Kwenu wavuta sigara wa bongo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu wavuta sigara wa bongo..

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtoboasiri, Dec 20, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  ...hivi ni kwa nini wengi wenu hamuwafikirii wasiovuta sigara mnapovuta sigara zenu? Utakuta mtu yupo katikati ya kundi la watu (hasa bar na sehemu nyingine zenye mikusanyanyiko ya starehe) anaamua kuwasha sigara yake na kuanza kuvuta! Kwa nini usiende kuvutia kando?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Hapo ndo kando nilipopaona.
  Ila kweli
  tatizo bar zetu hazijatenga sehemu za wavutaji na wasio wavutaji
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0

  Kwani maduka yanayouza condoms yametenga sehemu za kuzitumia au wanaozinunua wanazitumia hadharani?
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni mvuta sigara au wauza sigara? Mchawi ni mpokea kodi za sigara, serikali
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Samahani kuanzia leo nitavutia kando.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Mvuta sigara hajali afya yake, ndiyo maana anaweza kuvuta sigara, utategemea vipi ajali afya/ comfort ya mtu mwingine?
   
 7. P

  Pure nomaa JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 1,050
  Likes Received: 1,076
  Trophy Points: 280
  Kwani kando ndo wapi?naomba kufahamishwa
   
 8. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  mfano: nyuma ya masaburi yako.
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  we need smoking chambers/zones.
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa, Wananiboaga. Mtu anakukuta umechill anaanza kukupulizia mimoshi kutoja kwenye domo lake.
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  halafu ile nyota ulikuwa unavuta siku ile sijui ulikuwa umechanganya na nini........itabidi nikuletee ninazovuta uone laza mpya......
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  drinking without smoking is like a charming girl with one eye.bar ziweke smoking chambers kama billicanas walivyofanya!
   
 13. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Mi navuta kiasi! Ila kwa kweli ukitaka ugomvi instantly nipulizie moshi wa sigara lako lazima nkudunde. Au uvutie ndani. Penye mzunguko mdogo wa hewa. Lazma. Nkutoe
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Iko haja ya kuweka kanuni/sheria za
  - wenye baa/migahawa kutenga sehemu kwa ajili ya wavutaji na wasio wavutaji.
  - kupiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya maeneo ya umma: ndani ya majengo yanayohudhuriwa na watu.

  Wananchi wengi watashukuru kwa hili. Wavutaji na wenye biashara wanaweza kuona kero lakini baadae watazowea.
   
 15. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  tumbaku ihalalishwe
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  niletee halafu ushatest dunhill? Ipo poa hiyo.
   
 17. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,139
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Inaelekea nyie hamfuatilii sheria zinasemaje au kipindi kile ilipotungwa mlikuwa club!!

  Tatizo la Bongo rushwa imekithiri ilishatangazwa hairuhusiwi kuvuta sigara eneo lililosongamana watu haswa kwenye mabasi n.k
  [h=3]SIGARA INAMADHARA KULIKO MOSHI WA GARI[/h]Na aisha Mbaga
  Uvutaji sigara umekuwa kama kitu cha kawaida kwa watu wengi. Watu huvuta sigara
  ili kujisikia vizuri, kuchangamka, kupunguza mawazo na wengine huvuta kama
  sehemu ya starehe.
  Lakini, sigara au tumbaku hufanya nini miilini mwetu? Je unajua kuwa moshi wa
  sigara una madhara kuliko hewa inayotoka kwenye injini za magari?
  Dk. Phiilipo Kinabo wa hospitali ya Muzdalfa Yombo Vituka, anasema kuwa, wavutaji
  wengi wa Sugara wamekuwa na sfya mbaya kutokana na kuathurika kwa mapafu
  hivyo kusumbuliwa na ugonjwa wa TB na kusababisha vifo vingi zaidi.
  Kinabo alisema kuwa, wanaoathirika zaidi ni vijana ambao wameshindwa kuacha japo
  hawakuanza kuvuta kwa sababu ni dawa ama sigara inavurutubishi, lahasha , wengi
  wameathirika kwa tabia za kuiga na kuhisi kuwa wanaovuta sigara ni waungwana
  kuliko walevi.
  pia alisema kuwa, hakuna kitu kibaya chenye kutoa moshi kinachodhuru kama moshi
  wa sigara kutokana na madhara yake kuwa hasara kwa taifa. "Nashidwa kujua kwanini
  Serikali inashindwa kupiga marufuku utengenezwaji wa sigara wakati inafahamu wazi
  kuwa sigara inahatarisha maisha ya wanadamu wengi Diniana kote.
  "Tumbaku ni jani lenye sumu aina ya nicotine ambalo hutafunwa au kuvutwa.
  Tumbaku inachangamsha mwili kama ilivyo kwa sumu aina ya caffeine, ambayo
  hupatikana kwenye kahawa au chai. Sumu hii, humfanya mtumiaji aizoee kwa haraka
  sana. Inamchangamsha mtumiaji na kumfanya awe macho wakati mwingi. Haileweshi
  lakini inapunguza hamu ya kula," alisema Dk. Kinabo
  pia aliongezea kuwa Uvutaji sigara, unapunguza hewa ya oksijeni kutoka mwilini mwa
  mvutaji na kusababisha mwili kutofanya kazi vizuri. Moshi wake unaharibu mishipa na
  kusababisha shinikizo la damu na matatizo mengine ya moyo.
  "Tumbaku ina lami, ambayo husababisha mapafu kutojisafisha vizuri na kuchangia
  kupata maradhi kama vile saratani ya mapafu au koo. Huharibu ngozi na kuathiri
  viumbe ambavyo havijazaliwa,"alisma Kinabo.
  pia alieleza kuwa, pale mvutaji anapojikuta amekuwa mzoefu inamuwia vigumu
  kuacha sigara kutokana na hali halisi, "wengi hujaribu kuacha lakini hushindwa na
  kukosa raha, usingizi na kushindwa kufikiri vizuri" alisema Dk. Kinabo.
  "Sumu iliyopo kwenye sigara ina madhara makubwa kwa afya. Serikali kwa kutambua
  hilo, huwalazimisha watengenezaji wa sigara, kuweka onyo kali la tahadhari kwenye
  paketi zao lakini hiyo haitoshi kwani bado watavuta hivyo ni vyema ikapigwa marufuku
  kama ilivyo kwa bangi na mihadarati mingine," alieleza Kinabo.
  "Kiungo rahisi kuathirika katika uvutaji wa sigara ni mapafu. Baada ya kuvuta moshi
  wa kaboni na tindikali iliyomo kwenye tumbaku huishia kwenye mapafu ambavyo
  husababisha ugumu katika kupumua na kusababisha kutunga usaha kwenye
  mapafu"alisema.
  "Hii huchangia kupata maambukizi mengine kama kichomi, kifua kikuu na saratani.
  Nikotini vilevile ni mbaya kwa tumbo na husababisha kupoteza hamu ya kula na
  maumivu katika tumbo. Watu wanaovuta mara kwa mara hutoa harufu mbaya
  mdomoni na hupata matatizo ya ngozi", aliseleza Dk huyo wa mapafu.
  Akilinganisha moshi wa sigara na mwingineo barabarani, twaweza kujiuliza. "Je, hewa
  chafu na yenye moshi wa sigara ndani ya baa ikilinganishwa na barabarani, ambako
  kuna hewa nyingi zinazotoka kwenye injini za magari, kipi kina madhara zaidi", alihoji?
  Utafiti uliofanywa na wataalamu huko Marekani umedhihirisha kuwa hewa ya ndani ya
  baa ina madhara zaidi. Na uchafuzi kwa hewa ya ndani ya baa au majumba ya
  burudani, hautaweza kuondolewa kama watu hawatazuiwa kuvuta sigara ndani ya
  majengo hayo.
  Matokeo ya utafiti huo, yameonesha kuwa ikilinganishwa na ubora wa hewa iliyoko
  katika barabara ambazo magari huenda kwa kasi au zile za mijini, wakati ambao kuna
  msongamano wa magari, hewa iliyoko katika baa au majumba ya burudani ina
  chembechembe nyingi zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani kwa zaidi ya
  mara hamsini.
  Bw. Jeams Rapaz ni kiongozi aliyeongoza utafiti huo. Kwa mara ya kwanza aligundua
  kuwa, moshi unaotoka kwenye sigara unasababisha maelfu ya watu kufariki dunia kila
  mwaka.
  Katika utafiti huo, Bw. Jeams Rapaz aliona kuwa, kiwango cha chembechembe
  ndogo zenye uchafuzi wa mazingira katika maeneo wanakofanya kazi wafanyakazi
  wa majumba ya starehe na migahawa ni cha juu sana kuliko kiwango cha uchafuzi
  kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
  Kati ya mwezi Novemba mwaka 2002 na Januari mwaka 2003, Bw. Jean Rapaz
  alifanya uchunguzi kuhusu hali ya hewa katika majumba ya starehe na migahawa sita
  ya mkoani Delaware na kupima chembe za aina mbili zilizoko katika moshi wa sigara.
  Matokeo yake yalionesha kuwa kuna microgram mia mbili na thelathini na moja za
  chembechembe katika kila mita za ujazo, kiasi ambacho ni mara kumi na tano kuliko
  kikomo cha chembe kinachoruhusiwa na mamlaka ya mazingira nchini Marekani.
  Na ni mara arobaini na tisa kuliko chembe zilizoko katika barabara ya kasi ya
  Wilmington, Marekani wakati wenye msongamano wa magari.
  Chembe za uchafuzi za aina mbili, zenye madhara kwa afya za watu zilizoko katika
  moshi wa sigara ndani ya majengo manane ya burudani wakati wa usiku zilikuwa na
  microgram mia moja thelathini na nne, kiasi ambacho ni mara tano kuliko kikomo
  kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.
  Ingawa barabara ya kasi ya Wilmington, ambako kuna uchafuzi mwingi ndani ya hewa
  zinazotoka kwenye injini za magari wakati wa msongamano wa magari, lakini chembe
  za aina hizo ndani ya hewa ya huko ni microgram saba tu.
  Kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, hususan katika majengo ya
  burudani na migahawa ni njia nzuri. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baada ya
  kutolewa amri ya kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, chembechembe
  za aina hizo zenye uchafuzi katika hewa ya majengo ya burudani yaliyotajwa hapo juu,
  zimepungua kwa asilimia 90.
  Utekelezaji wa sheria ya matumizi ya tumbaku na bidhaa zake nchini Marekani
  adhabu dhidi ya matumizi inaanzia sh 56,250 mpaka sh milioni 1.2 au jela miezi sita
  kwa wavutaji na wamiliki wa sehemu zinazovunja sheria hiyo.
  Tunapaswa kujiuliza kama sheria ya udhibiti wa bidhaa za tumbaku iliyopitishwa
  bungeni hapa nchini inatiliwa maanani. Kifungu cha kumi na mbili cha sheria hiyo
  kinazuia uvutaji ua utumiaji wa bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma bali
  vitendo hivyo bado vinashuhudiwa.
  by aishasuleyman
   
Loading...