Kweli Mungu hana upendeleo?

Kweli Mungu hana upendeleo?

Ndugu yangu,

Kwanza, uhuru wa kuchagua haujawahi kumaanisha kufanya chochote bila mipaka.
Kila mfumo wa maadili na kila jamii huweka mipaka fulani. Mtu anaweza kuwa na gari lenye uwezo wa kukimbia sana, lakini sheria inaweka kikomo cha mwendo.
->Hapo hatusemi hana uhuru wa kuendesha gari, tunasema uhuru wake unaendana na utaratibu unaolinda ustawi wa wote.

Pili, hoja yako imejikita kwenye uwezo wa mtu binafsi, ana rasilimali, ana nguvu, ana nia.
->Lakini haijaangalia upande wa pili wa jambo, athari kwa wengine na mpangilio wa jamii.
Ndoa si suala la uwezo wa mwanaume peke yake; ni mfumo unaohusisha haki, wajibu, na ustawi wa watu zaidi ya mmoja. Ndiyo maana mifumo ya maadili huweka mipaka ili kulinda usawa na haki.

Tatu, kama tunajadili kwa mantiki ya kweli, lazima tuulize swali la msingi:
Je, uwezo wa kufanya kitu unamaanisha kwamba kitu hicho ni sahihi kimaadili?
Mtu anaweza kuwa na nguvu ya kumdhuru mwingine, anaweza kuwa na fedha za kuwanyonya wengine, au mamlaka ya kuwakandamiza walio dhaifu. Lakini ukweli kwamba ana uwezo huo hauifanyi tabia hiyo kuwa sahihi.

Hapo ndipo tunatambua kwamba maadili hayajengwi juu ya uwezo wa mtu kufanya jambo, bali juu ya kanuni zinazolinda haki, heshima na ustawi wa wote.

Kwa hiyo hoja ya msingi si kwamba mtu analazimishwa kuchagua, bali kwamba uhuru wa mwanadamu unaambatana na uwajibikaji na mipaka ya maadili.
->Bila mipaka hiyo, jamii ingeongozwa na nguvu ya mwenye uwezo zaidi badala ya haki na usawa.

Karibu Mkuu
Maadili ni nini?
Ni nani aliyetunga hizo sheria za maadili?
Na kwanini lazima tuzifuate?
 
Nature is neither immoral nor moral, only pitiless indifferent.
Kama una mzungumzia Mungu wa Utatu Mtakatifu (Trinitarian God) huyo hayupo hivyo hayo yanayosemwa juu yake ni UONGO.

Mateso na Uovu uliopo Dunia ni matokeo ya matendo ya viumbehai.

Mfumo wa Asili hautambui Maadili, kwake hakuna chema wala kibaya. Mfumo upo kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kujiendesha.

Virusi na Bacteria vinategemea viumbe hai kama binadamu kupata chakula na kuzaliana, Virusi na Bacteria hawana lengo la kusababisha maradhi, lengo lao kuu ni Maisha.

Tetemeko la Ardhi ña Majanga mengine ya Asili wakati dunia inapokuwa kwenye harakati za kujiendesha kupitia "plate tectonic movements", matokeo ya majanga hayo yaweza kuwa VIFO vya viumbe, ila kiasili ni faida kwasababu VIFO hivyo vitafanyika kuwa CHAKULA kwa viumbe wengine, matengenezo ya ardhi, matengenezo ya hewa ya oksijeni, nk.

Nature is neither immoral nor moral, only pitiless indifferent.

Kama viumbe wenye UTASHI tunapaswa kutumia AKILI zetu vizuri tulizopewa na Mama-Asili kusahihisha yale yanayosababisha Maumivu, na Kutengeneza yale yanayosababisha Furaha na Amani.

When Science and Reason is Used to its Maximum Potential, the Earth can become unimaginable Heaven.
Hence this is the answer we both don't wanna hear. Mkuu hapo umemaliza Kila kitu
 
Ngoja nikuongezee maswali mengine ili ufikiri zaidi.

Kama Mungu ni mjuzi wa yote, anajua mwanzo, kati na mwisho:

Je, Alijua mpema kuwa shetani ataasi na kusababisha mateso makubwa lakini akaamua kumuumba hivyohivyo?

Je, hii inamaanisha mateso ni sehemu ya mpango wake?

Je, Alijua kuwa Adam atakula tunda hata kabla hajaanza kuumba kitu chochote?

Je, Anajua alikotokea? Wapi?

Je, Anajua fulani ataenda motoni hata kabla huyo fulani hajazaliwa?

Na kama ana upendo, kwanini alimuumba shetani huku anajua atasababisha mateso makubwa?

Na kama ni wa haki, kwanini asingemuumba shetani kabisa?

Na kwanini atachoma moto watu kwa kosa lake mwenyewe la kumuumba shetani?
So what you mean ni kwamba Huyo Mungu hayupo. Kwamba ni dhana ya binadamu kutafuta safety in the midst of majonzi?
 
Biblia inasema Mungu ni upendo, kama ilivyoandikwa katika 1 Yohana 4:8 “Mungu ni upendo.” Pia inaonyesha Mungu anaweza yote katika Mathayo 19:26.

Lakini kama Mungu ni wa upendo na anaweza yote, kwa nini duniani kuna mateso makubwa—watu wanateseka kwa maradhi, umasikini na dhuluma?

Pia maandiko kama Yeremia 1:5 na Zaburi 139:16 yanaonyesha Mungu anamjua mtu kabla hajazaliwa. Je, hii ina maana hata mateso ya watu yalijulikana kabla?

Na kama Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu kama inavyoelezwa katika Yohana 3:16, kwa nini bado kuna mafundisho ya hukumu na adhabu ya milele kama katika Mathayo 25:46?

Ninauliza haya kwa nia ya kutafuta uelewa zaidi wa maandiko. Ningependa kusikia maoni na ufafanuzi wenu.

Wakuu karibuni🙏🙏
me sina maoni ila nachojua baada ya kukaa kutafakri kwa mda mrwfu nikagundndua huenda kwenye Bible zike ni propaganda hazina ukweli wowote we ishi unavoishi hakuna cha jehanamu sijui siku ya kiama sijui nini wala mungu hana upendo
 
Aiseee inafikirisha but tuendelee kujifunza zaidi
 
Ngoja nikuongezee maswali mengine ili ufikiri zaidi.

Kama Mungu ni mjuzi wa yote, anajua mwanzo, kati na mwisho:

Je, Alijua mpema kuwa shetani ataasi na kusababisha mateso makubwa lakini akaamua kumuumba hivyohivyo?

Je, hii inamaanisha mateso ni sehemu ya mpango wake?

Je, Alijua kuwa Adam atakula tunda hata kabla hajaanza kuumba kitu chochote?

Je, Anajua alikotokea? Wapi?

Je, Anajua fulani ataenda motoni hata kabla huyo fulani hajazaliwa?

Na kama ana upendo, kwanini alimuumba shetani huku anajua atasababisha mateso makubwa?

Na kama ni wa haki, kwanini asingemuumba shetani kabisa?

Na kwanini atachoma moto watu kwa kosa lake mwenyewe la kumuumba shetani?
Think Reba Mcentire GIF by ABC Network.gif
 
Back
Top Bottom