Kweli Lowassa alikuwa smart Sana, hii serikali ya awamu ya tano imeanza kuwanyang'anya wananchi Mali zao Kwa ajili michango ya ujenzi wa shule.

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,003
2,000
Hapo vip!!
Leo nimekutana na wananchi wanaotokea wilaya ya Arumeru wakililamika migambo kuvamia katika Nyumba zao na kuchukua Mali, Kwa madai ya kushindwa kulipa michango ya ujenzi wa shule ya shillingi elfu 25.

Nakauli mbiu ya hao Migambo ni kwamba michango lazima, vinginevyo hata kitanda watakiuza.

Anyway, sipingani na mpango Wa kujenga shule lakini kwa serikali hii inayokusanya kodi Sana mbali na kodi kuna vyanzo vingi vya kupata pesa, Kwa nini inawafilisi wananchi wake. ..?

Isitoshe serikali hii imesababisha maisha magumu kwa wananchi, kuanzia katika maeneo ya biashara (hakuna mzunguko wa pesa), hakuna ajira n. K

Leo inamtaka huyu mwananchi aliyekosa ajira, mwananchi ambaye biashara yake imefilisika kutoka na kuyumba Kwa uchumi wa Nchi...alipe mchango tena Kwa lazima.

Hivi Lowassa aliwezaje kujenga shule za Kata pasipo, kuwavamia wananchi na kuwanyang'anya Mali zao..?
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,843
2,000
Yaani serikali inakusanya kodi halafu bado inashindwa kuiletea jamij yake (ambayo ndio walipa kodi )
Halafu inaanza kuwavamia na kuwalazimisha watu watoe michango ya ujenzi wa shule " kodi ambazo huwa wanalipa huwa zinakwenda wapi au ndio zinatumika kujenga ujenzi wa kiwanja cha ndege cha chatle .....

Mambo mengine yana staajabisha Sana ina maana kwamba serikali imekosa watu weledi wa kufikiri ambao wanaweza kutumika katika kutoa maneno mazuri yenye ushawishi na hatimae kuweza kuwafanya wana nchi watoe michango yao wenyewe bila shurti " ......... !? Hii serikali imefilisika Akili haina jipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Gut

Gut

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
2,837
2,000
Hizo kodi halmashauri inakusanya wanapeleka wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom