Kwenu Kinana na Nape - Tuelezeni haya

KG.KASELO

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
252
195
Waziri wa elimu na watendaji wake wengine ni hatalishi kuendelea kubaki ndani ya nyanzifa zao,vijana wengi wataikimbia CCM ususani wale wanajiunga na elimu ya juu,,matatizo ya bodi ya mikopo.

Bodi ya mikopo kwa sasa ni matapeli wakubwa sana,eti mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita miaka mitatu iliyopita ni moja ya sababu ya kumnyima mkopo,

Hebu jiulize swali dogo tu,je,bodi hawafahamu matatazo ya watanzania?hawajui kwamba kuna watu wanamaliza kidato cha sita alafu inawalanzimu kufanya kazi za kilimo kwa muda wa mwaka au miaka ili wapata ela kuomba chuo?

Sasa angalia hiyo hapo chini,'',You were not allocated higher education loan for 2013/14 academic year for this reason:NOT ELIGIBLE FOR LOAN, COMPLETED FORM SIX/DIPLOMA MORE THAN THREE YEARS BACK'' tunalipeleka wapi Taifa hili?

Watoto wa masikini tunawapeleka wapi?

moja ya sera za chama cha mapinduzi[CCM] ni kuhakisha usawa ni kila mtu anapewa elimu,sasa unamnyima mkopo mtoto wa masikini alieomba kusoma kitivo cha elimu alafu unampa mkopo mtoto wa kigogo anayesomea political science ambayo kwa mujibu wa vipaumbele vya serikali ni non priority,hiyo ni sawa?

Polical science hiyo hiyo mtoto wa masikini kaomba amenyimwa!waziri wa elimu yupo,akuna atua zozote,mikakati hakuna.

Huyu ni mzigo ndani chama na serikalini kwani watanzania tupo milioni ngapi?nyingi sana tunashindwa kuondoa mawaziri kama hawa na kuweka watu wenye weledi.

Sio huyu tu,wapo wengi ambao ni mizigo.

Chukua hatua Nape katibu Kinana,chama kikipotea nyinyi tunawalaumu.
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,993
2,000
[h=2]Kinana na Nape: Mnachokifanya ni vurugu na utovu wa nidhamu kwa rais[/h]Watendaji wakuu wa CCM, katibu mkuu Abdrahaman Kinana na katibu wa itikadi na uenezi Nape Mnauye wapo katika ziara ndefu ya mikoa ya kusini. Tofauti na ziara nyingine ambapo tumezoea kusikia mashambulizi dhidi ya CHADEMA, safari hii mambo ni tofauti. Watendaji hao wanazunguka na ajenda ya kuishambulia serikali inayoongozwa na chama chao huku wakiwa na orodha ya mawaziri ambao wao wanawaona ni mizigo au dhaifu kiutendaji na hivyo wanapanda jukwaa moja hadi jingine wakiwapigia kelele wananchi wakisisitiza mawaziri hao lazima wahojiwe kwanini hawa wajibiki. Mawaziri waliopo kwenye ajenda ya ziara yao ni Dr. Shukuru Kawambwa , Christopher Chizza, Adam Malima na Dr. William Mgimwa

Mimi kwa mtizamo wangu naona watendaji hao wanafanya vurugu na kumkosea nidhamu rais ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chao. Hii ni kwasababu mawaziri hao wameteuliwa na rais ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chao ambacho ndicho chama tawala. Kuwasema hadharani kuwa ni mizigo ni sawa na kusema rais naye ni mzigo kwani ndiye aliyewateua. Na kwakuwa rais naye ni mzigo haoni umzigo wa mawaziri wake ndio maana hawaondoi. Sasa hivi wamemuweka njia panda rais kwani akiwaondoa itaonekana amewaondoa kwa shinikizo za Kinana na Nape na sio kwa utashi wake kwa kuzingatia utendaji wa mawaziri husika. Kwa upande mwingine mawaziri hao watakuwa na kinyongo na Kinana na Nape kuwa ndio waliosababisha wakaondolewa katika nafasi zao na si rais au “udhaifu”katika utendaji wao. Rais akiwaacha itaonekana amewapuuza Kinana na Nape hivyo kuwafanya mawaziri husika kuwadharau na kuwachukia Kinana na Nape

