Kweli Mungu hana upendeleo?

Kweli Mungu hana upendeleo?

Ni nani aliyeumba uovu kwa mara ya kwanza kabisa?
Swali la “nani aliyeumba uovu kwa mara ya kwanza” hutokana na kudhani kuwa uovu ni kitu kilichoumbwa kama vilivyoumbwa mbingu, ardhi au viumbe hai. Lakini kwa uhalisia, uovu si kiumbe wala kitu kinachojitegemea; uovu ni matokeo ya kuacha haki au kutumia vibaya uwezo ambao viumbe wamepewa. Mwenyezi Mungu ameumba viumbe na kuwapa akili, uwezo wa kuchagua, na njia mbili, njia ya mema na njia ya mabaya.

Hivyo, Mwenyezi Mungu ameumba uwezo wa kuchagua, lakini hakumlazimisha kiumbe kuchagua uovu. Uovu hutokea pale kiumbe kinapotumia vibaya uhuru huo. Ni sawa na mwanga na giza: mwanga unapokosekana ndipo giza linaonekana. Vivyo hivyo, mema yanapokosekana katika matendo ya viumbe ndipo uovu hujitokeza.

Kwa hiyo kusema Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba uovu kama kitu cha kwanza si sahihi. Mwenyezi Mungu ameumba uhai, akili, na uwezo wa kuchagua; lakini uovu unatokana na maamuzi ya viumbe wanapotoka kwenye haki. Ndiyo maana historia inaonyesha kuwa uovu mwingi duniani unatokana na matendo ya viumbe wenyewe, dhuluma, tamaa, chuki na udhalimu.
 
Ukisema uovu unatokana na dhuruma, tamaa, chuki na udhalimu unamaanisha nin?, kwasababu hayo matendo ndiyo uovu wenyewe.

Kama Mungu hajaumba uovu sasa hiyo akili ya kutenda uovu shetani aliitoa wapi?

Ukisema Mungu ametupa uhuru wa kuchagua kati ya wema na ubaya halafu bado unadai ubaya hajauumba yeye, sasa kwanini ameuweka kwenye machaguo?
 
Na kama Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu kama inavyoelezwa katika Yohana 3:16, kwa nini bado kuna mafundisho ya hukumu na adhabu ya milele kama katika Mathayo 25:46?
YESU kufa kwa ajili yetu ni kama alikuja wakati hakimu anakukuhumu kifo, YESU akasema usimuue huyo jamaa, niue mimi.

Au hakimu alisema hukumu yako ni kulipa Bilioni moja, YESU akaja akasema usimdai nitalipa mimi.

Sasa ukikataa ukasema mimi sitaki sitamtambui huyo jamaa, sitaki msaada wake, what do you expect? ?

MUNGU anataka ushirika wa hiari.

By the way,
ukichunguza vizuri maandiko, ni kwamba wasiomtaka MUNGU wataondolewa wasiwepo milele. Sio kuwa watakaa wanachomwe milele kama mishkaki isiyoiva.

Post in thread 'Ikiwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako lakini hakubaki amekufa, basi lengo lilikuwa nini?' Ikiwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako lakini hakubaki amekufa, basi lengo lilikuwa nini?
 
Kiufupi Mungu wa hizi dini anaenjoy sana kuona watu wakiteseka,
MUNGU aliingia hapa duniani unajua watu walichomfanya? ? ?

MUNGU ameshiriki mateso pamoja nasi.

Focus on the bigger picture. Ni muda mchache sana ametoa kwa ajili ya wateule kujua mema na mabaya. It's a painful process, lakini ni muda mfupi sana! !

Shetani amefanikiwa kudanganya watu wasio makini kuwa ni muda mreeefu, mamilioni ya miaka! !

Baadaye kwenye umilele tukisemam "mabaya" , tunajua mabaya ni nini in real time, sio tumesimuliwa, tumeona kwa macho yetu na tumepitia wenyewe.

Jishikilieni!

Ukombozi umekaribia!

