Kweli Bongo hamna mdada wa hivi hata wajiteteeje

Kweli Bongo hamna mdada wa hivi hata wajiteteeje

mwanaMtata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2014
Posts
2,393
Reaction score
1,433
BAADA YA KUCHUNIANA KWA
MUDA MREFU

MPENZI WA KIKE ANAAMUA
KUMPIGIA MSELA
WAKE SIMU.
Simu inaita kwa mara kwanza hadi
inakatika
bila kupokelewa. Manzi hakati
tamaa, anapiga
tena na baada ya ngrii ngrii kama
sita, jamaa
ndo anapokea simu.
Hata baada ya kupokea, jamaa
haongei neno
hata la HALOO. Manzi inabidi
alianzishe.
MANZI: Hey Frank, mambo.
LI-FRANK: Poa.
MANZI: Mbona hupokei simu
jamani.
LI-FRANK: Hii imejipokea, au?
MANZI: Hee yaishe basi. Mbona
kimya sana
siku hizi.
LI-FRANK: Unataka nimpigie nani
makelele.
MANZI: Mbona unanijibu hîvyo
Frankie.
LI-FRANK: Kukujibuje.
MANZI: Hivyo kifupi na majibu ya
chooni.
LI-FRANK: Unataka nikujibuje sasa
kama jibu la
swali lako ni hilo.
MANZI: Kwa hiyo hilo ndo jibu la
swali langu.
LI-FRANK: Ndo màana yake. Kama
unataka
majibu marefu na yenye maelezo,
nenda
kapime UKIMWI kisha ombea uwe
nao. Hapo
utapata majibu uyatakayo na
maelezo mengi
tu.
Manzi anakaa kimya kama dakika
1 hivi.
Anashusha pumzi ndefu ya
kuchoka au kukata
tamaa tuseme.
MANZI: Hivi Frank nimekukosea
nini?
LI-FRANK: Kunipigia simu.
MANZI: (huku kama anataka kulia)
Jamaniii.
LI-FRANK: Nyo nyo nyooo. Msyuuu.
Manzi anasikika anavuta vikamasi
ila hakati
simu.
LI-FRANK: Unakunywa supu.
MANZI: (Huku akiwa na sauti ya
kilio). Hivi
Frank kweli umebadilika hivi?
LI-FRANK: Kwa hiyo unanitukana.
Nimekuwa
Zombie mimi, au mzimu.
Unanitukana Marry, si
ndio eeh.
MANZI: Hapana si hivyo.
LI-FRANK: Ila.
MANZI: Basi nisamehe.
LI-FRANK: Umepiga simu ili iweje.
MANZI: Leo ni siku yako ya
kuzaliwa Frank.
LI-FRANK: Kwa hiyo.
MANZI: Happy Birthday.
LI-FRANK: Kingine.
MANZI: Nakupenda Frank.
LI-FRANK: Umemaliza?
MANZI: (Akiwa kakata tamaa juu
ya Frank).
Nimekumiss pia, naomba urudi
uwe nami.
LI-FRANK: Umemaliza?
MANZI: Ndio.
LI-FRANK: Haya kata simu.
MANZI: Frank please. Usinifanyie
hivyo jamani.
LI-FRANK: Sibadili neno, kata
simu.
MANZI: Ok. Aaah! Poa, asante
Frank.
Simu inakatwa.
Baada ya dakika kumi, simu ya
Manzi inaita.
Kucheki, ni Frank. Hata sekunde haiishi
inapokelewa.
FRANK: Umekasirika?
MANZI: Hapana, ila nimeumia.
FRANK: Chungulia dirishani.
Manzi ananyanyuka na kufungua
mapazia ya
dirisha laké. Uso kwa uso na
tabasamu la Frank
pale dirishani.
FRANK: Naamini utadumu na mimi
maishani
mwangumwote. Kama umeweza
kuvumilîa haya
madogo, na kuficha hisia zako
kuwa
hujakasirika, naamin utavumilia
na makubwa
na kuficha ya ndani. I miss you
too, Marry. Ni
wewe pekee uliyenitakia siku
yangu ya
kuzaliwa. Ukiwatoa dada na mama
yangu,
wewe ndiye mwanamke pekee
nitakae kuelewa.
Unajua Marry alikuwaje?
Nisikumalizie uhondo.
Jaribu na wewe kufata njia ya LI-
FRANK uone
kama Manzi wako atakuwaje.
TEHE.
Angalizo

Usijaribu hiyo Kibongobongo hata kama unatania utachwa kabisa
 
Huyo dada mvumilivu.....mimi nikipiga simu. Asipopokea nafuta namba afu sitaki mazoeaaaa
 
Muendelezo vip au ndo ile bday and x...?

Mkuu ukitaka kujua mfanyie ivo baby mama wako utajua muendelezo kama mtabaatika kufika uko maana wengi tutaishia kwenye sim kukatwa na mfyonzo wa hatari
 
Ai tn mtu asinijarbu kabisa, maana tungeishia kwenye salamu tu.. Huwa cpend maneno ya karaha masikion mwangu, hvyo km alikuwa ananipima bas nmeshafeli zamn tu
 
Ai tn mtu asinijarbu kabisa, maana tungeishia kwenye salamu tu.. Huwa cpend maneno ya karaha masikion mwangu, hvyo km alikuwa ananipima bas nmeshafeli zamn tu

Kwanza ungebeep usingepiga lol
 
I had a girl ni mvumilivu like that...mbaya zaidi mchaga....but mm sikuwa nafanya makusudi,ni vile yeye uelewa wake ulikua mdogo tu...kitu mnaweza kiongea fresh leo au muda kidogo ulopita,baadae akakianzisha upya akihitaji maelezo yaleyale ulompa mwanzo...honestly I found that job tiresome kwa kweli...
Mbaya zaidi akute mambo hayako poa mzigoni itakua balaa....yaani li-frank litupu.
Ila Kuna mwaswali mengine ni ya kipumbafu sana,eti why hupokei simu wakati nimepokea???

Anyway naomba msamaha kwa yeyote who'll be offended na hii comment.
 
Lol hao watu ni waajabu sana hawaelewegi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom