Kweli maendeleo lakini hii ya Dr Karume ni mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli maendeleo lakini hii ya Dr Karume ni mpya.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 26, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Karume ahutubia kupitia mkanda wa video

  2008-06-25 10:26:48
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar


  Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, jana aliwashangaza wanahabari, baada ya kuwaita kwenye mkutano lakini hakuzungumza nao moja kwa moja na badala yake mkanda wa video uliokuwa umerekodi hotuba yake ndiyo uliofunguliwa ili waisikilize.

  Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu, wapiga picha za magazeti hawakuambulia chochote, huku waandishi wakishindwa kuuliza maswali.

  Waandishi walioshiriki mkutano huo walisema walifika kwenye viwanja vya Ikulu na kusubiri kuingia ndani kwa ajili ya kukutana na Rais Karume lakini wakati huo wakiwa nje Rais alikuwa anaongea na maelezo yake kurekodiwa.

  \"Kutokana na sababu zisizoepukika hamtamuona Rais,\" alisema Msaidizi wa Rais, Bw. Haroub Said na kuwaacha wakiangalia video ya Rais inayoelezea kile alichokuwa amewaitia.

  Katika mkanda huo, Rais alizungumzia ma suala ya umeme Zanzibar, kuwa serikali iko mbioni kununua majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura iwapo kutatokea hitilafu katika gridi ya taifa ya umeme wa Bara.

  Alisema serikali yake imeagiza vipuri kwa ajili ya kukarabati majenereta yaliyoko Unguja ambavyo baadhi ya vipuri vyake vilipelekwa Pemba kutengeneza mashine za kufua umeme zilizoharibika.

  Rais Karume alisema tatizo la umeme litatatuliwa kwa kuwa na ufumbuzi wa kudumu na kwa sasa Marekani kupitia Akaunti ya Changamoto za Milenia (MCC) inaisaidia Zanzibar kutandaza waya mpya wa umeme wa chini ya bahari.

  Akizungumzia kauli za watu waliosema serikali yake haitamaliza tatizo la umeme, aliwaambia waliotoa vijembe hivyo sasa watimize yale waliyotamka.

  ``Kuna watu waliosema kama umeme huu utarudi ndani ya mwezi mmoja watanyoa ndevu zao, tunataka sasa wanyoe kama hawana viwembe tutawapatia,`` alisema katika hotuba yake iliyorekodiwa.
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  he he heeee akutukanaye hakuchagulii tusi, kunakutia akili hapo.
   
 3. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nafikiri amejitahidi sasa angalau anaanza kufikiri kuwa na mitambo ya Umeme wa dharura lakini mukumbushe asilete IPTL au Richmond zanzibar.

  Lakini ya kuwawekea video ilikuwa kali.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Ndiyo jeuri ya ukubwa hiyo!! Ya nini ukutane na waandishi wa habari wakati unaweza kurekodi mkanda na kuwawekea wasikilize? Nao wafanye jeuri ya kutoandika au kutangaza chochote kilichomo ndani ya mkanda huo.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwani alikuwepo hapo Ikulu? labda alikuwa nje ya nchi.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nina wasi wasi alikuwa amekwisha uchapa ulabu au ame over doze ,sababu zisizoweza kuzuilika.
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Hio ni dharau kubwa sana.

  Ni kaazi kweli kweli!
   
 8. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  alikuwa mtoto wa kijiweni saana tena .... kwa mkojo wa firauni humwambii kitu ... sijui kama hawachafulii CCM maana kipindi chake kinayoyoma .... na kila kukicha anazidisha nyodo na kusema hovyo
   
Loading...