Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Walishindwa kumuita kamati kuu na kumuhoji kwa tuhuma wanazozizungumza. In fact hakuna usaliti ila ni hombwe LA uongozi. Taarifa kamili anazo Mzee wao mtei. Yeye ndiye amtaki kumsikia kabisa Zitto. Kwa Mimi ambaye napenda ccm iachie Dora sifurahishi na siasa za cdm. Kafulila walimfukuza hivihivi, kama hasingejiunga na nccr ESCROW tungeijuaje!?
 
Act wazalendo ndicho chama kinachokuja kuwa imara na uimara wake umeanza onekana ni baada tu limbu kushindwa operation yake
 
Pamoja na maxuri yote uliyosema na kujiuliza ila usisahau kuwa LIMBU NDIYE ALIKUWA MPINI WA CDM KUMUUA ZITO na bahat mbay ameshindwa hivyo hawana njia nyingine zaid ya kuendeleza tuhuma hewa na chuki za kipuuz kama SIFA za chama chao ZILIVYO
Kuthibitisha hilo eti eti eti na yeye kagombes ubunge mwanzs kupitia chama kilichomtuma kumuua xito(CDM) Maskini Limbuuuu....Mboweeer...Slaaaa...
Lisuuuuu....AIBIKENI NA CHAGADEMA YENUU
Ulikuwa na hoja nzuri ila matumizi ya X yamenifanya nikudharau.
 
Tatizo uongo wewe unageuza JF ni platform ya kumtukana Zitto safi sana Mods hizi nyuzi za uongo uongo dawa ni kuziunganisha tu.

Ukweli huishi milele,wakati uwongo
huwa unakufa.Hivyo haina haja ya kufuta kitu kilichoandikwa,kwa maana Km ni kweli basi Ukweli utadhihirika lah km si kweli basi uongo utadhihirika pia.
 
Last edited by a moderator:
Hivi eti huyo ni afisa wa CDM anatweet kitu kama hicho na misukule inaamini kua hata kama ni kweli ZZK anatumika ni wajinga kiasi gani ifikie hadi kuwakilisha CCM tuache majungu Vijana Chapeni kazi.ZZK ni nani hadi kila akifanya yake mnapagawa? Huo muda si mngewambia vijana namna ya kujikomboa.Mtoi ni kilaza sana na hii inaonyesha makao makuu ya CDM ilivyokumbatia vilaza natamani sana wachukue nchi tuone hao vilaza watapewa nafasi gani.
Acheni siasa maji taka wakati huu ni Lala Salama.

Hata km ni muda wa kuchapa kazi haina maana mambo mabaya yanayofanyika ili kudhoofishana kwamba yasisemwe.
 
Dah kweli, huyu jamaa msaliti sana. Mtu mbaya kweli kweli kwenye mageuzi ya nchi hii, Simshangai lakini watu wa kigoma ndivyo walivyo. Amemfukuza limbu, akabadili jina la chama, akabadili katiba, ndani ya siku sita akajipa cheo cha uungu wa chama, au nuru kama anavyoita yeye. Inawezekana kweli siku sita tu ndani ya chama unapata cheo kikubwa kuliko wote? Ajabu pia ni mpinzani gani anaondolewa bungeni, wabunge wa ccm wanalia machozi na kuomboleza? Ni mpinzani huyo au mwenzao? Hivi kweli tundu lissu leo afukuzwe bungeni, wabunge wa ccm watalia kwa ajili yake na kuomboleza? Ukipata jibu hilo, utajua zitto ni nani..

Wengi hawamuelewi wala kumsoma yule jamaa,lengo lake yule jamaa ni kuua Upinzani Completely.
 
Yan zitto atawaacha hoi halaf yey anazid kufyeka mapori na octoba mtabak midomo kuchacha na kuvunda maana hamtakuwa na la kusema tena. Kwan lissu alianzia chagadema? Sialikuwa nccr? Kwahyo na yey ni msaliti wa nccr?
 