Listen to this man of GOD:

View: https://www.instagram.com/reel/DVnyfeCGv7c/?igsh=Z3ZudmtqNDl5ZW9n
 
Kama mepesi mbona wewe huna majibu yake?
Sio kila kitu mimi najua hata wewe pia kama hujui wengine wana
YESU kufa kwa ajili yetu ni kama alikuja wakati hakimu anakukuhumu kifo, YESU akasema usimuue huyo jamaa, niue mimi.

Au hakimu alisema hukumu yako ni kulipa Bilioni moja, YESU akaja akasema usimdai nitalipa mimi.

Sasa ukikataa ukasema mimi sitaki sitamtambui huyo jamaa, sitaki msaada wake, what do you expect? ?

MUNGU anataka ushirika wa hiari.

By the way,
ukichunguza vizuri maandiko, ni kwamba wasiomtaka MUNGU wataondolewa wasiwepo milele. Sio kuwa watakaa wanachomwe milele kama mishkaki isiyoiva.
Yeye si anajua mwanzo na mwisho kwa hiyo alijua kuna kundi la watu watakaomkataa
Then awageuze mishikaki🙌
 
Sio kila kitu mimi najua hata wewe pia kama hujui wengine wana

Yeye si anajua mwanzo na mwisho kwa hiyo alijua kuna kundi la watu watakaomkataa
Then awageuze mishikaki🙌
Yes alijua kuna watu wangemkataa pamoja na yote mazuri aliyoahidi kuwapa: uhai wa milele wenye furaha milele!

So wataondolewa! ! !

Ni kama mwansume amuahidi mwanamke atampa kila kitu anachotaka maishani mwake, akikubali kuolewa naye. Mwanamke akakataa.

Basi! Offer imepita!

Ndomana kanisa linaitwa Bibi harusi. Ni wale waliokubali offer.

Kwanini usikubali tu offer uka enjoy life forever?

Kwanini uchague kulalamika, kulaumu? Kwanini uchague mabaya?

Si uchague mazuri, ya raha ! !

It's literally in your hands! ! !
 
Ukisema uovu unatokana na dhuruma, tamaa, chuki na udhalimu unamaanisha nin?, kwasababu hayo matendo ndiyo uovu wenyewe.

Kama Mungu hajaumba uovu sasa hiyo akili ya kutenda uovu shetani aliitoa wapi?

Ukisema Mungu ametupa uhuru wa kuchagua kati ya wema na ubaya halafu bado unadai ubaya hajauumba yeye, sasa kwanini ameuweka kwenye machaguo?
Kwanza tufikiri kwa utulivu.
Uovu si kitu kilichoumbwa kama kiumbe au kitu kinachojitegemea. Uovu ni matokeo ya kuacha kufanya mema au kutumia vibaya uwezo tuliopewa.

Hebu jiulize:

Kama mtu amepewa akili, nguvu na uwezo wa kufanya jambo jema, halafu akaamua kutumia uwezo huo kudhulumu au kuonea, je, uovu umetoka kwa Mwenyezi Mungu au umetokana na maamuzi ya huyo mtu?

Fikiria mfano rahisi:
Kisu kimetengenezwa kwa ajili ya kukata chakula. Lakini mtu akakitumia kumdhuru mwenzake, je, tutasema mtengenezaji wa kisu ndiye aliyeumba uhalifu huo, au tatizo liko kwa aliyekitumia vibaya?

Sasa tafakari swali lingine muhimu:
Kama Mwenyezi Mungu angeumba viumbe wasioweza kabisa kufanya makosa, wasioweza kuchagua, je, hao bado wangekuwa na hiari, au wangekuwa kama mashine zinazofanya zilichopangiwa tu?

Na kama hakuna uwezekano wa kuchagua ubaya, je, wema ungekuwa na thamani gani?
=>Kwa sababu wema wa kweli hutambulika pale ambapo mtu ana uwezo wa kufanya mabaya lakini anachagua mema.

Kuhusu swali lako la kusema: “Kama ubaya haujaumbwa na Mwenyezi Mungu kwa nini umewekwa kwenye machaguo?”
Jiulize tena:
Je, kuwepo kwa uwezekano wa kufanya kosa ni sawa na kusema kosa lenyewe limeumbwa na kulazimishwa?

