Kwenu Board ya Uhasibu na Ukaguzi(NBAA)

Kwenu Board ya Uhasibu na Ukaguzi(NBAA)

laptop90

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2017
Posts
1,827
Reaction score
2,298
Kwa miaka mingi bodi hii imekuwa iki recognize wataalamu wa uhasibu wale wenye CPA kama wanachama wao walioko registered na board hiyo.

Kumekuwepo na board nyingi za wanataaluma, zikiwemo Board za madaktari, Board za ma engineers nk, board hizi hazihitaji kuwa mwanachama pale unapokuwa daktari bingwa au master of whatever engineering bali kuwa na digree moja pekee na kukidhi vigezo vingine unakuwa mwanachama wao.

Sasa unapokuwa huko NBAA ni tofauti, ubaguzi unaanzia hapo eti kana huna CPA regardless una madigirii hata matatu yote yame major kwenye uhasibu basi wewe syo member.

Ni wakati wa kubadilika maana syo lazima mwenye CPA ndiye anaejua accounting procedures kuliko wenye wengine walosoma uhasibu.

NAWASILISHA
 
Pointless... Fatilia historia ya NBAA then utaelewa zaidi bila kusahau bodi ya ugavi na ununuzi PSPTB kwa wale wasomi wa procurement wanakuaje recognized... Usiku mwema
Mkuu kama unajua basi msaidie na syo ku crush bila kumeleza, humu jamvini ni mahali pa kuelimishana.Na kwa vyovyote vile yeye amefananisha na Board ya madaktari na ma engineer ambako hakuhitaji uwe na madigirii(specialization). Anahoji iweje NBAA wa recognize CPA kama ndo qualified accountant tu, CPA ibaki kama specialization kama walivyo madaktari bingwa ila wahasibu wote watambulike na kwenye annual conference wawepo wote kama kulivyo na annual conference ya engineers.
NB:VIGEZO NA MASHARTI VIZINGATIWE
 
kuna tofauti kubwa ya kuwa na degree tatu na kuwa mhasibu qualify ndio maana hata hao wenye degree tatu ili wawe wahasibu inabidi wafanye mitihani ya board ila tu wanakuwa exempted na baadhi ya masomo
 
Pia tofauti hyo inaonekana kwa madaktari bingwa na MD wa kawaida lakini hawatengwi ktk registration ya Board zao
 
Kafanye mitihani ya CPA utambuliwe, bodi ipo kisheria, ninavyojua hata hao Engineers wanapomaliza masomo yao kuna miaka mitatu ya kufanya kazi na kusimamiwa na registered Eng na kujaza log books na kuomba usajili.
 
Kwa miaka mingi bodi hii imekuwa iki recognize wataalamu wa uhasibu wale wenye CPA kama wanachama wao walioko registered na board hiyo.
Kumekuwepo na board nyingi za wanataaluma, zikiwemo Board za madaktari, Board za ma engineers nk, board hizi hazihitaji kuwa mwanachama pale unapokuwa daktari bingwa au master of whatever engineering bali kuwa na digree moja pekee na kukidhi vigezo vingine unakuwa mwanachama wao.
Sasa unapokuwa huko NBAA ni tofauti, ubaguzi unaanzia hapo eti kana huna CPA regardless una madigirii hata matatu yote yame major kwenye uhasibu basi wewe syo member.

Ni wakati wa kubadilika maana syo lazima mwenye CPA ndiye anaejua accounting procedures kuliko wenye wengine walosoma uhasibu.
NAWAKILISHA

Mkuu! Nadhani kuna taarifa ambazo haujazielewa vizuri! Mie kwa ufahamu wangu ni kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa NBAA isipokuwa hao wanachama wanatambulika kwa makundi tofauti. Kuna wanachama tu, wanachama ambao ni watahiniwa (candidates), Wanachama ambao wamepata CPA chini ya miaka mitatu (graduate accountant GA), na wale magwiji wenyewe sasa (ACPA, ACPA-PP, FCPA). Hivyo NBAA inao wanachama wengi sana wasiokuwa na CPA ila tu huo uanachama ili uupate lazima ujaze fomu na kulipa kiingilio na ada ya kila mwezi. Sasa labda kama unataka members wote wajulikane kama ACPA!

Wasalaam!
 
izo board zote ni wizi wa pesa zetu sisi member wanatuibia tuu wapigaji azina umuhimu wowote zifutwe...Mkuu JPM zifute izi board.
 
Pia tofauti hyo inaonekana kwa madaktari bingwa na MD wa kawaida lakini hawatengwi ktk registration ya Board zao
uwezo wa qualified accountant ni tofauti na mtu mwenye degree tatu, tatizo watu wanapenda mkatomkato kama una degree tatu unaona shida gani kusoma cpa wakati kuna kozi nyingi umesamehewa
 
Kafanye mitihani ya CPA utambuliwe, bodi ipo kisheria, ninavyojua hata hao Engineers wanapomaliza masomo yao kuna miaka mitatu ya kufanya kazi na kusimamiwa na registered Eng na kujaza log books na kuomba usajili.

Kwani wahasibu hawafanyi kazi hyo miaka mitatu ndg?
 
uwezo wa qualified accountant ni tofauti na mtu mwenye degree tatu, tatizo watu wanapenda mkatomkato kama una degree tatu unaona shida gani kusoma cpa wakati kuna kozi nyingi umesamehewa
CPA inabase kwenye academic unapimwa uwezo kwa mitihani ya darasani ya bodi.Bodi zingine ni practical unapimwa uwezo kwa kufanya practically kwa miaka kadhaa chini ya usimamizi wa aliyesajiliwa kabla ya kusajiliwa kama proffessional.Nafikiri mleta mada hasa ndicho anacholenga kuwa mitihani ya darasani kutambua mtu kama professional accountant uondoke
 
Mimi wananiboa tu na kile kiwebsite chao. Utafikiri wameandika kwa mkono. Members wote wa board wangekuwa na account zao ambazo wana-login kujua hata mienendo yao. Lakini duh.
Pesa wanazotulipisha kwenye mambo mbalimbali ni nyingi ukichanganya na ruzuku sidhani kama wanashindwa ku-hire web desiner mzuri na kuhost taarifa za members

Poor us[emoji22]
 
Kila taaluma ina utaratibu wake na hii ni dunia nzima. Nenda nchi yoyote duniani na degree yako kama wataku certify direct.

Tena nchi zingine kama USA wana masharti magumu sana ikiwemo GPA kali ili uruhusiwe kufanya mitihani.

Nenda kapige CPA exams ndio utajua kwanini ni muhimu. Kwa hizi degree za chupi na kubebana mnataka wote muwe qualified accountants!
 
Mkuu! Nadhani kuna taarifa ambazo haujazielewa vizuri! Mie kwa ufahamu wangu ni kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa NBAA isipokuwa hao wanachama wanatambulika kwa makundi tofauti. Kuna wanachama tu, wanachama ambao ni watahiniwa (candidates), Wanachama ambao wamepata CPA chini ya miaka mitatu (graduate accountant GA), na wale magwiji wenyewe sasa (ACPA, ACPA-PP, FCPA). Hivyo NBAA inao wanachama wengi sana wasiokuwa na CPA ila tu huo uanachama ili uupate lazima ujaze fomu na kulipa kiingilio na ada ya kila mwezi. Sasa labda kama unataka members wote wajulikane kama ACPA!

Wasalaam!
Kweli. Kila qualifications ya uhasibu ina category yake ya registration hadi certificates ya uhasibu. Degree ya uhasibu pia inatambuliwa na ina category yake ya kuwa member ila sio kuwa certified.
 
Mitihani ya CPA migumu watu wanatafuta pa kutokea!!!! Ndio msingi hasa wa mada.
Kuna madogo vipanga wanaitusua tu...tabu wale tia maji tia maji na unakuta hata degree wamemaliza kiujanjaujanja sometimes hata GPA zao ni nzuri lakini janja janja mingi.
 
Back
Top Bottom