Kweli TAKURURU wana lao jambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli TAKURURU wana lao jambo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tankthinker, May 5, 2011.

 1. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWELI TAKUKURU WANA LAO JAMBO!!!.

  Ndugu wana JF,

  Nilivutiwa sana na mada ilitumwa siku chache zilizopita iliyohusu "TAKUKURU WASHINDWA KUWACHUNGUZA MAFISADI, SASA WAGEUKIA MAASKOFU".

  Hata nikaamua kuchukua hatua ya kujitafutia mwenyewe sheria inayowapa kazi wana TAKUKURU - THE PREVENTION AND COMBATING OF CORRUPTION ACT, 2007 iliyopitishwa na Bunge letu tarehe 16 April 2007.

  Nilipokuwa nikiendelea kusoma kuhusu majukumu ya sheria na kulinganisha hiyo assigmemnt wanayoifuatilia kwa Maaskofu, inaonyesha kuwa wanafanya kazi wasiyopewa na Bunge letu, au hawaielewi sheria waliyopewa au wanatumikia kusudi na mtu fulani kwa maslahi binafsi.

  Kwa mfano sheria inasema hivi, na hapa nitanukuu katika lugha ya Kiingereza kuhusu makusudi ya sheria hiyo (Objective of the Act) Ukurasa wa 218.

  4.-(1) The objective of this act is to provide for promotion and enhancement of good governance and eradication of corruption.

  (2) In the promotion of the objectives reffered to under subsection (1), this Act provides an institutional and legal framework necessary for prevention and combating corruption by-

  (a) examining and advising on practices and procedures of public,and parastatal
  and private organisation, in order to facilitate the detection of corruption or
  prevent corruption.

  (b) disseminating information to the public on evils and effects of corruption and
  corrupt practices as well as negative traditions and usage.

  (c) cooperating and collaborating with local and international institutions,
  agencies or organisations in the fight against corruption.

  (d) promote and foster public support and combating corruption; and

  (e) investigate and prosecute offences relating to corruption.

  Kwa mtazamo wa haraka unagundua kuwa jukumu lao kubwa ni kinga dhidi ya rushwa kwa mujibu wa fungu hili hapo juu. Ninaanza kuwa na kigugumizi na mashaka na hizi mbio za kuwageukia viongozi wa dini.

  Leo Maaskofu, kesho Mashehe ili mradi tu wafanikishe azma yao ya kuwanyamazisha ili jamii isipate elimu wanayostahili. Nami nasema, viongozi wa dini msitishwe na hawa vibaraka walioacha majukumu yao kufuata maslahi binafsi.

  Hivi kweli kipindi hiki ni cha kusikia TAKUKURU wanawachunguza viongozi wa dini? Hivi hawasikii vilio vya Watanzania walio wengi kwa sasa kuhusiana na ufisadi uliokithiri katika nchi?

  These people are not keen and serious on what has been entrusted to them.


  KWELI TAKUKURU WANA LAO JAMBO.
   
 2. m

  mkulimamwema Senior Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawakupaswa kusomeshwa na nchi utadhani hawajasoma kwanini wasitumie elimu yao na kuwa na msimamo yaani tunawalipa mishahara bado tu wanaendekeza mambo ya kijinga
   
 3. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Lakini hebu tusome vizuri hiyo section 4(2)(a) uliyoinukuu, ambapo kwa maoni yangu taasisi za dini zinaangukia kwenye kundi la private organisations. Nafikiri TAKUKURU wanayo mamlaka kwa mujibu wa sheria hii kumchunguza kila mtu anayefanya makosa ndani ya Tanzania Bara pekee ( tazama section 2(1) ya sheria hiyo).

  Tabu ni kwamba hatujazoea kuona dini zikiguswa, sasa zimeguswa. Zitakapoguswa tena na tena tutazoea tu. Hivyo sioni kama TAKUKURU wamevunja sheria yao au wamevuka mipaka yao.
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Rudia kusoma tena sheria waonekana hujaielewa vizuri, wamefanya kazi kwa mujibu wa taratibu zao
   
 5. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe GenuisBrain naona ndo hukunielewa au hukuuelewa msisitizo nilio uweka kwenye nukuu yangu hiyo.

  Naona umekurupuka kujibu tu bila hata kujua kinacho sisitizwa, ni heri ungesoma tu na kukaa kimya ungezaniwa una hekima lakini sasa.....

  Ni kwa mujibu wa taratibu gani hizo ambzo hazitumiki kwenye maswala yanayo ibomoa nchi hii kwa ufisadi uliopitiliza, ambao watuhumiwa wake wanajulikana wazi wazi na hawajashughulikwa na baadala yake wanapoteza muda kwa kufuata watu ambao mwisho wake wala hautasaidia chochote.

  Maana kutokana na maelezo ya thread ile iliyo kuwa imeletwa jamvini, Huyo Askofu inasemekana ni muadilifu tena ni vile amekuwa akikemea mafisadi na wabadhirifu wa mali za uma katika mikutano yake, na hata alipofatwa na TAKUKURU ametoa ushirikiano na wala hawajapata chochote kile.

  Sasa nguvu yote hiyo imepotea na maasaa ya kazi yametumika vibaya wakati kuna watu ambao wakifuatwa taifa litanufaika kutokana na wizi walio ufanya kwa taifa hili.

  Mimi nadhani hii TAKUKURU ifutwe haina maana yeyote ile. Na watu kama ninyi mnaoshabikia bila kuwa naufahamu wa yanayo tendeka sijui ni lini mtafunguka.
   
 6. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Komeo, nakubaliana kuwa TAKUKURU wanayo mamlaka ya kumchunguza kila mtu Tza bara. Hoja yangu ni kwa nini TAKUKURU haionyeshi nia ya dhati ya kutaka kushughulikia RUSHWA na UFISADI ulio pitiliza ambao wahusika wanjulikana?

  Na badala yake wanapoteza muda na pesa za walipa kodi kwa kufanya shughuli zisizo na tija kwa taifa?

  Maana yule Askofu aliye jadiliwa hapa jamvini inasemekana kuwa ni kwa sababu ya yeye kuwakemea mafisadi na wabadhilifu wa maili za umma katika mikutano yake ndicho kimepelekea yeye kufuatwa fatwa na TAKUKURU.

  Na hata walipo mhoji yeye aliwapa ushirikiano wa kila walichotaka maana anajiamini kuwa ni muadilifu na mpaka sasa hawajaambulia chochote kile.

  Wakati wange wafuata watuhumiwa wa kweli taifa lingenufaika kutokana na mali za hawa wajanja ambazo wameliibia taifa kwa muda mrefu.

  Kudhania kuwa hawa jamaa wanafanya kazi yao ni udhihilisho kuwa kweli sisi tuko kwenye usingizi mzito sana. Maana ni kazi ipi inayo fanywa na hii TAKUKURU?

  Ni lini umesikia kuwa kuna mtuhumiwa ambaye kweli kakamatwa na kufilisiwa baada ya uchunguzi wa TAKUKURU kukamilika? nani? lini? kiasi gani?.

  Aaaah! hiki chombo nakijifie hakina maana yeyote ila kwa walio wajinga tu.
   
 7. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nionavyo, Takukuru ni chombo kilichowekwa ki-propaganda zaidi ili serikali ionekane kwa mataifa ya nje na hasa yanayotoa misaada kuwa inapambana na rushwa ila ukweli ni kuwa ni usanii mtupu. Ningeshauri hii taasisi ivunjwe maana hela zinazotumika kwa mishahara na uendeshaji zingeweza kupelekwa kwenye mambo mengine ya muhimu (kama serikali inayo hayo ya muhimu).:A S cry:.
   
Loading...