Kweli pale penye maumivu, ndo utamu ulipo

Kweli pale penye maumivu, ndo utamu ulipo

I know ni lawama, you know some relationships are not stairways to marriage eh?
We all do knows that, ila inashindikana nini kumuambia muhusika ukweli kuwa we are only having fun? No strings attached?
 
Padre mmoja baada ya kumuozesha mdogo wake .

Dada na mumewe maisha yalikua mazuri sana mwanzoni

Mara kipigo kikaanza..mdada anapigwa utadhan mbwa.

Akirudi kwa kaka yake Padre ...Jamaa anamsomea mafungu ya Biblia ,mdada anasamehe anarudi.

Siku zinaenda anapigwa kipigo cha mbwa koko, Mdada anaenda kwa kaka yake, anamwambia Nitauliwa ..Jamaa anasoma Bible, kisha anamwambia "Huna kazi, hujasoma" unataka kua mzigo wanani????.


Mwisho mdada kila akipigwa, akawa anaishia kulilia ndani mwake, na akawa haendi tena kwao wala kwa kaka yake...isipokua akawa anaandika.


Nikatika kutafuta kisa cha Mdada huyu kufa, zilikutwa BARUA 13 ikimanisha Vipigo kwa siku tofaut 13, na Barua ya Mwisho akawa ameandika

"Kaka, Nimepigwa sana Hapa nilipo Kichwa na tumbo ,mbavu zinaniuma sana , sina wakunipeleka Hosp, kwasasa hata nikikojoa naona Damu".



Padre siku ya Mazishi ..ndo watu walijua kumbe hata watumishi hawa Wana Hasira[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]



Nadhan, kwa Mwanamke Huru, anayejiamin, asotetereka, ambaye kwake Maisha ni Uhai........ .......... Hawezi kaaa vumilia Kipigo cha aina hiii.


Jana nikiwa Kazin, analetwa Mmama wa miaka 43 na kaka yake, mmama hata kuhema hawez, ukimgusa Mikono analiaa..ukigusa tumbo analia..ukigusa mbavu. Mgongo, kichwan yaan nikulia , kavimba mwili wote ...

Nikauliza nini??? Et Mumewe alikua anampiga na kuni Juzi, Lijamaa likakataa katakata kumleta Hosp, Majiran ndo kumpigia simu Kaka wa Mwanamke, Kaka kaja kambeba Mdogo wake kaenda polisi kwa pf3 , ndo sasa akamleta .

Bahati nzuri kwa vipimo nlivoagiza, Mama hajapata tatizo hatarishi.


Kuna kakipigo..kuna kipigo..kuna Likipigo...... Acheni ujinga,, Alochomwa na Gunia la Mkaa, hakuchomwa akiwa hai.... Bali alipigwa kipigo, kikafuata Likipigo ndo akafariki.... Kwaiyo swali la wapi nimpeleke???nikifukia mifupa wataipata..nifanyaeje??? "Ndo lilipelekea Jamaa kumchoma kwa Gunia mbili".


#wanawake pambaneni kua Huru, kwa mwanaume mjinga? Ili akuheshimu ni lazima Uwe na cha kwako[emoji23][emoji23]..mtabisha ila ukweli ndio huoooo.......

Na km umeolewa/Uliozeshwa kwa kupunguza mzigo/upepo wakisulisuli...ndo hayo yanawakuta.
Hua nashangaa mtu anavumiliaje kupigwa,
kitendo cha kupiga ni kumtoa thamani mpigwaji na kitendo cha kuvumilia kupigwa ni kujitoa thamani na utu, yaan mtu anajiona si kitu mbele ya mtu, amejidharau.

Wanawake wa kiafrica wanastahili ukombozi kwenye hili suala.
 
Kwani wewe uko tayari kumuacha akupendaye kirahisi rahisi??
 
My bestfriend alini video call namuona jicho limevimba anasema boyfriend kampiga, acha nipanic, nikamcall her boyfriend hapokei nikasend a voice note nilimpa sio maneno bali mijineno mizito mizito,

After a week naona wamepostiana kwenye status, "girl whaaat!!?" ananiambia the guy alijirudi and is so sweet kwa sasa, mie eeh na vipi ile voice note yangu nilomtumia eti ooh usijali ameelewa ulikua unani defend as a bestfriend, nikamwambia "bitch, next time anakunyofoa jicho don video call me go back to him na umuombe akuweke la mbuzi muendelee kupostiana"
Inaumiza sana kwakweli, so at the end wewe ndo unaonekana snitch wa mapenzi ya watu.! Mimi sahii sishauri mtu vibaya tena, kila mmoja apambane tu na furushi lake.!
 
