Kweli hii ni shida!

kwetumasoko

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
866
Reaction score
518
Jamani waungwana

Leo baada ya kutoka kanisani, nimemkaribisha nyumbani dada mmoja ambaye ni rafiki yangu na tunaheshimiana sana, kwa hiyo tumeongozana naye mpaka nyumbani. Nikawatambulisha mgeni aliyetutembelea. Tukapata chakula cha mchana pamoja na familia yangu iliyopo hapo nyumbani, baada ya hapo akatuaga na kuondoka.

Kutokana na wingi wa kazi ofisini kwangu, nikaona ni jambo jema angalau niende nikapunguze baadhi ya kazi.

Naishi na wanangu wawili, wote wa kike hapo nyumbani, mama yao hatupo pamoja nae aliniacha kwa muda mrefu na anaishi mkoa mwingine.

Baada ya kutoka nyumbani, watoto waliongea na mama yao na mara nyingi huwa ana kawaida ya kuwapigia simu siku ya jumapili ambayo huwa wapo nyumbani, sasa kumbe akawa anawadadisi na wamemweleza kuhusu mgeni aliyefika hapo nyumbani.

Niko ofisini, nasikia mlio wa msg inaingia. Kusoma, hakuna cha salam, kaandika "usiwafundishe watoto tabia mbaya, we ma.....ya, huna akili, huwezi leta mwanamke ndani ya nyumba mbele ya watoto, unawajengea tabia mbaya" Nikafikiri sana kwa kweli kaniondolea amani ndani ya moyo wangu kwa siku ya leo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji3] mzazi mwenzio ana point kubwa kusema usiwafundishe watoto tabia mbaya ,

Ila kwa upande mwingine ana kosa, vizur angeanza kukuuliza kwanza.

Nisaidie namba ya mzazi mwenzio nijaribu kumuelekeza[emoji23][emoji23]
 
Nitakupa mkuu
 
Inawezekana bado ana feelings na wewe, kama angekuwa na nia ya kulinda environment ya watoto wake, angeanza, baba A, kuna kitu ningependa tuonge ukipata nafasi. Hii technic aliyotumia ni kama bado anakumiliki na analinda territory yake.
 
Shetani chadema katika ubora wake
 
Inawezekana bado ana feelings na wewe, kama angekuwa na nia ya kulinda environment ya watoto wake, angeanza, baba A, kuna kitu ningependa tuonge ukipata nafasi. Hii technic aliyotumia ni kama bado anakumiliki na analinda territory yake.
Ok, hakuna shida
 
Hajakuacha moyoni kakuacha kimwili huyo!!! Kama vipi muite myajenge
 
Umenikumbusha kisa cha familia moja, mama aliondoka miaka saba, baada ya baba kupata ubunge alirudi na kumfanyia fujo mchumba aliyekuwepo, ilikuwa vita na mwisho mama watoto alishinda.
 
Huyo bado anakuchunga
dawa yake ni kuleta mwanamke aje aishi hapo kabisaa
 
Umenikumbusha kisa cha familia moja, mama aliondoka miaka saba, baada ya baba kupata ubunge alirudi na kumfanyia fujo mchumba aliyekuwepo, ilikuwa vita na mwisho mama watoto alishinda.
Mh! mkuu, nami ni seven years ago
 
Unajua maneno tu yanaweza kukuharibia siku!
mlivoachana kwani mlisema ham,tajihusisha tena na mapenzi? kuachana ni kwamba kila mtu aangalie mtu mwingine wa kuendana nae .wewe unamuogopa nini? au hapo ni kwake?
 
Kwan yeye haingizi wanaume huko alipo?!

Mlete halaf this time to.mba kbs
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…