Zitto Zuberi Kabwe amekuwa akishambuliwa mara kwa mara kwa tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikirudiwa rudiwa bila ushahidi.Amekuwa akiitwa msaliti lakini bila ushahidi dhahiri.Pamoja na kufukuzwa ndani ya Chadema na kujiunga na ACT ambayo ni haki yake kikatiba lakini bado mashambulizi yanaendelea.
MASWALI YA KUJIULIZA;
1.Je, ana athari gani katika siasa?
2.Je, ni kweli ni tuhuma za usaliti tu ndizo zinazofanya aendelee kushambuliwa?
3.Je, ni hofu ya kushika nguvu ya upinzani?
4.Je, ni uwezo alionao katika kujenga hoja?
5.Je, kama hana madhara katika siasa za upinzani kwa nini anashambuliwa kwa tuhuma zisizothibitishwa?

Hivi unahitaji ushahidi gani cdm watoe ili uamini kwamba muha ni saliti!?
Nimesema hapo juu katika uzi wangu kuwa zito akane zile namba za simu zilizokuwa zinaonesha miamala ya kuhamisha pesa za usaliti.
Aikane ile account ya benk iliyofunguliwa German.
 
Kuna hoja zimetolewa kwenye bandiko hili zina mantiki sana.

1. Zitto keshafukuzwa na chama chake cha zamani ni kwa nini asiachiwe andeleze siasa kwenye chama chake Kipya?

2. Kwa nini CUF hawashughuliki na usaliti wa Hamad Rashid kama CHADEMA wanavyofanya kwa Zitto?

3. Baadhi ya tuhumu zilizoletwa na TAWA kama ile ya mwanamke Mjerumani ilishawahi kukanushwa kwa barua ya Mnyika baada ya Mwanamke (?) huyo kupitia wakili wake kutaka maelezo kutoka CHADEMA kuhusu waraka uliokuwa umesambazwa kwenye mitandao kwamba alihusika kwenye mlungula huo wa Zitto, Mnyika kwa niaba ya CHADEMA alikanusha chama kuhusika na waraka huo. Kimantiki kama kiongozi wa chama anaukana waraka maana yake uhalali wake hupotea.
 
- Sijawahi ona kokote siasa inakofanywa mwanachama wa chama kimoja kwa wakati huohuo ni mwanzilishi wa chama kingine cha siasa, sijawahi.

- Sijawahi kuona mtu anajiunga na chama fulani baada ya siku tano anapewa uongozi mkuu wa chama hicho, sijawahi

- Sijawahi kuona popote siasa inapofanywa, mwenyekiti wa chama yupo chini ya mtu fulani. Yahani kikatiba kabisa kuna mtu yupo juu ya mwenyekiti, hii pia sijawahi kuona.

- Sijawahi kuona popote pale chama cha upinzani kukipinga chama cha upinzani na si chama tawala. AGAINST CHADEMA TANZANIA(ACT). Kwa maneno au hata vitendo. Chama kinafanya sherehe kikipata wafuasi wa upinzani kuliko wa chama tawala.

- Sijawahi kuona chama cha upinzani kinafadhiliwa na chama tawala kiuchumi na kimikakati. Tumefanya uzinduzi wa chama chako Zuberi kwa gharama kubwa sana, air time ITV, chakula, ukumbi expensive, na mbwembwe nyingi. Lakini mbona hujawahi kuchangisha pesa toka kwa wanachama wako? Kama kuna mtu anachangia ni nani huyo? Mtamlipaje baadae?

- Sijawahi ona chama cha upinzani popote pale siasa inapofanywa, wafuasi wake ni wale wanachama na wafuasi wa chama tawala. Le mutuz, laki si pesa, musa alani n.k, hii nayo sijawahi ona.

