Kweli Tanzania nitapata mkweli huko?

Kweli Tanzania nitapata mkweli huko?

bidodo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
217
Reaction score
90
Jamani naombeni ushauri.

Mimi mkazi wa Admonton Canada, sasa nipo chuo ila nimepanga nikimaliza chuo baada ya 2 years nije kwetu kuolewa na Mzanzibari because hao wa huku nilowaona sijawapenda kitabia. Tabia zao ni zile zile za kuvaa vidani na mie familia yangu nataka iwe ya maadili ya home.

Nimejitahidi kumrekebisha kijana mmoja alinipenda ila hapendi mtu amwingilie katika maisha yake, anasema huku free, kila mtu anaishi apendavyo.

Kwa vile ni mdogo sana nimeachana na hayo mapenzi, nipo 22 sasa napiga kitabu. Ila swali ni, ni kweli nikija huko nitapata mchumba? Maana nasikia kila mtu na wake. Naogopa nisije danganywa mie maana maisha yangu ni ya huku hata kama nikiolewa nitaishi huku.

Itabidi nimchukue tu maana wazazi na familia ipo huku. Samahanini kwa upungufu wa kuandika Kiswahili.
 
Utapata tu! Wewe rudi huku upigwe ndoa za mitala.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
unatafuta mme kama unatafuta ajira?
Upendo hauna nafasi?
Una hakika gani utampenda huyu 'ready made' wa TZ?
 
Na wewe Kongosho wacha kumkatisha tamaaa mwenzako, bidodo tupo wengi tu wala usiogope, tena na deal ya kupelekwa Canada juu? We ukirudi anza na mimi wala sivai vidani...
 
Last edited by a moderator:
kwenye haya mambo moyo ndo hua unaamua wenyewe upende wapi!
 
ndoa za mitala ndo nini Sumu
 
Last edited by a moderator:
Utapata Tu wala Usihofu binti...

We Jitunze tu...Ila sasa Ukubali na Malengo ya atakayekuoa..Kama ye hataki Kuishi Huko Canada Utafanyaje sasa?
 
ndoa za mitala ndo nini Sumu

Ndoa za mitala ni zile ambazo mwanaume anaoa mke zaidi ya mmoja.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
owww ok ya itabidi nilikubali hilo la ndoa za mitala kama muislam ila inataka moyo huku Canada hazijulikani mwisho mmoja kwaiyo naona nitakuja mpa shida mwenzangu. Naomba salama too sasa ndo mambo ya kwenda nchi za watu ukubali matokeo
 
Bidodo yakheee wewe uko 22 binti wa kizenji bado wajiona mdogooo?????? Mbona ushakuwa bibi weye sema hujashtuka mapemaaa! Ukirudi huku utakuwa 25 na ulivo msomi utapata vijana Wakitwana tuuu!

Fanya hima shosti! Wale wanaume zetu Udongo wa Dubai hawapendi watu walipita sanaa skuli ati! Na hivo umri ushasogea utazaa lini weyeee!? Fanya kupata hukohuko! Ohoooo! Huku wote washaenda wete kuoa! Na watoto wao utakuta skuli washaanza! Fanya unielewe uzuri haya nayokumegea!

Labda sanaa utapata hawa waliopita skuli wenzio vijana wakitwana ama uende Dubai ama Muscut! Mie nikutakie skuli njemaaa! Ndo ujue huku visiwani twakutegemea weyeee uje utukomboe wanawake wenzio na kupika kachori, bajia, urojo, na kutengeneza chatney siku nzima!:becky:
 
Mpaka ukija huku na Muungano tutakuwa tumeshavunja kwahiyo jiandae kuolewa na Gaidi la Kizanzibar tena uwe mke wa 4.
 
awahi mapema, afu a-recruit hazibend maeneo ya Sinza au Kinondoni, hakosi mme.

Mpaka ukija huku na Muungano tutakuwa tumeshavunja kwahiyo jiandae kuolewa na Gaidi la Kizanzibar tena uwe mke wa 4.
 
@ Tuvako apo mtihani mana wengi wanoletwa wanawake huku mume anakuja owa wengine huingia baruti wakiona washaletwa na wakiona unyunyu wa pesa hurudiana na wapenzi wao hasa sijui kama wanaume ndo watakua ivo ivo?apo mtihani
 
asante kwa ushauri @lara uko hukosi mchumba najua ao wa dubai na maskati nawaogopa na weete kabisa kuna vichuna ukooooo wasije kunidanganya bora niwe na subra pengine huku nitapata
 
awahi mapema, afu a-recruit hazibend maeneo ya Sinza au Kinondoni, hakosi mme.
Unampoteza, Sinza na Kinondoni Watoto wa kiume wanajipodowa na kusafishwa kucha kama mashori ili kutega mashugar Mummy ndio unamshauri aingie mkenge huo? bora haje kwetu huku Mkuranga angalau anaweza kupata Mwanaume mwenye nguvu kama Sauli.
 
ndoa za mitala ndo nini Sumu

Jamani bidodo, kwahiyo plan yako ni nini eti?
Umalize chuo..
uje Tanzania (au Zanzibar)..
utafute mchumba (mume?) ..sijui umejipa muda gani wa kumpata huyu mume
then muondoke wote mkaishi Canada??


Au mimi sijakuelewa?
 
Last edited by a moderator:
Kongosho mapenzi kokote haijalishi wapi. Mii siangalii pochi wala iyo ready made wa tanz nataka mapenzi ya kweli na mtu mwenye tabia nnazo dream. huwezi kukurupuka bora jitahidi kufatilia ni maisha yanayozungumzwa
 
Last edited by a moderator:
Mentor ndo ivo ivo nimalize chuo nije zanzibar au tanzania uko kote kumejaaa wazenj ata bongo muhimu muislam too awe na tabia na hulka za kiislam ila nikimpenda ndo nianze process za kumchukua lakini kunatisha navoskia kila mtu ana wake. KUMEKUCHA UKOOO??? Kweli. Daaa mazali ninasoma sitoshindwa kumleta
 
Last edited by a moderator:
Wee bidodo, kwani yule mbwiga aliyekwambia usipoenda kwake humpendi mmefikishana wapi???
 
Back
Top Bottom