Kweli pale penye maumivu, ndo utamu ulipo

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,503
25,117
Hi guys,

Mwajionaje na hali? How's weekend outta there? Natumaini mnaendelea tu poa, so am I.

Nimejiuliza nikashindwa kupata jibu hivi ni kwanini pale tunapoumizwa na kupatesekea sana ndo pahala amani yetu ya mioyo inapopatikana? Mtu ashauriwe hata kirumi bado atarudi tu mulemule.

Nitasemea haya matukio machache kati ya mengi yaliyopo.

Tukio la 1: Nilikuwa nina rafiki yangu ana mtu wake walikuwa wanapendana sana, (hii ni tofauti na ile niliwahi iletea bandiko humu maana wale waliachana). Sasa this couple wameishi kwa muda kweli wakiwa kwenye mapenzi yale ya kihindi na kifilipino kabisa.

Kama kawaida kashetani kakaingilia kati, dada akaanza kupigwa, mwanzoni vilikuwa vipigo romantic vile ambavyo haviumi sana, ila as days passes by akaanza pigwa kweli ile ya mikanda mpaka kuvimba na imagine ni keupe pee.

Sasa kipigo kikubwa kabisa huyu rafiki yangu huyu akawa ananificha maana nilishamshauri sana ila anampotezea kidogo then anarudi, kapigwa mpaka ngozi haifai imeharibika, halafu kakaa humo ndani mwanaume anamkanda mwenyewe, hajasema kwa yeyote yule. Akaja nitumia picha baadaye kabisa, kiukweli nililia nikaleta noma sana. Akanambia kaniomba msamaha nimeshamsamehe, wakati hapo me nina hasira kama vile nimepigwa mimi. Matokeo yake binti sahii ana mimba ya yule mshkaji kuuubwa, nakaribia zangu kuwa auntie.

Tukio la 2: Nina jirani yangu wa kiume huwa ananichukulia kama dada yake, he was dating this girl yaani ako humble na ni wife material hasa jamani, mstaarabu mpaka basii! Anakuja anamfanyia kila kitu kijana wa watu,

Mwisho wa siku, this guy nafsi inamsuta maana binti wa watu kawiva kwa ndoa naye hana mpango wa kuoa leo wala kesho wala mwakani kwa mipango yake, so akaona kama anamchelewesha dada wa watu kupata mtu sahihi na wakati binti tayari anajua huyu ndo mumewe,

Ikabidi amuite amuambie ukweli akipata mtu sahihi aolewe tu, sababu yeye wazazi wake wamegoma aoe mkoa aliopo tofauti na kabila lao (hapa alidanganya). Dada wa watu alilia kidogo achizike,

Kijana akaniomba dada please talk to her, me hapa nitampotezea tu muda.! Wengine ushauri ndo vitengo vyetu, nikaongea na yule dada jamani mpaka nikaona ushauri unanirudia. Zile za muache tu MUNGU atakupatia mtu sahihi.

Haya mwana kiranga mie baada ya siku chache naamka asubuhi, napishana na binti na kanga yake moja koridoni asubuhi na mapema. Washarudiana.

Tukio la mwisho: Ndugu yangu anamdate huyo kaka ni mnywaji kupindukia, inafikia pahala pesa za mrembo ndo zinatumika kula bata na rafiki zake, na akirudi anamuhadithia walivyolewa.

Mrembo anaenda kwake ndo anaitake care ile nyumba kama yake, akitoka hapo analalamika guy hamsaidii wala kumjali kwa chochote kile hata siku moja! Binti yeye ndo anadangwa anavumilia kisa kaahidiwa ndoa so anahisi anapimwa uvumilivu.

Anakuja analalamika, unamshauri weeh' mpaka maneno ya busara yanakuishia, siku 2 3 kesharudi na hakuambii mpaka apigwe tukio tena!

Ukimuuliza hivi tulikubalianaje? Anakujibu 'sasa mumie me nitafanyaje'? So, I was like okay, this time pambana tu, muombee atabadilika.

Nilichojifunza saa hii, mtu akiniletea kesi yake ya mahusiano namuambia kuwa mvumilivu tu utayashinda, Kumshauri mtu tena eti 'achana naye', Mimi? Hapana kila mtu sasa hivi anyanyasike zake tu mpaka aondoke mwenyewe, nimekoma.

Ni mwendo wa 'maumivu per day', kila mtu aubebe msalaba wake mpaka Golgotha..

Nice Weekend dears.
 
Watu singo, watu broke, watu walio na huzuni, watu wenye manyanyaso ya mwili na akili ni washauri wazuri sana..

Reason behind,huwa hawapendi kuona watu wengine kupitia kwenye tabu walizomo. Je wewe uko kundi gani dadaa..

Itakuwa upo singo weewe..:(:(:(:(:(:(
 
Nilishasema binadamu tukifanikiwa kuzi control hisia zetu kwa kutozipa nafasi ya kutuongoza kwenye kufanya maamuzi, hakika tutakuwa tumepunguza possibility ya kuumizwa kwenye mapenzi kwa asilimia nyingi mno.

Mara nyingi tunaumizwa kwa sababu tunaruhusu our emotions to cloud our sense of judgment in the situation that needs sensibility mostly.

Hisia ndio kitu ambacho kinatupa pleasure kwenye mahusiano lakini pia ndio kitu ambacho kinatupa mateso. Unakuta mtu yuko kwenye mahusiano na mtu ambaye ana mnyanyasa, anamsaliti yaani anamfanyia vitimbwi vya kila aina lakini anaishia kulalamika tu wala haondoki.

Yote hiyo ni kwa sababu upendo(hisia zake) umemuweka kwenye cage ya mtu huyo na hawezi kuondoka. Na mpaka anafikia hatua ya kukaa kwenye cage ni baada ya sensibility/akili kufunikwa na hisia wakati wa maamuzi.

Binafsi mimi najiitahidi sana nitumie zaidi akili hata kwa haya yanayoitwa mapenzi, yaani kila nnachoamua nakipitisha kwanza kwenye logical table. Inaniepusha na hayo mabalaha kama unayoelezea hapa kwenye mada.
 
Back
Top Bottom