Kwa yote hayo juu Zuberi kwa nini nisikuite kwamba wewe ni msaliti halisi wa demokrasia hapa nchini. Kama kweli wewe siyo msaliti mbona hujawahi kujitokeza na kukataa zile namba za simu walizozitoa chama chako cha zamani kuwa zilitumika katika ufisadi? Mbona sijasikia kuikana ile akaunti ya benki wa yule dada kule ujerumani?

UKINIJIBU HAYO KWA UFASHA WEWE KWELI SI MSALITI.

Wewe hufuatilii mambo cjui unapewa tu umbea unakuja kuutapika hapa. Suala la hujawahi kuona mtu zaidi ya mwenyekiti wa chama nakushauri ufuatilie siasa za kenya. Nchi ambayo si Tanzania wala uganda au nchi yeyote ile inayoweza kujisifu kwa ukuaji wa demokrasia zaidi ya nchi hiyo. Suala la kuhamia kwenye chama na kupewa uongozi sijui unataka kiongozi awe na muda gani ndani ya chama. Lakini kabla ya kuandika hivyo ungejiuliza hichi chama kina umri gani? Kama utasema kiongozi awe amekaa ndani ya chama kwa miaka kadhaa kama vyama vya zamani, kuna mambo mawili. Hujieleewi au unajitoa ufahamu kwa ushabiki wa kisiasa. Na moja kwa moja wenye uelewa tunajua wewe ni Bavicha. Suala la Ujerumani na pesa mnazosema ni akili huna za ufuatiliaji.Zitto ameliongelea swala hilo karibu kwenye kila interview. Aliwaambia alipoiona hiyo taarifa alimwandikia barua babu slaa kama hizo ni tuhuma za chama ili ajitetee. Anasema babu slaa hajawahi kuijibu barua hiyo. Vilevile yule dada wa Ujerumani nae alikiandikia chama barua akidai maelezo. Yeye alijibiwa kwamba sio taarifa cha chama. Zitto akaamua kuchukua hatua ikiwa ni Pamoja na kuripoti polisi. Baada ya kuona wahusika wa uandaaji wa skendo hiyo wanaanza kukamatwa chama kikadai eti ni taarifa kutoka usalama wa taifa. Mwenye akili unajiuliza. Waliomtumia hizo pesa inadaiwa ni Ccm. Chama kilichopo madarakani. Usalama wa taifa uko chini ya serikali hiyo hiyo. Sasa iweje wavujishe habari hizo. Sasa mengine fuatlia. Akili za kuambiwa changanya na zako. Kama hujafanya utafiti acha kukurupuka kupost. Sio lazima upost. ...Lakini jitambue alafu ujikomboe.....
 
Umekuwa muongomuongo na kinyonga. Mara useme hili;mara ukane lile.Umekuwa mwanasiasa mwigizaji kwelikweli.Kigoma uliaga Ubunge mara mbilimbili. Kiko wapi? CHADEMA uliapa kuwa wa mwisho kutoka. Kiko wapi? Kwani umepatwa na nini? Umebadilika Zitto!

Nasubiri Bunge livunjwe ili niwaone Wabunge 50 wa UKAWA watakohamia ACT-Wazalendo kama ulivyojinadi. Isipokuwa kweli,nitajiunga na wasiokuamini na kukuona msaliti. Juzijuzi hapa umewaita watanzania Mwembeyanga uwatajie waficha mabilioni Uswisi.Nikaona kurejea kwa Dr. Slaa wa Mwembeyanga aliyetaja mafisadi 11 wa Tanzania. Pamoja na mbwembwe zote kwenye vyombo vya habari na magari ya matangazo,hukutaja.Ukagawa bahasha yenye majina ya wahindi!

Uko wapi uthubutu wako? Uko wapi ushujaa wako wa Buzwagi? Yuko wapi Zitto? Sijui umekuwaje. Lakini,chunga sana usije ukawa tapeli!

Mzee Tupatupa (kwasasa Dodoma)
 
zitto saa hii anacheza sankororo wala hana habari , nyie bado amewaganda ktk vichwa vyenu kama vya kuku
 
Back
Top Bottom