Kweli milima haikutani ila binadamu wanakutana

Kweli milima haikutani ila binadamu wanakutana

thomas_360

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
1,456
Reaction score
1,436
Leo katika kukatiza mitaa kurudi home nikiwa natoka job! mara paaah jamaa mmoja mbele kaniita jina langu halafu nilikuwa sina lile wala lile, kuangalia vizur daah sikuamini kabisa nilihisi kama ndoto vile maana ilikuwa ni unexpected event to occur in front of my eyes...

Ni jamaa ambaye nilisoma naye shule ya msingi tena darasa moja lakini alikuja kuhama shule baada ya kufika darasa la 6, baada ya hapo hatukuwahi kukutana tena, mpaka Leo Hii ni zaidi ya miaka 14 tena nimekuja kukutana naye mkoa mwingine kabisa....

HAKIKA LEO NDO NIMEPROVE HUU MSEMO MILIMA HAIKUTANI LAKINI BINADAMU HUKUTANA.....

JE ww hii hali ishawahi kukutokea na ulijisikiaje??

don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
Shost alikuwa anafanya biashara ya vipodozi, alikuwa analetewa Fashion Fair, Iman, Flory Roberts, enzi hizo Marc haijaingia. Wateja wake wakubwa walikuwa wake wa vigogo.

Kuna dada alichukua mzigo wa laki nne, baada ya hapo alipotea na simu alibadili namba. Kumbe mume wake alipandishwa cheo kuwa mkuu wa Idara mkoani huko.

Baada ya miaka mitatu shost ameshasahau habari ya laki nne ingawa zilimuuma. Alialikwa kwenye harusi ya binti wa mdogo wake. Kufika kule yule mdaiwa ndiyo mwenye kiti wa Kamati ya maandalizi.

Mbona alirudi na laki nne shost. Mwenyekiti alikuwa mdogo na harusi aliiyona chungu.
 
daaah!! wazaz wangu walikuwa hawana hata wazo la kunileta duniani Iseee!! kwa huo mwaka
Japo sio haki lakini leo asubuhi nilikuwa nawaza namna ya kuandika humu jf. Je kuna member yeyote humu JF aliyekuwa Kozi ya 1982 pale MATI MLINGANO Agromech?? Njoo tukutane

don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
daaah!! wazaz wangu walikuwa hawana hata wazo la kunileta duniani Iseee!! kwa huo mwaka

don't waste your time on lecturing me, this is 2020
Nikaja mbio nikidhani ati wewe ulikuwa huko miaka hiyo. Hapo ndo tungesema; Kweli milima haikutani
 
Mimi Mara kibao tu. Moja Ni hii ya kupotezana na mtu nikiwahi darasa la sita baada ya mimi kuhama shule na kwenda kukutana nae Chuo Kikuu.
 
Mimi nilisoma na Hassan 'chekechea' si nursery. Nikaja kutana nae nikiwa form two yeye anauza sabuni stendi kuu. Rafiki yangu wa std one nilikutana nae form three nikamtajia majina yake matatu na hakuwa ananikumbuka kabisa, nikataja majina ya rafiki zetu kipindi kile na jina la dada yake. Mwishowe nikamtajia baba yake alivokuwa na gari jekundu ndo akanambia baba yake alikufa na mali zao walidhurumiwa hivo kwa muda huo namuona alikuwa anaishi kwa bibi yake. Alinambia kauli moja kuwa "siku hizi sisi sio matajiri tena".
 
Back
Top Bottom