We all do knows that, ila inashindikana nini kumuambia muhusika ukweli kuwa we are only having fun? No strings attached?

Unajua ni nini? Mara ya kwanz akwanza unaweza ukasema hapa ndio natia nanga sing'oi,but as the time goes unaona kabisa huyu tutashindwana hko mbele,its not that humpendi,its just the fact kumbe unapemda future yako and not troubles kwa mtu usiweza kumbasilisha. Sasa unamwambia but yeye ndio haelewi,na kubadilika habadiliki. What u gonna do?
 
dah'...!!
It's a way touching kwakweli, kitendo cha kupigwa kila siku and still mtu bado unarudi ulipopigika mie siafikini nako!
Na ile mindset ya 'ndoa ni uvumilivu' tunaitumia vibaya sana nadhani.! Utavumiliaje vipigo kila siku!
Kuna tofauti kubwa sana kati ya uvumilivu na ujinga nadhani hapo ndo tunashindwa tofautisha.!!

Hilo suala la wanawake kuwa huru, subiri kushukiwa hapa kama mwewe.!! [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]wao wanishukie tu..watabisha ila huo ndo ukweli..

Kwa mwanaume Asokua na akili.,, basi ili akuheshimuu lazima uwe nankazi au shuguli yako inayokuingizia kipato.

Kwa mwanaume makini, kutokua nakazi au kipato sio shida.
 
Nadhani pia unajua kuwa kuna watu wanaamini katika kuyafurahia maisha ya mahusiano bila kuweka kigezo cha ndoa?


Wapo lakini sio wengi,mini huwa kila mahusiano niliyokuwa nayo nilitamani iishie mpka kwenye ndoa lakin huwa something come in between, usaliti, non compactibility, irresponsibility and others.... I dont consider having fun kama justification ya kuwa-na au kuhitaji relationship.
 
Hua nashangaa mtu anavumiliaje kupigwa,
kitendo cha kupiga ni kumtoa thamani mpigwaji na kitendo cha kuvumilia kupigwa ni kujitoa thamani na utu, yaan mtu anajiona si kitu mbele ya mtu, amejidharau.

Wanawake wa kiafrica wanastahili ukombozi kwenye hili suala.
Hihih Pacha, ndo mambo ya mwanamke kuolewa kwa sababu Umri umeenda, presha za wazazi na upepo wa kisulisuli...

Hakupata muda wakuchunguza mtu sahihi kwake.


Hahaha, wao wanasema..."Mwanaume ndio Muoaji, sisi ni waolewaji"

Sasa mimi ni mwanaume...muoaji..namimu niwambie..." Mwanamke ananafasi kubwa ya kuchagua kile kilicho bora"[emoji23]
 
Unajua ni nini? Mara ya kwanz akwanza unaweza ukasema hapa ndio natia nanga sing'oi,but as the time goes unaona kabisa huyu tutashindwana hko mbele,its not that humpendi,its just the fact kumbe unapemda future yako and not troubles kwa mtu usiweza kumbasilisha. Sasa unamwambia but yeye ndio haelewi,na kubadilika habadiliki. What u gonna do?
tell her the truth and let her be free!!

you're forcing me to say this lakini.!! At the end usije niona me ndo mvurugaji, muombee tu mkuu atabadilika!
 
Hakuna akili iwezayo kuzidhibiti hisia ktk ulimwengu huu....
Kidogo walioteswa na mapenz wanaweza kias2, kama huyu mtoa uzi...
mapenz yanasahaulisha maumiv makubwa na majuto uloyapata kwa some1 ndan ya mda mchache....
Haha..!!
Nimependa hapo eti 'kama huyu mtoa uzi'..!! Hapa naomba Lizarazu aje kutusaidia maana alisema tunapaswa ku control hisia.
 
Hi guys,
Mwajionaje na khali.? How's weekend outta there??
Natumaini mnaendelea tu poa, so am I..!!

Nimejiuliza nikashindwa kupata jibu hivi ni kwanini pale tunapoumizwa na kupatesekea sana ndo pahala amani yetu ya mioyo inapopatikana? Mtu ashauriwe hata kirumi bado atarudi tu mulemule!

Nitasemea haya matukio machache kati ya mengi yaliyopo.!!

tukio la 1, nilikuwa nina rafiki yangu ana mtu wake walikuwa wanapendana sana, (hii ni tofauti na ile niliwahi iletea bandiko humu maana wale waliachana)..! Sasa this couple wameishi kwa muda kweli wakiwa kwenye mapenzi yale ya kihindi na kifilipino kabisa!
Kama kawaida kashetani kakaingilia kati, dada akaanza kupigwa, mwanzoni vilikuwa vipigo romantic vile ambavyo haviumi sana, ila as days passes by akaanza pigwa kweli ile ya mikanda mpaka kuvimba na imagine ni keupe pee'..!!