Kwa nafasi zao Kinana na Nape wangeweza kuonana na rais na kumweleza hayo wanayoyahubiri majukwaani kuhusu mawaziri mizigo na rais akachukua hatua bila wananchi kujua kuwa ni kwasababu ya shinikizoau mashitaka ya Kinana na Nape na mawaziri nao watajua ni uamuzi wa rais. Mawaziri wanateuliwa na rais kwa mujibu wa katiba na wanawajibika kwake sasa kusema wakajieleze kamati kuu ya chama ni kama kusema kamati kuu ndiyo inayowateua au rais hawezi kutangaza baraza la mawaziri mpaka kamati kuu iridhie. Kinana na Nape hawajawaza vizuri kuwashambulia wateule wa rais hadharani wakati mteuzi ndiye mwenyekiti wa chama chao na ndiye rais wa nchi. Mambo haya yakifanywa na vyama vya upinzani tutaelewa lakini sio chama tawala dhidi ya serikali yake.

Nape amesahau kuwa tabia hii ya kuzunguka majukwaani kuwashambulia viongozi wa serikali na wabunge wa CCM imewahi kumdhalilisha, kumshushia hadhi na kumjengea chuki kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali au wabunge wa CCM. Alidandia hoja ya magamba maarufu kama mapacha watatu na kuanza kuzunguka nayo majukwaani akianza na siku 90 baadaye 120 baadaye halmashauri kuu na baadaye kamati ya maadili ambako mmoja wa aliokuwa anawashambulia ndiye mwenyekiti baada ya hapo vita yake ikafa. Alishindwa na kuvuna aibu lakini hajakoma. Aliokuwa anawashambulia ndio wako kwenye mtandao wa rais na sasa wanautafuta urais. Kesho atakuwa wapi wao wakiwa wameshika mpini?
 
kenethedmund

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
348
195
[h=2]Kinana & nape: Mnapaswa kujiuzulu[/h]Baada ya kufanya mikutano mikubwa mkiwaaminisha watanzania kuwa ccm inawajali na inafungua ukurasa mpya katika kutetea maslahi yao. Huku mkitaja mawaziri mizigo na kusema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi yao, lakini kwa upande wa rais yeye amewaona ndio wanafaa na bado katika kuchagua baraza jipya la mawaziri bado ameonyesha kuridhishwa na utendaji mbovu wa mawaziri mizigo. Kiasi cha kuwaacha waendelee kuwa mizigo tena na kuongeza mawaziri wengine mizigo.

Ushauri wangu ni bora kujiuzuru ili mlinde heshima ndogo mliyobaki nayo, kwa maana mtaenda kuwaambia nini wananchi na mtawezaje kufanya kazi na mizigo. Bora kujiuzuru mumuache Kikwete na mizigo yake, yanini kufanya kazi ambayo mwisho wa siku mnaonekana vichaa.

Ila kweli Kikwete ashauriki !
 
KG.KASELO

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
252
195
Hao hawana mamlaka hayo. Mwambie mwajiri wao - Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Tutengamishe vyama vya siasa na serikali kiutendaji.

Wewe kumbuka serikali inaundwa na chama kilichoshinda uchaguzi,na viongozi wa chama wanauwezo wa kumshauli rais amtoe mtendaji ambaye utendaji wake unahatalisha chama,,,,katibu mkuu wa chama na katibu mwenezi wanauwezo wa kumwambia rais mtendaji huyo ni mzigo ndani ya chama,,,,wakishasema hivyo,,hiyo inakuwa ni moja ya atua mkuu,,,,wizara ya elimu ni wizara nyeti sana,,,inatakiwa apewe mtu ambaye anaifahamu Tanzania vizuri,,na ufahamu wake unatakiwa uanze toka huku chini kabisa[grass root].mtu anayeua elimu,anaua Taifa.waziri huyo kuendelea kwake ndani ya wizara,,,elimu inakaa pabaya sana.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,093
2,000
Waziri wa elimu na watendaji wake wengine ni hatalishi kuendelea kubaki ndani ya nyanzifa zao,vijana wengi wataikimbia CCM ususani wale wanajiunga na elimu ya juu,,matatizo ya bodi ya mikopo.

Bodi ya mikopo kwa sasa ni matapeli wakubwa sana,eti mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita miaka mitatu iliyopita ni moja ya sababu ya kumnyima mkopo,

Hebu jiulize swali dogo tu,je,bodi hawafahamu matatazo ya watanzania?hawajui kwamba kuna watu wanamaliza kidato cha sita alafu inawalanzimu kufanya kazi za kilimo kwa muda wa mwaka au miaka ili wapata ela kuomba chuo?

Sasa angalia hiyo hapo chini,'',You were not allocated higher education loan for 2013/14 academic year for this reason:NOT ELIGIBLE FOR LOAN, COMPLETED FORM SIX/DIPLOMA MORE THAN THREE YEARS BACK'' tunalipeleka wapi Taifa hili?

Watoto wa masikini tunawapeleka wapi?

moja ya sera za chama cha mapinduzi[CCM] ni kuhakisha usawa ni kila mtu anapewa elimu,sasa unamnyima mkopo mtoto wa masikini alieomba kusoma kitivo cha elimu alafu unampa mkopo mtoto wa kigogo anayesomea political science ambayo kwa mujibu wa vipaumbele vya serikali ni non priority,hiyo ni sawa?

Polical science hiyo hiyo mtoto wa masikini kaomba amenyimwa!waziri wa elimu yupo,akuna atua zozote,mikakati hakuna.

Huyu ni mzigo ndani chama na serikalini kwani watanzania tupo milioni ngapi?nyingi sana tunashindwa kuondoa mawaziri kama hawa na kuweka watu wenye weledi.

Sio huyu tu,wapo wengi ambao ni mizigo.

Chukua hatua Nape katibu Kinana,chama kikipotea nyinyi tunawalaumu.

Mungu pishia mbali isije ikawa na wewe unasubiri kujiunga na chuo kikuu!!! Kwasababu unaonekana hata nani ni nani hapa Tanzania hujui! Ati Nape na Kinana?
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,093
2,000
Wewe kumbuka serikali inaundwa na chama kilichoshinda uchaguzi,na viongozi wa chama wanauwezo wa kumshauli rais amtoe mtendaji ambaye utendaji wake unahatalisha chama,,,,katibu mkuu wa chama na katibu mwenezi wanauwezo wa kumwambia rais mtendaji huyo ni mzigo ndani ya chama,,,,wakishasema hivyo,,hiyo inakuwa ni moja ya atua mkuu,,,,wizara ya elimu ni wizara nyeti sana,,,inatakiwa apewe mtu ambaye anaifahamu Tanzania vizuri,,na ufahamu wake unatakiwa uanze toka huku chini kabisa[grass root].mtu anayeua elimu,anaua Taifa.waziri huyo kuendelea kwake ndani ya wizara,,,elimu inakaa pabaya sana.

Kwa kusoma ulivyoandika naweza kusema bila shaka yoyote elimu ilishakufa zamani sana, hivyo haiwezi tena kufa. Labda ifufuke!
 
Bibigula

Senior Member
Jul 15, 2012
141
195
Yani huyu waziri pamoja na mauozo yake yote bado tu yupo lol sijui anakizizi hivi hata haoni aibu duh
 
measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,784
2,000
Yani huyu waziri pamoja na mauozo yake yote bado tu yupo lol sijui anakizizi hivi hata haoni aibu duh

Kinana katika ziara yake alimtaka ajiuzulu anasahau huyu huyu JK ndo anawachagua marafiki zake kuwa mawaziri bila hata kuwa na utendaji wenye tija kwa taifa
 
bandu bandu

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
2,727
2,000
sasa wewe ulishawahi kuona wapi mwizi akimkamata mwizi mwenzake,pole sana kijana hao ndio MAGAMBA bwana hawajui shida za matanzania wa kawaida wao wanachojua ni kupambana na CHADEMA tu.
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,660
2,000
Wewe kumbuka serikali inaundwa na chama kilichoshinda uchaguzi,na viongozi wa chama wanauwezo wa kumshauli rais amtoe mtendaji ambaye utendaji wake unahatalisha chama,,,,katibu mkuu wa chama na katibu mwenezi wanauwezo wa kumwambia rais mtendaji huyo ni mzigo ndani ya chama,,,,wakishasema hivyo,,hiyo inakuwa ni moja ya atua mkuu,,,,wizara ya elimu ni wizara nyeti sana,,,inatakiwa apewe mtu ambaye anaifahamu Tanzania vizuri,,na ufahamu wake unatakiwa uanze toka huku chini kabisa[grass root].mtu anayeua elimu,anaua Taifa.waziri huyo kuendelea kwake ndani ya wizara,,,elimu inakaa pabaya sana.

Umenena vyema -wanashauri. Hata hivyo hao hawatekelezi kilicho kinyume cha sera ya serikali! Na kwa jinsi hiyo labda useme serikali mzima ijiuzulu...
 
Tumake

Member
Mar 27, 2013
56
0
Udhaifu wa Mulugo na Kawambwa ni mtaji kwa vyama vya upinzani. Kama wataendelea kuwepo hadi 2015, watapaisha sana kura za wapinzami. Huhitaji kujua kusoma na kuandika ili uweze kung'amua udhaifu uliokithiri wa uongozi katika elimu
 
mwitendeone

Senior Member
Aug 12, 2013
159
195
wewe unaleta kichekesho walitoa siku 90 za kusafisha mafisadi ndani ya chama ikawa bure enzi ya Mukama (katibu mkuu wa ccm) badala yake yeye ndiye amewekwa kando akaja kinana na timu yake wakato miezi 6 kufukuza wanachama wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa nalo limepita je itakuwa hili la waziri wa elimu hii si saizi yao
 
Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
1,815
0
Mkuu huyu Nape na Kinana ni wakuwapuuza tu. Kama wana nia njema kwanini wasiwaandikie barua hao Mawaziri nakuwaita kwa kuwaoji katika vikao vyao vya ndani?

Sasa kwa kuwa akili zao ni ndogo basi wanafikiri na Watanzania wote akili zao ni ndogo pia kumbe no.

WAPUUZWE.
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Kama Nape ana uchungu na nchi hii amwambie ukweli Kinana kuwa watu tumemchoka kwa unyama na ukatili anaofanya dhidi ya Tembo. Amchane live, haiwezekani kuwaona watu usiowapenda kuwa hawafanyi kazi halafu wale unaowapenda unakuwa na makengeza nao...
View attachment 124614

Na vipi kuhusu yule Chura aliyetudanganya kuwa mgao wa umeme utakuwa historia lakini mgao wa umeme unaendelea na akina Nape hawana mpango wa kumuita kwenye kamati kuu?? Huu ni usanii wa mchana kweupe wanaofanya Nape na Kinana dhidi ya wabaya wao. Nape ni Kichwa Nazi
View attachment 124615
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Wana miaka zaid ya hamsini hao madarakani! !!!!!!
Chama kikongwe na serikali yake; hao wote ni sub ordinates wake ana nguvu ya kuwaelekeza kwa simu tu!!!!

Una uhakika hajawaagiza,kama hajawaagiza anashindwa kuwakataza????!!!!!
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,446
2,000
Kwenye taarifa ya habari nawasikia wakina Nape wanawaambia viongozi waende kwa wananchi wakasikilize kero
Ivi 50 years of freedom you are still mentioning this?
Ina maana hamyajui matatizo ya nchi hii?
sasa ilani mliyoipitisha 2010 ilikuwa feki?

Embu ona hii ujinga mtupu
Mnatufanya sisi kama mambumbu fulani
Mnakera sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom