Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,346
- 3,033
27-10-1980 katika kijiji changu, majira ya saa 4 usiku mama ukiwa umelala baada ya uchovu wa shughuli za pale nyumbani, ukiwa na ujauzito wa miezi tisa , ndipo baba alipo kuja na mwana mke mwingine ndani ya nyumba na kuamua kukupiga na kukusukumia nje ya nyumba huku mvua kubwa ilio ambatana na upepo ilikua ikinyesha, mama yangu mpenzi ilipo fika saa 8 usiku huku ukipigwa na baridi kali kule polini, ulishikwa na uchungu na ilipo fika saa 9 usiku mama yangu ulijifungua ukiwa peke yako pale polini.
Ilipo fika asubuhi msamarimia mwema mmoja alie kua katika pita pita zake za kutafuta kuni pale polini ndipo alipo kuona ukiteseka na kulia kwa uchungu kwa maumivu uliyo kua nayo ndipo alipo sogea kujua yaliyo kusibu, msamaria aliamua kukuchukua hadi kwake pamoja na kichanga chako, baada ya kukufikisha kwake alikuhudumia nawe ukamsimilimua yote yaliyo kusibu. Msamalia alienda jikoni kuandaa uji, kabla ya uji kuiva mama yangu mpenzi ukaiga dunia na kuniacha mwanao mpendwa wa kwanza na msamaria.
Mama yangu mpenzi msamalia alinitunza na kuniudumia kama mwanae hadi leo hii, jana usiku msamaria alinisimulia yalio kusibu mama yangu mpenzi na ndipo nilipo amua kukuandikia waraka wangu huu kua mama nimefahamu yaliyo kusibu katika maisha yako, sikua nafahamu mama yangu mpenzi na ndio maana uliona kimya. Leo hii naitwa Baba wa watoto wawili ambao mama yao kipindi anajifungua alifariki.
Mama yangu mpenzi upumzike kwa amani, Daima utakua ndani ya nafsi yangu na mapenzi yako nita yaishi...

![get-well-soon4[1].jpg get-well-soon4[1].jpg](https://www.jamiiforums.com/data/attachments/3160/3160293-dd0a908eeca51c231c1652c61856edc9.jpg?hash=3QqQjuylHC)
![1590_get_well_soon_card[1].png 1590_get_well_soon_card[1].png](https://www.jamiiforums.com/data/attachments/3160/3160294-98c0a599ce7969025a671d7b496faa37.jpg?hash=mMClmc55aQ)