CCM ni ile ile siku zote. Magufuli ni CCM iliyochangamka hata ukiangalia matendo yake
1. Alifuta ajira za walimu na madaktari
2. Kulikuwa hakuna kufuata sheria hapa ndipo Sabaya na Makonda waliibuka. Ukimsifia Mwendake na kuuponda upinzani unapewa teuzi.
3. Watu wasiojulikana walikuwa wengi sana
4. Kufukuza kazi ilikuwa kawaida sana. Unaweza ukachelewa kwenye mkutano, ukafukuzwa kazi au kufungwa jela
5. Uchaguzi ulikuwa wa ovyo sana. Huyu bwana haliharibu uchaguzi kbsa.
Kipindi cha Magu umeme na maji uhakika ila amekufa imekuwa vyanzo vya maji.
Usitegemee jipya kwa CCM. Ni sawa na mwanamke uliyemfumania ukamsamehe mkarudiana. Siku ukimfumania tena usishangae