Kihodombi Kingamba
JF-Expert Member
- Feb 9, 2016
- 243
- 108
Nimesoma leo kwenye gazeti la nipashe habari zenye matumaini makubwa kwa taifa letu zikisema kuwa ujenzi wa bomba la mafuta kwenda Uganda utaanza mwezi August mwaka huu.
Hizi kwangu mimi ni taarifa nzuri katika misingi kwamba serikali yetu kweli sasa imedhamiria kuitumia mianya yote muhimu kwa haraka ili kujenga uchumi wetu.
Tumezoea miaka iliyopita kuona mipango kama hii yenye kuleta matumaini kwa nchi yetu inachukua miaka mingi wakati fulani bila hata kutekelezwa.
Ni juzi tu tulimsikia Rais wetu mpendwa mara baada ya kikao cha wakuu wa Nchi za Afrika mashariki kwisha akatujuza kuwa wamekubaliana na Rais Mseveni kuwa bomba la kusafirisha mafuta litajengwa toka bandari ya Tanga.
Leo watendaji wake wamedai wanafanya kazi usiku kucha kuhakikisha bomba hili linaanza kujengwa ifikapo August mwaka huu.
Wataalamu hao wameeleza kuwa hata mabomba yatakayolazwa yataletwa hapa nchini kupitia bandari hiyo hiyo ya Tanga.
Inamaanisha bandari yetu itakuwa busy. Nimpongeze Mheshimiwa Rais wetu kwa ufanisi uliobobea na tunakuomba zinapotokea fursa kama hizi usizilazie damu maana ndio ukombozi wetu.
Ajira kwa watu 15000 sio mchezo achilia mbali na mambo mengine ya ushuru wa mafuta yenyewe kwa kupitia kwetu.
Wakenya sasa wanalalamika sana kwa uamzi uliofanywa maana walitegemea sana mradi huo upite kwao kama walivyofanya ujenzi wa reli inayotumia umeme ili kuteka biashara iliyokuwepo tangu awali ya kusafirisha mizigo ya waganda kupitia reli ya kati ambayo tangu 2000 nimekuwa nasikia tutajenga reli ya kisasa mpaka leo hii ni wimbo tu.
Kilichonikatisha tamaa zaidi ni pale nilipomsikia waziri wetu wa fedha aliposema kama tutajenga kwa kutumia fedha zetu za ndani (bajet) tutatumia miaka 300 kuimaliza. Labda mheshimiwa utachukua hatua.