Kweli Mungu hana upendeleo?

Kweli Mungu hana upendeleo?

Kama una mzungumzia Mungu wa Utatu Mtakatifu (Trinitarian God) huyo hayupo hivyo hayo yanayosemwa juu yake ni UONGO.

Mateso na Uovu uliopo Dunia ni matokeo ya matendo ya viumbehai.

Mfumo wa Asili hautambui Maadili, kwake hakuna chema wala kibaya. Mfumo upo kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kujiendesha.

Virusi na Bacteria vinategemea viumbe hai kama binadamu kupata chakula na kuzaliana, Virusi na Bacteria hawana lengo la kusababisha maradhi, lengo lao kuu ni Maisha.

Tetemeko la Ardhi ña Majanga mengine ya Asili wakati dunia inapokuwa kwenye harakati za kujiendesha kupitia "plate tectonic movements", matokeo ya majanga hayo yaweza kuwa VIFO vya viumbe, ila kiasili ni faida kwasababu VIFO hivyo vitafanyika kuwa CHAKULA kwa viumbe wengine, matengenezo ya ardhi, matengenezo ya hewa ya oksijeni, nk.

Nature is neither immoral nor moral, only pitiless indifferent.

Kama viumbe wenye UTASHI tunapaswa kutumia AKILI zetu vizuri tulizopewa na Mama-Asili kusahihisha yale yanayosababisha Maumivu, na Kutengeneza yale yanayosababisha Furaha na Amani.

When Science and Reason is Used to its Maximum Potential, the Earth can become unimaginable Heaven.
Huyo huyo wa utatu mtakatifu ambae amesema anajua mwanzo na mwisho kwahiyo kila kinachotokea anajua

Mfano alijua zamani kabra ya kuzaliwa kua nitakua muuwaji kwann sasa asingezuia hilo lisitokee badala yake anakuacha ufanye ili akakuchome moto?
 
Mungu wa hizi dini anao upendeleo hili wala halihitaji akili nyingi kulijua, ndiomaana kuna wahuni pamoja na makandokando yao hutowai kuona wakiteseka, ila kuna wewe apo mateso ni sehemu ya maisha yako, pia kuna watoto wadogo wasiojua lolote ovu lkn mabaya yanawakuta, kuna wale wanakesha kumuomba huyo Mungu usiku na mchana lkn mabaya yamekuwa sehemu ya maisha yao

Kiufupi Mungu wa hizi dini anaenjoy sana kuona watu wakiteseka, kuna muda anashirikiana na kijana wake shetani kuwahujumu wanadamu kwa mitego na mapito magumu ili waanguke apate sababu ya kuwahukumu.

Mungu wa dini hatabiriki, kwenye vitabu vyake anasema hili na kiuhalisia anatenda tofauti kabisa, yaani hana mazoea wala ushikaji na kiumbe chochote kiitwacho binadamu.

Mungu wa ukristo na uislamu ni mzushi kaundwa na wazungu/waarabu kwa madhumuni ya kuharibu fikra za watu watawalike kiwepesi (Allah& Yehova/yesu hawa ni viumbe wa kusadikika tu hawapo na hawatowai kuwepo)
 
Nakupa mfano, kijana kazaliwa daslam ana ujua umeme, magari, shule ziko hapo.

Mwingine kazaliwa kazula mimba, yebo ya shilingi elfu 3 ni miracle kwake.
Maji machafu, nyumba ya tope, shule iko km 200 huko.

Still ako fair ehh?
 
cocastic nina popcorn 🍿 tayari, njoo tujisomee zetu comments.

giphy.gif
 
Yaan umenyooka 🤝na ukihoji unaoneka una kufuru me before nilikua Muslim nikachoka vitisho maana kule unatishwa mpaka unachanganyikiwa , Ajabu huku nako naona mazingaombwe😎

Chomezo: niliwahi kuigiza nimepandisha wakati naombewa na mchungaji akawa anakemea 😂😂 kwann hakushtukia mchongo🙌
Nakupa mfano, kijana kazaliwa daslam ana ujua umeme, magari, shule ziko hapo.

Mwingine kazaliwa kazula mimba, yebo ya shilingi elfu 3 ni miracle kwake.
Maji machafu, nyumba ya tope, shule iko km 200 huko.

Still ako fair ehh?
Ajabu hii
 
Mwingi wa rehema mwingi wa huruma ?
Sasa mbona watu wanakula msoto wa magonjwa umasikini mpka wanatapeliwa na kina mwamposa kutumia jina lake na amekaa kimya?
Rehema na huruma ya Mwenyezi Mungu haimaanishi kwamba dunia itakuwa mahali pasipo na majaribu. Maisha ya duniani yameumbwa kuwa na furaha na huzuni, afya na maradhi, utajiri na umasikini. Hali hizi huwa sehemu ya mtihani wa maisha ya mwanadamu, si ishara kwamba Mungu amekosa huruma. Rehema yake inaonekana kwa kuwapa wanadamu uhai, akili ya kutambua mema na mabaya, na nafasi ya kubadilika kila siku.

Kuhusu watu kuteseka kwa sababu ya matapeli wanaotumia jina la Mungu, hilo mara nyingi si kimya cha Mungu bali ni matokeo ya matendo ya binadamu wenyewe. Mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua; anaweza kufanya mema au mabaya. Watu kama wanaotumia dini kujinufaisha wanatumia vibaya uhuru huo, na dhuluma hiyo hubeba matokeo yake. Hivyo, udanganyifu wa mtu kama Josephat Gwajima Mwamposa au mtu mwingine yeyote anayehusishwa na kashfa za kutumia dini hauwezi kuwa kipimo cha huruma ya Mungu, bali ni kipimo cha tabia ya mwanadamu.

Kwa hiyo mateso mengi tunayoyaona duniani mara nyingi yanatokana na udhaifu, tamaa, na ujinga wa wanadamu, si kwa sababu Mungu hana huruma. Ndiyo maana historia inaonyesha pia kuwa pamoja na mateso, bado kuna watu wanaopona, wanasaidiana, na wanapata farajahayo nayo ni sehemu ya rehema inayodhihirika katika maisha.
 
Mkuu lile somo la "Geography" Topic ya "Soil Formation" ulisoma kweli?
Elimu ya Geography kuhusu soil formation haipingani na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Sayansi inaeleza jinsi mambo yanavyotokea, lakini mara nyingi haiwezi kueleza kwa nini mfumo huo upo au nani aliweka kanuni zake. Soil formation inaeleza mchakato wa kuvunjika kwa miamba, hali ya hewa, na viumbe hai kuunda udongo kwa muda mrefu. Lakini kuwepo kwa sheria hizo za asili na mpangilio wake bado ni swali la kina zaidi kuhusu chanzo chake.
Kwa hiyo kusoma soil formation hakumwondolei mtu uwezo wa kumtukuza Mungu; badala yake kwa wengine huongeza mshangao kuhusu mpangilio wa ulimwengu. Sayansi inaeleza taratibu za asili, lakini watu wengi wanaona taratibu hizo pia kama sehemu ya hekima ya Muumba.
 
Rehema na huruma ya Mwenyezi Mungu haimaanishi kwamba dunia itakuwa mahali pasipo na majaribu. Maisha ya duniani yameumbwa kuwa na furaha na huzuni, afya na maradhi, utajiri na umasikini. Hali hizi huwa sehemu ya mtihani wa maisha ya mwanadamu, si ishara kwamba Mungu amekosa huruma. Rehema yake inaonekana kwa kuwapa wanadamu uhai, akili ya kutambua mema na mabaya, na nafasi ya kubadilika kila siku.

Kuhusu watu kuteseka kwa sababu ya matapeli wanaotumia jina la Mungu, hilo mara nyingi si kimya cha Mungu bali ni matokeo ya matendo ya binadamu wenyewe. Mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua; anaweza kufanya mema au mabaya. Watu kama wanaotumia dini kujinufaisha wanatumia vibaya uhuru huo, na dhuluma hiyo hubeba matokeo yake. Hivyo, udanganyifu wa mtu kama Josephat Gwajima Mwamposa au mtu mwingine yeyote anayehusishwa na kashfa za kutumia dini hauwezi kuwa kipimo cha huruma ya Mungu, bali ni kipimo cha tabia ya mwanadamu.

