Kwenye hili,wazee walichemsha . . . . . . !!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye hili,wazee walichemsha . . . . . . !!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Oct 11, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Kwa makabila mengine sina uhakika,lakini uchagani nina uhakika.Pia sijui kama jambo hili linafanyika hata leo.Ni kwamba,kwenye familia anapozaliwa kijana wa kiume,na jogoo akawa hapandi mtungi,au akawa hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito,kijana hutakiwa kuoa lakini inapohitajika mtoto,huitwa ndugu wa tumbo moja wa mume kisha kuingia na kukutana kimwili na mke wa kaka/mdogo wake na mtoto atakae patikana huhesabiwa wa mwenye mke!Ki ukweli hapa kwa mtazamo wangu wazee wa zamani walichemsha unless wanifafanulie kilichokuwa kinawafanya wasiwafundishe watoto wao wasijikubali.Ila sidhani kama jambo hili lipo siku hizi.Kama lipo nafikiri ni wakati wa kulipiga vita hata kwenye makabila mengine kwani ni udhalilishaji wa utu!Wewe unaonaje?Walikua sawa?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ngoja waje wenyewe lol
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Haikuhusu . . . . ????
   
 4. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kaka wanataka kukudowea wa ubavu wako! kama halipandi kuwa mpole! ila nimewahi kusikia kuna biashara ya sperm, ina inaingizwa kwa mwanamke bila kuingiliwa.Hayo mabo ya mila za zamani sinahakika kama bado yapo tena labda wenzangu waje kufafanua
   
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Walikuwa sawa kabisaaaa! Wewe unajua zamani LEVEL YA IGNORANCE, NA SEGREGATION ILIVOKUWA JUUU, Alafu mtu aonekane HANISI!!!!! SI ANGENYANYASIKA SANA KATIKA JAMII??? Angetengwaje!!!! Angebaguliwaje? Angedharauliwaje? Kwa kuona kuwa hilo swala litakuwa AIBU YAO WENYEWE WENYE UKOO WAKAONA WAMSITIRI NDUGU YAO!!!! Watu wa nje wanamuona bonge ya RIJALI MUAMINIFU!!! LOL! EVERY BODY IS HAPPY!!! KUFUNGUKA KASORO ZAKO MBELE YA HII JAMII YETU YA WANAFIKI SI JAMBO RAHISI!!!! Hata mimi kama nina ndugu hata na leo, NITAMUUNGA MKONO ACHEZE DILI LA KUSITIRI UTU WAKE!!!! NAUNGA MKONO HOJA!!!
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kumbe ndiyo maana watoto wengi wa kichaga ima hufanana na baba zao, wajomba hata babu zao! Hapa nimekupata. Kama ni hivyo basi kuna wachaga wengi jogoo hapandi mtumbwi. Na hili la mtu kutembea na kaka au mjomba unalisemeaje mwanangu? Maana kupitia hapa jamvini watu wengi walikuwa wakilaani ile tabia ya anko anko na kaka. Sina ushahidi wa hili ila nasikia wamachame na wapare wanaongoza kwenye kamchezo haka ambako twaweza kuita incest.
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unadhani kila akiandikacho mtu kinamhusu?
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Unadhani unaweza ukahifadhi maji kwenye gunia?
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama upo sahihi hapo!
   
 10. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii mada ni safi. Mkuu Eiyer, makabila mengi katika Afrika mali ya mwanafamilia mmoja inakuwa mali ya familia nzima. Mila hii ina vijifaida vyake, lakini matatizo ni mengi. Mtizamo wa kijasiriamali utapendekeza mila hii ifutwe, kwani ukianzisha duka ujue ni la familia, na hii ni mbaya sana. Watakuja watu wakataka kula wasipopanda.

  Lakini unaweza kuototeza mazuri ya mila hii pia, ninavyoona mimi, hasa pale itapohusu kwa mfano hili unalolisemea hapa. Mke wa mwanafamilia mmoja anakuwa mke wa familia. Uzuri unakuja wapi? Chukulia anapokufa mume. Tabia hii iliruhusu mke, watoto na majukumu yote ya yule mume aliyekufa yachukuliwe na mume wa karibu zaidi na marehemu. Of course hili linakuwa na sura mbaya kidogo enzi hizi za ukimwi kwa sababu moja ya majukumu hayo ilikuwa ni pamoja na kulala na mke wa marehemu kumuondolea ile shida ya kukosa mume. Lakini ukiliangalia kwa karibu, kama si ukimwi, mi kwa kweli sioni tatizo hapo! Unalea watoto na kila kitu cha marehemu.

  Katika kabila yangu wazee walikuwa wanaombaa ridhaa ya Mke mkubwa wa mume aliyehai, lakini pia mke mfiwa alikuwa anapewa demokrasia ya kuchagua mwanamume anayemtaka kumrithi katika ukoo wa marehemu mume wake. Mfiwa alifanya uchaguzi kwa kumnywesha pombe togwa mke mkubwa wa mume aliyemchagua. Mke mkubwa akiwa amekubali kushea mume alikuwa anakubali kunywa lile pombe togwa analopewa na mke mfiwa. Wakinywa pamoja wanawake wanaokuwa pale chumbani saa hizo za usiku wanakuwa mashahidi kuwa wale kina mama wamekubali kushea mume.

  Sasa nije kwenye mada yako: Mke wa ndugu yako amekuja kuongeza familia. Huu nadhani ndio mtizamo wa makabila mengi. Na kwa bahati mbaya, Mwafrika alimchukulia mke kama property ya mume. Pale juu tuliona mali za mwanafamilia mmoja ni mali za familia. Kwa hiyo basi, inakuwa sawa kusema mke ni mali ya familia iliyooa. Na ujue hapo kuwa familia zilikuwa zinaoza mabinti zao kwenye familia. Na hakuna kuvunja udugu huo wa familia mbili.

  hili la mwisho nadhani utakuwa ni moja ya misingi ya kutaka mwenye kizazi katika watoto wa familia hiyo amtie mimba binti kwa maana ya kubaki katika familia iliyooa. Mi sioni tatizo hapo kwa kweli... Labda tu hofu ya wivu na hasira za yule asiyekuwa na kizazi. Lakini halo pengine si tatizo kwa sababu atakuwa anafanya kwa hiari kama lile la kuridhiwa katika kabila ya kwangu. Au we Eiyer unasemaje
   
 11. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hao jogoo wanaopanda mitumbwi ni wa wapi ndugu?....huku kwetu wanapanda mitungi
   
 12. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwani wewe sio mzee? lol

  mwanaume kushindwa kuzalisha ni the worst nightmare for most us, hasa kijijini ambapo elimu ni ndogo na unyanyapaa ni mkubwa. ukisikia flani hasimamishi basi huyo mtu alikuwa anadharauliwa kupita maelezo. wazee walikuwa wanafanya hivo kulinda heshima ya ukoo na zamani hapakuwa na IVF, they did the best they could with the little resources they had.
   
 13. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  SASA JE! Mbona WANAUME KIBAO WANABAMBIKWA WATOTO NA WALA HAWASTUKI!!! SIRI YA KATA AIJUAE MTUNGI! UNALEA TU HUKU MKEO ANAJISEMEA MOYONI WE LEA TUUU ILA UNGEJUA NIMEKUCHAKACHUA KWA MBILIMBI!!!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii ni ngumu kumeza kwa nyakati hizi,.........!
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Highlander,asante kwa mchango wako mzuri sana,ila kuna kitu ambacho huwa sikubaliani nacho.Kitu hicho ni kufanya maamuzi kwa sababu bandia.Mfano ulioutoa wa kukubali kumrithi mke kwa nyakati zile lakini ukakataa kwa nyakati hizi kwa sababu ya ukimwi hapo ndipo penye tatizo.Unafanya jambo,japokua ni sahihi lakini kilichokufanya ufanye ni chepesi ni bandia hakina uzito.Yaani kungekua hakuna ukimwi ungekubaliana na mila hii!Highlander,hivi binadamu mwenye akili timamu na anaefikiri kwa usahihi anaweza kumrithi mke au kulala na mke wa ndugu yake?This is insane.Sane people can't do such thing.Naomba mkuu unipe sababu zinazotosha kuhalalisha jambo hili!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mitumbwi na mitungi kwangu sawa tu mwanangu uzee tena. Nilimaanisha mitungi nisameheni baba yenu.
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Lara,suala la kulea mtoto asie wako sidhani kama linahusika hapa!
   
 18. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Linahusika sana, hapo ni kukuonesha kuwa USIPOJUA MTOTO SI WAKO HUTOMBAGUA WALA KULETA VURUMAI KWA MKEO!! Na kwa mahanisi pia ilikuwa hivohivo JAMII AMBAVO HAIKUJUA KUWA YULE MTU NI HANISII ILIMPENDA, ILIMUHESHIMU, WALA HAIKUMBUGUDHI tofauti na ingejua ukweli!
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Wewe unafikiri ni sahihi kumbagua mtu kwa kuwa hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito?
   
 20. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Naomba niwe muwazi katika hili Mkuu Eiyer, kwamba mchango wangu hapa kwa leo ni wa kiimani zaidi kuliko kuwa ya kielimu.

  Mimi nimetokea kuamini kuwa si kila walichofikiri na kutenda babu zetu kilikuwa na makosa. Hili la kumzalisha mke wa kaka yako au mdogo wako ni moja katika hayo ambayo nataka kuyaunga mkono, sababu zikiwa hizo ambazo wachangiaji wengine wamezitoa pia.

  Sasa kwenye hili la kurithi, hata kama ni katika hizi enzi za ukimwi, hebu chukulia kuwa huyu bwana anaerithi kwa bahati nzuri hana virusi, na ikatokea bahati nzuri kuwa mjane hana virusi; hivi kweli wewe Eiyer, pamoja na uwezo wako wote huo wa kufikiri huwezi kuona kwamba ina maana kubwa kwamba mjane asiingizwe kwenye hatari ya kutafuta kuridhishwa na watu baki huko mtaani, ambao pengine watakuwa si salama?

  Haya. Huo ni mtazamo wa kuepusha kumwambukiza huyu mjane ukimwi kwa kumpa iliyo salama katika ukoo. Kumbuka pia kuwa kuna upande wa binadamu ambao si tofauti sana na wanyama, yaani kwamba kuna wanaume wanaweza kufanya wanawake hata watatu kwa siku bila kuchoka--kama jogoo lenye afya vile. Where is the problem!!!

  Unajua Eiyer, binadamu ni mnyama mnafiki sana. Anaeza jifanya ana mmoja, lakini ile sirka yake ya mnyama dume inabaki palepale. Atapiga sehemu mbili mchana na usiku mke hatakaa ajue. Kwanini lisiwe tu wazi kikaeleweka. Hapo sasa ndo unakuja kujua kuwa Waafrika wa zamani hata kama tunawasimanga kuwa walikuwa na akili ndogo, lakini ingalau walikuwa wakweli, wawazi, na kwa kiwango kikubwa sana walikuwa waadilifu in their own way.

  Let us be honest. Hivi kweli wewe Eiyer uwezi kupiga sehemu mbili tatu kutwa na hao wote wasijue kama umeshapiga sehemu? Be honest now..... Kwanini lisiwe tu wazi. Babu zetu walichagua kuwa honest. Kurithi mke wa mdogo wako au kaka yako mi navyoona ilikuwa sehemu tu ya kukiri kuwapo uwezo huo katika binadamu wa kiume lijali. Where is the problem?
   
Loading...