Sasa kipigo kikubwa kabisa huyu rafiki yangu huyu akawa ananificha maana nilishamshauri sana ila anampotezea kidogo then anarudi, kapigwa mpaka ngozi haifai imeharibika, halafu kakaa humo ndani mwanaume anamkanda mwenyewe, hajasema kwa yeyote yule! kaja nitumia picha baadaye kabisa, kiukweli nililia nikaleta noma sana..!!
Akanambia kaniomba msamaha nimeshamsamehe, wakati hapo me nna hasira kama vile nimepigwa mimi,.
Matokeo yake binti sahii ana mimba ya yule mshkaji kuuubwa, nakaribia zangu kuwa auntie,

tukio la 2, nina jirani yangu wa kiume huwa ananichukulia kama dada yake, he was dating this girl yaani ako humble na ni wife material hasa jamani, mstaarabu mpaka basii! Anakuja anamfanyia kila kitu kijana wa watu,

Mwisho wa siku, this guy nafsi inamsuta maana binti wa watu kawiva kwa ndoa naye hana mpango wa kuoa Leo wala kesho wala mwakani kwa mipango yake, so akaona kama anamchelewesha dada wa watu kupata mtu sahihi na wakati binti tayari anajua huyu ndo mumewe,

Ikabidi amuite amuambie ukweli akipata mtu sahihi aolewe tu, sababu yeye wazazi wake wamegoma aoe mkoa aliopo tofauti na kabila lao(hapa alidanganya).. Dada wa watu alilia kidogo achizike,

Kijana akaniomba dada please talk to her, me hapa nitampotezea tu muda.! Wengine ushauri ndo vitengo vyetu, nikaongea na yule dada jamani mpaka nikaona ushauri unanirudia.!! Zile za muache tu MUNGU atakupatia mtu sahihi..!!

Haya mwana kiranga mie baada ya siku chache naamka asubuhi, napishana na binti na kanga yake moja koridoni asubuhi na mapema.! Washarudiana.!!

tukio la mwisho, ndugu yangu anamdate huyo kaka ni mnywaji kupindukia, inafikia pahala pesa za mrembo ndo zinatumika kula bata na rafiki zake, na akirudi anamuhadithia walivyolewa!

Mrembo anaenda kwake ndo anai take care ile nyumba kama yake, akitoka hapo analalamika guy hamsaidii wala kumjali kwa chochote kile hata siku moja! Binti yeye ndo anadangwa anavumilia kisa kaahidiwa ndoa so anahisi anapimwa uvumilivu.!

Anakuja analalamika, unamshauri weeh' mpaka maneno ya busara yanakuishia, siku 2 3 kesharudi na hakuambii mpaka apigwe tukio tena!

Ukimuuliza hivi tulikubalianaje?? Anakujibu 'sasa mumie me nitafanyaje'..?? So, I was like okay, this time pambana tu, muombee atabadilika.!!

'Nilichojifunza sahii, mtu akiniletea kesi yake ya mahusiano namuambia kuwa mvumilivu tu utayashinda, Kumshauri mtu tena eti 'achana naye', Miiimi?? Hapana kila mtu sahivi anyanyasike zake tu mpaka aondoke mwenyewe, nimekoma'..!!

Ni mwendo wa 'maumivu per day', kila mtu aubebe msalaba wake mpaka Golgotha..

Nice Weekend dears!
Nina nawasiwasu wewe hujaolewa na ndio maana kila anaekuomba ushauri unamwambia eti waachane huona kama wewe ndo unachangia wapendanao wavurugane zaidi
 
[emoji23][emoji23][emoji23]wao wanishukie tu..watabisha ila huo ndo ukweli..

Kwa mwanaume Asokua na akili.,, basi ili akuheshimuu lazima uwe nankazi au shuguli yako inayokuingizia kipato.

Kwa mwanaume makini, kutokua nakazi au kipato sio shida.
Wanakuja mkuu, andaa tu juice na popcorn zako!!
Kwa jinsi dunia ya sasa inavyokwenda kasi na maisha yalivyobadilka naona kila kitu kinaenda shaghala baghala.!!
 
tell her the truth and let her be free!!

you're forcing me to say this lakini.!! At the end usije niona me ndo mvurugaji, muombee tu mkuu atabadilika!


The worst thing is that, i am not ready to have her as a w*f*,and she doesnt accept that fact....She is now using my friends to getvto me again since i stopped communicating with her.... I dont want to torture her in anyway, i thought it will go smoothly..😐
 
Back
Top Bottom