gazeti la the Citizen, wamepita kwa wauzaji wa mwisho (retailers) ili kujua bei elekezi inatekelezeka au la.

Tanzania retailers want sugar importers investigated

Kwa mujibu wa the citizen, bei wanayonunuliwa kwa wholesalers iko juu. Naibu (W) Mhe. Stella Manyanya akiongea bungeni alipendekeza tutumie asali kama mbadala wakati asali iko juu kuliko sukari.

Waziri Hasunga na Waziri Bashungwa, fahamuni kuwa distributors wa sukari nchi hii ni chache sana; huko ndiko source ya tatizo na sio wauzaji wa mwisho. 2016 Sukari ilipanda, jitihada ikafanyika kuifukunyua, hata sukari iliporejea, bei haikushuka.

Tunawataka udhibiti uanzie kwa distributors na wholesalers; huko bei ikiwa ya chini, it's obvious mauzo ya rejareja yatakuwa chini.

To every cause there is effect, AR Bernard anasema, if you don't like the effect change the cause. Temporarily, tucheze na bei, ila kwa suluhisho la muda mrefu, Wizara ya viwanda fanyeni muwezalo kutoa govt guarantee wenye vision ya kujenga viwanda wajenge kukidhi uhitaji wa ndani na nchi majirani.
 
Leo asb nimesikiza baadhi ya magazeti na vyanzo vingine vikionesha bei ya sukari bado iko juu na vingine vikionesha imepotea.

Nakumbuka mwaka 2016 jambo kama hili la kupanda bei, lilitokea.
Mkurugenzi wa bodi ya sukari wakati huo akatoa elekezi bei kuwa 1,800. Basically maelekezo yale hayakutekelezeka.

SERIKALI YATOA BEI ELEKEZI YA SUKARI

1588752347157.png


Mwaka huu, bei kwa kawaida ilikuwa wastani wa 2600/2700. Mara bei ikanda mpaka 3,000, 3,500, 4,500.

Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara ikaja na bei elekezi

1588752736954.png

Tuna viwanda vya
Kagera Sugar
Mtibwa Sugar
Kilimbero SUGAR
TPC
Manyara Sugar
Kwa kuwa kuna kuna viwanda viwili Morogoro, kwanini bei ya Moro iwe 2,700 na sio chini yake. Haina mantiki cost of delivery iko chini yet mnunuzi anunue kwa bei kubwa.

Kagera Sugar bei mkoani Kagera. Kwanini unafuu usiwepo kwa watu wa Kagera. Au ni assumption sukari yote kwa bei elekezi imeagizwa.

Je, uzalishaji ukirejea, kama viwanda vimefungwa bei itashuka.

Ni akina nani kwenye hili saga hili mwenye ubavu wa kugomea maelekezo ya Serikali?

Kuna maeneo serikali inafanya vizuri kama bei ya mafuta ya petrol/diezel na tunatoa nje. Hapa kwenye sukari kuna nini au kuna nani? kwanini nyakati za mfungo wa ramadhani??
Kinachosikitisha, huwa tunachukulia poa tu?

Sijui kama kuna haja ya kusimama ni hili kuona haki inatendeka ili "wajanja wachache" wanaoagiza na wholesalers wasiwaumize retailers ambao in most cases, ndiyo wanaonekana wabaya. Kwanini udhibiti wa bei usianzie kwa distributors na wholeselers
 
One thing distributors wakiuza waweke kumbukumbu ya efd receipt ya bei waliouzia na kwa retailer yupi?
2. Retailer akiuza juu ashikwe yeye yeye, akidai ni whole sale au distributor, a produce receipt.
Na tatizo likiendelea Suma Jkt wapewe deal la kuwa distributors au retailers
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom