Kwenu vijana mnaokula na kulala kwenu

Kwenu vijana mnaokula na kulala kwenu

Assalam wanajamvi,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,

Napenda kuwaongelea vijana/wanaume wanaoishi kwa wazazi, walezi, au ndugu yeyote.

Katika maisha Mara nyingi sisi wanadamu huwa ni watu wa kutotosheka ama kudhani kuna ofa fulani tunazostahili lakini hatupewi na wazazi, walezi ama ndugu zetu.

Hali hii hujenga dhana ya kulalamikia au kuwabeza wazazi, walezi au ndugu wanaotulea.

Kuna tabia zifuatazo ni mbaya sana kuzionyesha iwapo unaishi kwa ndugu zako au wazazi:-

1. Kulalamikia aina ya chakula.
Hapa utakuta wewe kijana unakaa kwenu au kwa ndugu zako unalalamika kuhusu chakula, Mara kila siku dagaa tumechoka ilihali hujui hata bei ya bamia gengeni. Elewa kuwa kulisha familia ni mzigo kwa mtoa matumizi, usilalamike iwapo wewe hutoi hata pesa ya unga.

2. Kugomea kazi, unakuta wewe umetoka kijijini ukaenda mjini kwa brother ako au mjomba kukaa, mama mjomba ako anakupa hata kazi ya kusafisha banda la kuku hutaki, kulima nyasi hutaki, unataka kushinda kwenye TV unaangalia series za wakorea tena zilizotafsriwa kiswahili.
Elewa kuwa upo kwa watu sio kwako fuata masharti, ukijenga mji wako utafanya huo uzembe wako uone utakavyokufa maskini.

3. Kuwa wa mwisho kurudi nyumbani, utakuta wewe ndio wa mwisho kufika nyumbani usiku, unaanza kuita watu waje kukufungulia geti kana kwamba we ndo baba mwenye familia, matokeo yake mjomba ako au shemeji yako anakuja kukufungulia geti/mlango, kama ni mstaarabu atakwambia jitahidi shemeji uwe unawahi ( hapo jiongeze).

4. Kutaka haki sawa na watoto wazawa wa familia.
Utakuta wewe upo tu nyumbani, ukitumwa kwenda sehemu unataka uende kwa gari, ukinyimwa unaanza kulalamika mbona Ali ( kijana mzawa wa familia) huwa anaendesha. Hapo jua upo for granted maana yake uwepo wapo ni gharama kwa familia husika, usijilinganishe na wenye haki katika familia hiyo.

5. Uvaaji,
Hapa utakuta kijana unakatiza sebuleni ukiwa na boksa tena bila wasiwasi, huu ni upumbavu wa hali ya juu, ukosefu wa staha ni dharau kubwa sana. Vaa vizuri bila kukwaza watu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, maisha ni magumu sana ila kama unakaa kwenu huwezi jua hii shida, anayeijua ni yule anayehakikisha kila siku mnaenda chooni, usijifanye nunda kwenye kaya za watu fuata masharti na uwe mcheshi ujitume hakika utapendwa na kupewa vingi.
Sasa kijana ulivyomwaga nyongo iyo. Kama ndugu yako yupo umu Jamii Forum. Na kaiona Thread yako kesho lazima afungashe MIZIGO yake aondoke
 
imekukatisha tamaa kuja kuwawezesha wengine? pole sana
Nitawawezesha kwa kadiri Mungu atakavyonisaidia lakini si kwa kujinyima na kujisahau kujali mipango ya maisha yangu na wanangu kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Hayupo sawa. Ni jamaa mwenye roho mbaya tu. Ukimkaribisha mtu kwako uwe mwema. Usitegemee malipo. Halafu, mimi ni baba mwenye nyumba. SIpo hivyo.Naitwa baba Nyambuge
Una ubongo gani wewe? Yawezekana unakaa kwa MTU wewe sio bure[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] jitegemee
 
Sasa kijana ulivyomwaga nyongo iyo. Kama ndugu yako yupo umu Jamii Forum. Na kaiona Thread yako kesho lazima afungashe MIZIGO yake aondoke
Sijaandika kwa nia mbaya, uelewa wenu ndio una determine maudhui yangu.
 
Ubinafsi tu na roho mbaya eti ukiwa mgeni usipewe haki sawa na mzawa uwo ni ubinafsi na roho mbaya tuu kaa na mitoto yako na mke wako kwny ilo lijumba lako...
 
Ubinafsi tu na roho mbaya eti ukiwa mgeni usipewe haki sawa na mzawa uwo ni ubinafsi na roho mbaya tuu kaa na mitoto yako na mke wako kwny ilo lijumba lako...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nchi hii haitaendelea iwapo kizazi chenye mawazo tegemezi kama yako kitaendelea kusurvive,
Jaribu kuchukua Ujumbe mzima na sio kipande cha Uzi.
 
Mjini kugumu, usije mjini kama hujajipanga. Mjini hadi mboga ya majani inanunuliwa
 
Mjini kugumu, usije mjini kama hujajipanga. Mjini hadi mboga ya majani inanunuliwa
Acha kabisa, kisamvu pesa, hadi mrenda wakati kijijini mihogo unafuata shambani, halafu upate watu tegemezi wenye miili timamu isiyo na ulemavu wowote wasubiri nguna na kutawanyika kwenda kubeti na kucheza draft. Hapo big no.
 
Una ubongo gani wewe? Yawezekana unakaa kwa MTU wewe sio bure[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] jitegemee
You don't have to panic young man! Molimoli. Mkuu wangu, acha kuruka kichura huku umevaa gagulo. Hahahahahaaa
 
Back
Top Bottom