tinna cute
JF-Expert Member
- Sep 22, 2013
- 4,630
- 2,317
unalaani kama nani,ucpanic bibie mwenye kulaani ni yule Aliye2umba!tena yeye ka2kumbusha 2waheshimu wazazi!...wewe unaleta ujenda wako hp,kwan mzaz ni mama2?baba sio mzazi ee!.Futa hyo kauli ndg
Nimesikitishwa sana hadi nimetoa machozi kwa hiki kilichokuwa kinaendelea kwenye uzi wa Wanawake wanajiuza.
Wanaume mnataka nini? Mmekosa hata staha kwa hao wachache mnaowajali mkabaki mnashabikia haya. Najua watakuwepo wa rika mbali mbali na mmeonyesha ushirikiano mzuri kweli. Mmeona mnayowafanyia humo vyumbani haitoshi mpaka mje kuanika u.p.u.m.b.a.f.u wenu hapa.
Haikutosha kutoa fedheha hizi kwenye vijiwe vyenu ambavyo sisi hatupo mkatuhabarisha na kutuweka katika madaraja.
Kuna mwanamke anakuwepo kwenye vikao vya kupanga mahari?
Kuna mwanamke anapenda yaliyomkuta yeye yamkute na bintiye?
Kuna kahaba anayefundisha mwanae wa kike kazi?
Ni wanawake wangapi wanalea watoto bila baba zao?
Wanajiuza ehh?
Mnatutukana nyumbani, vijiweni na humu pia.
Mnaendelea kushirikiana kudhalilisha utu wa wanawake.
Eti wanawake wanajiuza!
Si ni nyie kwa u.m.a.l.a.y.a wenu mnaoenda mnatafuta mabikra wachanga na kuwahadaa na vijimali vyenu, leo hawawezi sahau siku waliyotoa utu wao kwa wanaume waliodhani wanaheshimu. Mnasimama kusema wanajiuza.
Si ni nyie mmewazalisha wake zenu,mkisisitiza watoto waitwe kwa majina yenu hamjali familia zenu mnaondoka mnapeleka pesa kwa makahaba wawafanyie mnayotaka. Leo mnasema wanawake wanajiuza.
Si ni nyie mnaozalisha mabinti wa watu kwa hila za ahadi za ndoa halafu mnatelekeza watoto, mnadai siyo wife material. Kabla alikuwa malkia huyu, leo anajiuza.
Si ni nyie mnaita wake zenu m.a.l.a.y.a na pengine kuwapiga ngumi mkijificha kwenye sura ya kichwa cha familia halafu baadaye mkiwaletea watoto wa matunda ya ufuska wenu mkitaka wawalee, leo mnasema wanajiuza.
Si ni nyie mlio maofisini na vyuoni mnawajaribu wanawake waliobahatika kusoma mkitaka mlale nao ndo mwape stahili yao. Hao nao hujiuza!
Si ni nyie mnaogongana na watoto wenu mkishindana kuwatumia mahousegirl kama vyombo vya kujistarehesha bila gharama. Hii ni part time ehh?
Si ni nyie mnawabaka watoto wadogo pengine watoto wa ndugu zenu bila haya wakipata mimba mnawalazimisha kutoa mimba wangali vigoli. Wanajiuza hawa ehh?
Si ni nyie mnasema mnapenda huduma ya kikahaba na kuwalazimisha pengine wake wenu kushiriki mkiwatumia kinyume cha maumbile kukidhi haja zenu, eti akulidhishe kimapenzi. Hawa wameliwa kwa kujiuza,eeeh!
Si ni nyie mnaowafuata watoto wanaolingana na watoto wenu mnabebwa kwenye vifua vya watoto hawa bila aibu. Wanajiuza?
Si ni nyie mnawalaghai mabinti wanapiga picha za ngono. Picha hizo sura za mabinti hawa tu zinaonekana za kwenu huwa mnaficha. Malipo ya kujiuza hayo ehh?
Si ni nyie kwa tamaa zenu mnabaka hadi viumbe vingine ili mridhishe hamu zenu. Hapa bei sokoni iko juu ehh?
Si ni nyie mnaokaa vijiweni kutathimini ya nani tamu ipi hajaguswa mnawekeana dau kumpata bikra. Mpango wa kupata bidhaa adimu ehh?
Jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Kama wazazi mmetuita m.a.l.a.y.a tungali wadogo wakati hatujui mtu mme, tumeshuhudia mkiwanyanyasa mama zetu kwa tabia zenu mbaya huku mkitaka wawape heshima tumekua katika jamii ambayo mwanamke si mtu ni bidhaa, wengine mmewachagulia maisha mkiwanyima hata elimu achilia kina sie tusiojua sura za baba zetu. Mnataka nini?
Naandika haya baada ya moyo wangu kushindwa kuvumilia kuendelea kutukanwa namna hii. Nakataa udhalilishwaji huu.
Ole wenu! Ole wenu! Ole wenu mnaojipa moyo kuwa wanawake wanajiuza na kuendelea kuwafanyia maovu.
.
