Kwenu CRDB Bank

meliyasumu

Member
Jul 20, 2021
16
9
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kuendelea kuwepo katika biashara ya fedha katika kipindi chote na kuendelea kuwa miongoni mwa Bank bora Tanzania

Baada ya Kimei kuondoka Bank iliendelea kuwa strong chini ya mkurugenzi mpya aliyekuwa CRDB mwanzoni na kuondoka kwenda NMB na baadae kurudi kuwa mkurugenzi, hii ni ishara ana kitu cha ziada na tunamuombea aendelee

Katikati mwezi wa 6 mwaka jana mliajiri vijana karibia Mia mbili (dse/bdo) katika zone zenu zote tanzania mzima, mkataba ulikuwa wa mwaka na mliwapangia vituo na majukumu yao, mwezi wa sita mwaka 2021 mkawapigia kuanza likizo ya wiki mbili kuanzia 15/6/2021, hadi 30/6/2021, cha ajabu mkaendelea kuwa kimya toka tarehe ya kuripoti hadi 01/09/2021, baadae akaja external recruiter kwa jina la eag ambao pia wanaajili chapchap wa NMB, hv mtu mmoja anaweza kudeal na mahasimu wawili katika kipindi kimoja?

Mkataba wa awali ulikuwa na CRDB wa sasa ni wa eag hakuna end of Contract toka crdb na COPY za mikataba zinaonyesha eag ndio mwajiri but hakuna lolote bank wamefanya, hv mkiulizwa nani amekubaliana na eag mtasema nini? CRDB tafadhari mliangalie hili kwa mapana na weledi, kama kuna mtu ananufaika na eag ajitafakari na kujiangalia, mnapoteza future za watoto wa watu kwa faida zenu, eag hawezi kuwa mwajiri wa hawa bdo/dse maana hakuna makubaliano yoyote, hivi mwezi miwili waliyokaa hawa vijana wakati mliwapa likizo ya wiki mbili inatafsiri gani?

Hamkuwaambia kuwa itakuwa likizo bila malipo na vijana walitii, bad enough mkawapa mshahara tofauti maana mishahara yap huwa wanalipwa khlingana na PERFOMANCE na huwa PERFOMANCE ya mwezi wa nyuma hulipwa mwezi mpya, je mshahara w mwezi wa5 ambao mlilipa mwezi wa sita kweli unaenda na PERFOMANCE zao?

Je, mwezi miwili waliyokaa vila kuwaambia chochote nani anawalipa wakati hamkuwaambia kuwa mkataba umeisha kama utaratibu za kazi zinavyotaka?

Kama mnashindwa kuwaajiri si mngewapeleka eag wakati wa mkataba wa awali maana mnasema bank haiwezi kipindi hiki kuwaajiri watu wengi?

Niwasihi sana tena sana kama hamkujipanga mtaharibu image ya bank maana hamuwezi kuamua nyie wenyewe tu na bank hii ni kubwa na vigezo vya kushindwa kuwaajiri watu Mia mbili hakiwezi kuwa kichaka cha kufichia makosa yenu

Naiomba BoT na Wizara ya Ajira na kazi kufuatilia hili jambo kwa mapana take ili tuwasaidie vijana hawa waliojitoa barabarani kuitetea CRDB (wao wanawaita foot soldiers) kufikisha hizo target ambazo leo wanajisifu nazo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limulike hili kuongeza uwajibikaji ili tuwe nchi ya kufuata kanuni, sheria na taratibu za nchi
Nikiongea kutoka shimoni handakini ni mimi meliyasumu
Msinizike bahati mbaya, niwanukie makusudi.
 
Back
Top Bottom