Au ni sehemu ya kuwapa viumbe uhuru wa kuchagua?
Kwa hiyo ukweli ni huu:
Mwenyezi Mungu ameumba uwezo, akili na uhuru wa kuchagua. Lakini uovu hutokea pale viumbe wanapotumia vibaya vipawa hivyo.

Ndiyo maana swali la mwisho la kutafakari ni hili:
Je, ulimwengu wa viumbe wenye hiari wanaoweza kuchagua mema kwa utashi wao una hekima zaidi, au ulimwengu wa viumbe wasiokuwa na uwezo wa kuchagua chochote?
 
Yes alijua kuna watu wangemkataa pamoja na yote mazuri aliyoahidi kuwapa: uhai wa milele wenye furaha milele!

So wataondolewa! ! !

Ni kama mwansume amuahidi mwanamke atampa kila kitu anachotaka maishani mwake, akikubali kuolewa naye. Mwanamke akakataa.

Basi! Offer imepita!

Ndomana kanisa linaitwa Bibi harusi. Ni wale waliokubali offer.

Kwanini usikubali tu offer uka enjoy life forever?

Kwanini uchague kulalamika, kulaumu? Kwanini uchague mabaya?

Si uchague mazuri, ya raha ! !

It's literally in your hands! ! !
Sawaa🙏
 
Elimu ya Geography kuhusu soil formation haipingani na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Sayansi inaeleza jinsi mambo yanavyotokea, lakini mara nyingi haiwezi kueleza kwa nini mfumo huo upo au nani aliweka kanuni zake. Soil formation inaeleza mchakato wa kuvunjika kwa miamba, hali ya hewa, na viumbe hai kuunda udongo kwa muda mrefu. Lakini kuwepo kwa sheria hizo za asili na mpangilio wake bado ni swali la kina zaidi kuhusu chanzo chake.
Kwa hiyo kusoma soil formation hakumwondolei mtu uwezo wa kumtukuza Mungu; badala yake kwa wengine huongeza mshangao kuhusu mpangilio wa ulimwengu. Sayansi inaeleza taratibu za asili, lakini watu wengi wanaona taratibu hizo pia kama sehemu ya hekima ya Muumba.
Elimu ya Geography inapingana na ulichokiandika.

Hakuna mbingu kwenye Geography.

Sayansi INAPINGANA na Imani za kidini.

Unachokifanya kutaka kuifanya SAYANSI iwe compatible na Imani yako ni matokeo ya kitu kinachoitwa kitaalamu kama "Cognitive Dissonance".

Cognitive Dissonance: Is the psychology tension that arises when someone holds two conflicting beliefs at the same time. To resuce the discomfort, people often try to make the beliefs compatible, even if it means rationalizing or adjusting one of them.

Kuhusu chanzo cha Ulimwengu: Hilo ni swali linaloweza kujibiwa na sayansi pekee na wala siyo kwa stori za kale za kidini.

Mungu/Muumba anaweza kuwapo, ila hawezi kuwa yule anayezungumzwa misikitini, makanisani, mahekaluni, nk, Because Those Gods are Incompatible with the Physical Reality.

Kwa maelezo zaidi soma kitabu hiki.
Faith Versus Fact: Why Science and Religion Are Incompatible, by Jerry Coyne
 
Kama viumbe wenye UTASHI tunapaswa kutumia AKILI zetu vizuri tulizopewa na Mama-Asili kusahihisha yale yanayosababisha Maumivu, na Kutengeneza yale yanayosababisha Furaha na Amani....
 
Kwa sababu hekima ya Mungu ni kubwa kuliko uwezo wa akili ya mwanadamu kuielewa kikamilifu
Hakuna kitu kama hiko kila kitu kina tafsiri

Emotion kila kitu inawezekana kwakuwa chaguzi ni mbili tu kurutubisha au kuharibu

Ila kimaumbile ni infinity ni upuuzi kutafsiri mambo huku
 
Back
Top Bottom