Kwa hiyo mateso mengi tunayoyaona duniani mara nyingi yanatokana na udhaifu, tamaa, na ujinga wa wanadamu, si kwa sababu Mungu hana huruma. Ndiyo maana historia inaonyesha pia kuwa pamoja na mateso, bado kuna watu wanaopona, wanasaidiana, na wanapata farajahayo nayo ni sehemu ya rehema inayodhihirika katika maisha.
Kwann ameumba dunia kua ya furaha na huzuni na si furaha pekee ?
Kwann wakati wa huzuni siwe kwa wote yaan kwamba hii ni season ya huzuni tulie wote
Then hii ni season ya furaha tufurahi wote kwa pamoja

Hiv unajua kuna watu wao kila siku mambo ni shwari isipokua maudhi madogo?

Unajua kuna watu hawajawahi kuonja furaha hata siku nzima furaha yao ni kwa masaa kadha ?

Aisee 🙌🙌
 
Mungu anaupendeleo kuliko hata mimi nawewe

Mungu aliamua kuwapendelea wana wa Israel yaani kazi yao kuvamia nchi za watu na kuwaua watu wale kwenye mataifa yao.

Mungu alikuwa anampenda sana Musa kuliko binadamu yeyote yule pamoja na Daniel.(Huu nao ni upendeleo)

Kwenye ghalika ya Nuhu akachagua familia ya Nuhu pekee
Wengine wote akawaua hadi watoto wadogo wasio na hatia

Visa ni vingi mno vimejaa upendeleo tupu.
Yaan jamani ukihoji unakemewa et una pepo kakuvamia
 
Mungu wa hizi dini anao upendeleo hili wala halihitaji akili nyingi kulijua, ndiomaana kuna wahuni pamoja na makandokando yao hutowai kuona wakiteseka, ila kuna wewe apo mateso ni sehemu ya maisha yako, pia kuna watoto wadogo wasiojua lolote ovu lkn mabaya yanawakuta, kuna wale wanakesha kumuomba huyo Mungu usiku na mchana lkn mabaya yamekuwa sehemu ya maisha yao

Kiufupi Mungu wa hizi dini anaenjoy sana kuona watu wakiteseka, kuna muda anashirikiana na kijana wake shetani kuwahujumu wanadamu kwa mitego na mapito magumu ili waanguke apate sababu ya kuwahukumu.

Mungu wa dini hatabiriki, kwenye vitabu vyake anasema hili na kiuhalisia anatenda tofauti kabisa, yaani hana mazoea wala ushikaji na kiumbe chochote kiitwacho binadamu.

Mungu wa ukristo na uislamu ni mzushi kaundwa na wazungu/waarabu kwa madhumuni ya kuharibu fikra za watu watawalike kiwepesi (Allah& Yehova/yesu hawa ni viumbe wa kusadikika tu hawapo na hawatowai kuwepo)
Mwenyezi Mungu ni Mtukufu juu ya mawazo na hukumu za wanadamu. Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, Mmiliki wa uhai na mauti, na Mfalme wa kila kilichopo. Hekima yake ni kubwa kuliko akili za viumbe wake, na hukumu zake hazipimwi kwa mizani ya hisia za binadamu. Mwanadamu anaona sehemu ndogo ya maisha ya dunia, lakini Mwenyezi Mungu anaona mwanzo na mwisho wa kila kitu.

Utukufu wa Mwenyezi Mungu haupungui kwa sababu ya mateso ya dunia, wala hauongezeki kwa sababu ya furaha ya wanadamu. Yeye ndiye anayetoa uhai, anayetoa riziki, na anayefungua milango ya rehema kila siku. Hata wale wanaomkataa bado wanaishi kwa neema zake—wanavuta pumzi, wanakula, na wanaendelea kuishi kwa uwezo wake.

Mwenyezi Mungu ni Mkuu kuliko dhana za wanadamu, ni Mtawala wa wakati na hatima. Hakuna anayeweza kumshirikisha katika utukufu wake, wala hakuna anayeweza kupunguza mamlaka yake. Mbingu na ardhi zinamtukuza, na kila kilichoumbwa kinashuhudia ukuu wake. Yeye ndiye wa kwanza bila mwanzo, na wa mwisho bila mwisho, Mwingi wa rehema na Mwingi wa hekima.
 
Kwann ameumba dunia kua ya furaha na huzuni na si furaha pekee ?
Kwann wakati wa huzuni siwe kwa wote yaan kwamba hii ni season ya huzuni tulie wote
Then hii ni season ya furaha tufurahi wote kwa pamoja

Hiv unajua kuna watu wao kila siku mambo ni shwari isipokua maudhi madogo?

Unajua kuna watu hawajawahi kuonja furaha hata siku nzima furaha yao ni kwa masaa kadha ?

Aisee 🙌🙌
Kwanza fahamu kuwa maisha ya duniani hayakuumbwa kuwa mwisho wa furaha ya mwanadamu, bali ni sehemu ya safari. Ndiyo maana ndani yake kuna mchanganyiko wa furaha na huzuni. Kama dunia ingeumbwa kuwa furaha tupu, basi usingeweza kutambua thamani ya furaha, kwa sababu usingekuwa na kitu cha kuilinganisha nacho. Furaha hutambulika kwa sababu kuna huzuni, afya hutambulika kwa sababu kuna maradhi, na amani hutambulika kwa sababu kuna shida.

Pili, kama huzuni na furaha zingekuwa zinakuja kwa msimu mmoja kwa watu wote—leo wote tulie, kesho wote tufurahi—basi maisha yangekuwa kama ratiba ya mashine. Lakini maisha ya wanadamu yamejengwa juu ya tofauti za hali na nafasi. Ndiyo maana leo mmoja anasaidiwa na mwenzake, kesho yule aliyesaidiwa naye anakuwa msaada kwa mwingine. Hapo ndipo huruma, msaada, na utu wa mwanadamu huonekana.

Tatu, ni kweli kabisa kuna watu ambao maisha yao yanaonekana kuwa rahisi na kuna wengine wanaobeba mizigo mikubwa sana. Lakini macho ya mwanadamu huona sehemu ndogo tu ya maisha ya mtu. Mara nyingi furaha au huzuni ya mtu haionekani yote kwa nje. Watu wengi wanaonekana kuwa na maisha mazuri lakini ndani wanabeba maumivu yao, na wengine wanaonekana kuteseka lakini ndani wana utulivu ambao wengine hawana.

Mwisho, dunia si mahali pa mwisho wa haki kamili. Ndiyo maana ndani yake kuna tofauti nyingi za maisha. Lakini utukufu wa Mwenyezi Mungu haupimwi kwa tofauti hizo; yeye ndiye Muumba wa maisha, na hekima yake inazidi uelewa wa mwanadamu. Mwanadamu huona kipande cha leo, lakini Mwenyezi Mungu anaona mwanzo na mwisho wa safari ya kila kiumbe.
 
Ngoja ninywe maji kwanza
 
Ngoja nikuongezee maswali mengine ili ufikiri zaidi.

Kama Mungu ni mjuzi wa yote, anajua mwanzo, kati na mwisho:

Je, Alijua mpema kuwa shetani ataasi na kusababisha mateso makubwa lakini akaamua kumuumba hivyohivyo?

Je, hii inamaanisha mateso ni sehemu ya mpango wake?

Je, Alijua kuwa Adam atakula tunda hata kabla hajaanza kuumba kitu chochote?

Je, Anajua alikotokea? Wapi?

Je, Anajua fulani ataenda motoni hata kabla huyo fulani hajazaliwa?

Na kama ana upendo, kwanini alimuumba shetani huku anajua atasababisha mateso makubwa?

Na kama ni wa haki, kwanini asingemuumba shetani kabisa?

Na kwanini atachoma moto watu kwa kosa lake mwenyewe la kumuumba shetani?
 
Hakika umeniongezea maswali zaidi
Inaonekana kila kitu ilikua ni mpango wake

Kwanini atuchome moto🔥
 
Back
Top Bottom