Mbona unaangalia upande mmoja wa Tshiling?
Na nyie mnavyokuwa na bwana zaid ya mmoja tuwaitaje? Kuwa Malay.a sio mpaka ujiuze..
Mnavyobambikia wanaume watoto? Tuwaitaje..
Afterall kuombwa tigo hujashikiwa bunduki ni kutokuwa na msimamo ndio yanayowakuta.
Wapo hadi w/wake wanaokaa vijiweni such as Saloon na kupiga umbea ya flani kibamia, haujui kazi mara yule m/ume suruali.
Kupigwa picha ya uchi na kukubali ni kuwa na akili yako finyu, kwann usimwambie na mimi nataka picha yako ya uchi?
Tunapenda huduma yenu ya kikahaba kwakuwa mnaenda kujiuza, sitisheni hiyo biashara ya kuuza utu tuone m/ume ataenda kufanya nini. Kisingizio eti maisha magumi mpaka unauza utu wakati kuchoma vitumbua unaona aibu.
Tunawaacha na kuwaita sio"Wife Material" kutokana na tabia zenu mlizonazo such as Tamaa kuwa m/ume zaidi ya mmoja, kiburi n.k
Kikubwa mbadilike na nyie mnaojiona wanawake wa kisasa mbona hamjiulizi miaka ya nyuma hamkuitwa Malay.a na kwanini sasa hivi ndio mnaitwa hivyo.
Majaribu2013 aje hapa awaombe radhi dada/mama/watoto na shangazi zetu. Binafsi sikufurahishwa na yaliyoandikwa katika ile habari!
ngoja niondoke hapa.. hivi kumbe na huyu mwanangu atakuja kunitukana siku moja??,hiv kumbe kuzaliwa mwanamke ni kuwa malaya,
kweli Jf ni home of Great thinkers
Wanaume wenyewe malioo kibao wengine wameoa kumbe nyuma ya panzia mashoga,wakipata wanawake wenye kipato wanakua nae kwa c kwamapenz bali apate tu pesa bila kujali hisia za mwanamke na still wanatudharau eti tunajiuza, kama unaona hatuna mapenzi ya kweli acha kujishughulisha na mapenzi.
hata mwanaume mwenye wanawake zaidi ya mmoja ni malay.. ila siwezi kukaa chini na kusema all men are dogs..Kama una mabwana wengi we ni Malay.a tu hata uwe nani. Ndio mana mna kauli mbiu yenu Baba wa Mtoto anamjua mama tu.
hata mwanaume mwenye wanawake zaidi ya mmoja ni malay.. ila siwezi kukaa chini na kusema all men are dogs..
na kusema ati mtu akikataa jambo ndo limemgusa uko soooooo wrong ndugu yangu,kama ulisoma psychology hata kidogo tu utaelewa sio lazima jambo likukute ndio likuumize na kama uko hivyo wewe ni selfish wa kutupwa..kwani ukikuta mtoto katupwa jalalani utasema sio wangu so it doesnt hurt?au hujawahi ona watu wanamvisha kichaa nguo sababu tu it hurts seeing another human being in that state?
Usifanye experience yako iwe ndo pie kwenye maisha ya watu,.ndio maana kuna maneno like kama,baadhi, etc kwasababu tu maisha yako sio maisha ya mwingine.
Kama unahitaji mtu au baadhi ya watu wabadilike,show them the cause and effect(positive and negative|)sio ushadadizi
ndo yamefika huku.......kazi kweli kweli
Nimefurahi kwakuwa hujaingia kwenye huu mkenge. Janja sana wewe kama Habby.
Majaribu2013 aje hapa awaombe radhi dada/mama/watoto na shangazi zetu. Binafsi sikufurahishwa na yaliyoandikwa katika ile habari!
majaribu 2013...
Kuna sababu yoyote inakufanya uwafikirie wanawake kwenye hali hasi kiasi hicho, au lengo lako ni kurekebisha baadhi ya dada/mama/shangazi na watoto wetu?
.>>> Tunajua wapo ila hawawauzii wanawake wenzao, wanatuuzia sisi kwa hiyo tujiangalie pia. Pia kuwasema hao walioolewa, wenye waume zao kuwa wanajiuza? Kwani wahudumiwe na nani?
Kama wewe ni mkristo naomba usome kitabu cha mwanzo, wakati Mungu anaamlaani Adam baada ya kuanguka dhambini,. HAKIKA KWA JASHO LAKO UTAKULA, NA MIIBA ITAKUCHOMA(sijaichukua kama ilivyo ), na mwanamke alilaaniwa vipi, KWA UCHUNGU UTAZAA! sasa wewe ungependa mwanamke ndo akupe na kukutafutia chakula?
Kutafuta rizki ni jukumu la mwanaume, mwanamke anabaki kuwa msaidizi.... hapa nazungumzia mume na mke, hao wanaojiuza huko buguruni mimi sina la kuchangia.
Hivi kuna jambo gani linaendelea hapa...
simo na sihitaji kuwemo..huu muda si bora nije Facebook pub tujipatie moja moto moja baridi