Mwaka 2012nikiwa musoma mjini, j, mosi saa nne tukipanda mlima wa Kilimanjaro na washikaji zangu watatu. Mara line ya voda ikapokea 650,000/=.nikawaonyesha washikaji tukaenda kutoa fasta. Tukiwa kwa wakala moyo ukauma usiibe,ujui ilitumwa kwa kazi gani? Wewe mkristo kuwa shaidi wa wa injili, nikaailisha kutoa. Lafiki zangu wakaja juu tukatofautiana nilipoailisha kuzitoa. Ilipofika j, tatu nikapokea CM, samahani nilikosea kutuma pesa ijumamosi nikajua niliemtumia kazipata. Ila kanipigia Leo hajapata ndio nacheki naona nilikosea. Tafadhali niludishie nusu ya pesa kwani nilikuwa namtumia mwanafunzi yuko bukoba. Mimi ni Mchungaji wa kanisa la kiroho niko Arusha, wewe uko wapi? Nikamjibu niko musoma mjini. Ata pesa izo nimechangiwa na waumini kijana yuko high school. Nikamjibu niko kwenye bus naenda Mwanza, CM ina arati chaji inaisha, nikifika Mwanza saa Saba nitakutumia zote ila Sina ela kwenye CM ivyo watakata ya kutumi....... CM ikazima!!!. Baada ya masaa mawili nilikuwa Mwanza nikachaji CM kisha nikamtumia PESA 645,000/=. Mara akapiga cm akashukulu kisha akaniambia bwana Mungu wa Israeli akaulinde uchumi wako. Baada, ya wiki tatu nilimtumia Mke wangu PESA ya kodi ya nyumba huko Dodoma. Niliituma siku ya ijumaa shilingi 900,0000/= nikiwa musoma mjini. Jioni yake tuliwasiliana na wife tukapiga story mbili tatu, akuulizia tena kodi nami nikaamiñi alipata PESA. Jumapili pia tuliwasiliana akuniuliza PESA ya kodi nami sigusii nikijua alishalipia. Ijumatatu saa nne akaniulizia kodi!! Nikamwambia mbona nilituma!!, sijapata mie, nilituma ijumaa!. Nikakuta nilikosea kwani nilitumia CM ya Android isio na Batan. Nikaamua kumpigia niliemtumia, akapokea nikamueleza nilikosea kutuma PESA ijumaa. Akasema nilipokea PESA ijumaa kwa namba hii unayotumia, nikawa nangojea unipigie ila ukupiga CM wikendi nzima!. Ivyo niko ofisini muda huu na niko bize, nitakutumia saa Saba muda wa lunch. Kwani uko wapi wewe? Akaniuliza, nikajibu niko musoma mkoa wa Mara. Daah, niko Lindi nachingwea Mimi!! Subili lunch time. OK. Saa Saba na robo PESA ikawa imeludishwa imekatwa ya Kitumb tu!!! Dunia waaminifu wapo.