Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Wana JF,
Kwa elimu aliyonayo na mambo anayoyafanya hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.

Tangu alipochaguliwa awe M/Kiti wa PAC hapo ndipo nilijua mwisho wa siasa za Uadilifu kwa ZZK umewadia.

uZito amekuwa mjanja mjanja tu anaanzisha jambo hutaona ukamilifu na mwisho wa dhamira ya kweli,Mfano:-Suala la walioweka fedha nje ya Nchi Uswisi,Zito Kabwe alilimaliza suala hili kiaina tu kwa mtindo wa kujipatia Umaarufu tu na sio kumaliza kiini cha tatizo.

Ametumika kuvunja nguvu za CHADEMA NA UPINZANI,kwa ujumla mpaka sasa hilo nalo hajafanikiwa.

ZITO ni bilionea amezitoa hizo fedha wapi???
Tukisema ni fisadi mnatoa macho kaa mchusi kabanywa na mlango.

Uadilifu wa Zito ni Sifuri tena yenye masikio.
Ni mpenda Madaraka sana na yuko tayari apokee fedha za Aibu na kuwatelekeza wenzake.

ZITO SIO MPAMBANAJI WA KWELI,
Anatumika kufifisha na kuua Demokrasia ya Vyama vingi Nchini.

Kwa hili ZITO ZUBERI KABWE anatia aibu sana,ni bora tu angejiunga na CCM hio ingetufanya tujue yeye sio mpinzani,kuliko sasa kubadilibadili rangi kaa Kinyonga hakufai na haitamsadia lolote.

WATANZANIA TUNA AKILI TIMAMU HATUDAGANYIKI.
SASA TUMEKUJUA JINSI ULIVYO,
POLE SANA.

Nawasilisha kwenu!!!

mkuu una chuki mpaka unatia aibu! sasa hapo zitto kaathirika nini??

pia ukianzisha thread au kumjadili zitto maana yake anakutawala !

best way to deal na watu usiowapenda ni ku wa ignore usipofanya hivyo...huyo mtu anakutawala, naona wengi sana mnavyoweweseka

na kwenye SIASA MTAJI NI KUWA KWENYE HEADLINE....KWA UZURI AU UBAYA...NDIO SIASA!

unachofanya ni kumpaisha kwa sababu mwisho wa siku

UNAYEMCHUKIA WEWE, MWENZAKO ANAMPENDA

Pole
 
Tena mtu kama huyu ni wa kumwogopa kama ukoma.Hata TLP sie hatukubaliani na tabia ya huyu kijana.Amekuwa ndumilakuwili.
 
Ni wazi kwamba sasa Zitto Kabwe amechanganyikiwa! Baada ya kutimuliwa Chadema kutokana na usaliti, Zitto amejiunga na ACT, chama alichokiasisi tangu akiwa ndani ya Chadema (usaliti!). Hivi sasa anatafuta namna ya kujenga umaarufu kupitia chama hiki kidogo cha siasa kwa kuzusha mambo mengi ya uongo, kama alivyofanya akiwa Mwenyekiti wa PAC na kulidanganya taifa zima kuhusu Tegeta Escrow Account.

Zitto amethubutu tena kuwadanganya Watanzania kuwa mradi mkubwa wa Mwambani Economic Corridor unaosimamiwa na wazalendo wa nchi hii eti ni ufisadi! Huku akijua au kwa ujinga wake tu, anadanganya kuwa mradi huo unafanywa kwa ubia kati ya serikali na Kampuni ya James Rugemalira. (Soma toleo la leo tarehe 13 Aprili la Tanzania Daima kupata majibu aliyopewa na mwanasheria Cuthbert Tenga)

Mtu huyu Zitto amejenga chuki dhidi ya Rugemalira baada ya kuumbuliwa kuwa alilidandanya taifa katika ripoti yake ya Escrow kama ilivyobainishwa na mtafiti mmoja aitwaye Salim Khatri. Zitto sasa anatafuta pa kujishikilia ili aweze kurejesha umaarufu wake wa kisiasa ulioporomoka vibaya, na yupo tayari kutumia uwongo ili kufanikisha azma yake.

Sasa tunamfahamu vizuri zaidi Zitto Kabwe, mtu aliyetumiwa na Nimrod Mkono kuzusha kile alichokiita kashfa ya Escrow kwa maslahi ya benki ya kigeni ya Standard Chartered. Tunakamilisha uchunguzi kuhusu kiasi cha pesa alicholipwa na Mkono na Standard Chartered kisha kila kitu kitakuwa hadharani na Watanzania wamjue vizuri zaidi mtu huyu anayejinadi kuwa mzalendo.

Zitto ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.
 
zito nae kadakia mada hii habari ilishakuja hapa jf mda kama wa wiki kadhaa kama kuna mtu anayo anaweza kuileta tena ...sio habari mpya na member waliijadili sana sasa zito asije akaichukua ili impe umaarufu
 
Mleta mada maelezo yako ni ya kusadikika na una maswali kadhaa ya kujibu:
1.Amelidanganya taifa kupitia kamati yake ya PAC,amelidanganyaje taifa? hebu toa vigezo reliable.
Note: Tanzanians are not the same anymore,usidhani watu watamchukia Zitto kwa kuwa wewe tu kwa maslahi yako binafsi umeamua kumchukia.
2.Ametumiwa na Nimrod Mkono,how? tuwekee maelezo wazi,Mi naweza sema tu na wewe unatumiwa na Rugemalila unakubali? kama hukubali kwa nini?
3.You dont sound like Chadema guy lakini naona unajaribu kum-tight Zitto na ishu yake ya Chadema ili upate support ya wanachadema ambao katika upade wa escrow wako Pamoja nae sasa sijui mtajigawa vp ili mumshambulie kwa pamoja mtajua wenyewe.
4.Tunataka uje na matokeo ya uchunguzi unaoufanya please,sio kwamba tunamtetea Zitto hapana akibainika ni fisadi nae atakuwa kwenye moto wa mafisadi tu lakini tunataka aje mtu a-prove kwamba ni fisadi sio kusema tu Zitto fisadi.
 
Zitto na kamati yake walitoa mapendedkezo ya kutaifisha mitambo ya umeme huku wakijua kwamba katika karne hii utaifishaji hauendani na sheria na mazingira ya biashara ya karne ya ishirini na moja. Nadhani ana chiki biafsi na James Rugemarila
 
zito nae kadakia mada hii habari ilishakuja hapa jf mda kama wa wiki kadhaa kama kuna mtu anayo anaweza kuileta tena ...sio habari mpya na member waliijadili sana sasa zito asije akaichukua ili impe umaarufu

Ovyoo kbisa acha husuda je hata kma kaichukua huoni kwamba anasaidia ijulikane mbn akina mnyika hawajaisemea na walikuwa kusini wanafungua kanda mtakufa kwa vihoro mwaka huu shame on u
 
Kwa kuwa ukileta chochote kinachomponda Zitto hapa JF unapata uungwaji mkono kumtukana basi kila mwenye makohozi yake anayamwaga jamvini.

Huu mswada wa makosa ya mtandao ukitiwa saini Jukwaa la siasa linazikwa rasmi maana uzushi uzushi tu hakuna hata uthibitisho.
 
ni wazi kwamba sasa zitto kabwe amechanganyikiwa! Baada ya kutimuliwa chadema kutokana na usaliti, zitto amejiunga na act, chama alichokiasisi tangu akiwa ndani ya chadema (usaliti!). Hivi sasa anatafuta namna ya kujenga umaarufu kupitia chama hiki kidogo cha siasa kwa kuzusha mambo mengi ya uongo, kama alivyofanya akiwa mwenyekiti wa pac na kulidanganya taifa zima kuhusu tegeta escrow account.
Zitto amethubutu tena kuwadanganya watanzania kuwa mradi mkubwa wa mwambani economic corridor unaosimamiwa na wazalendo wa nchi hii eti ni ufisadi! Huku akijua au kwa ujinga wake tu, anadanganya kuwa mradi huo unafanywa kwa ubia kati ya serikali na kampuni ya james rugemalira. (soma toleo la leo tarehe 13 aprili la tanzania daima kupata majibu aliyopewa na mwanasheria cuthbert tenga)
mtu huyu zitto amejenga chuki dhidi ya rugemalira baada ya kuumbuliwa kuwa alilidandanya taifa katika ripoti yake ya escrow kama ilivyobainishwa na mtafiti mmoja aitwaye salim khatri. Zitto sasa anatafuta pa kujishikilia ili aweze kurejesha umaarufu wake wa kisiasa ulioporomoka vibaya, na yupo tayari kutumia uwongo ili kufanikisha azma yake.
Sasa tunamfahamu vizuri zaidi zitto kabwe, mtu aliyetumiwa na nimrod mkono kuzusha kile alichokiita kashfa ya escrow kwa maslahi ya benki ya kigeni ya standard chartered. Tunakamilisha uchunguzi kuhusu kiasi cha pesa alicholipwa na mkono na standard chartered kisha kila kitu kitakuwa hadharani na watanzania wamjue vizuri zaidi mtu huyu anayejinadi kuwa mzalendo. Zitto ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.

shame n u bibiyako angebaki ardhi
 
10011236_903211636366201_6175244748885457022_n.jpg
 
zito nae kadakia mada hii habari ilishakuja hapa jf mda kama wa wiki kadhaa kama kuna mtu anayo anaweza kuileta tena ...sio habari mpya na member waliijadili sana sasa zito asije akaichukua ili impe umaarufu

Ilijadiliwa JF na ikaishia hapa hapa watanzania waliowengi walikuwa hawajui chochote sasa zitto ameichukua anautangazia umma ufisadi mwengine mkubwa unaofanyika sasa yeye kosa lake nini hapo?
 
Zitto kadanganya mno Taifa na Bunge letu tuuuuu
1.Fedha zile sio za serikali na imeonekana wazi na Mh Rais kusema wazi swala la element ya kodi TRA wanashughurikia.
2.STD Chartered Bank hawajawahi kukopesha bali matapeli mid man kutaka kununua Deni lakini hawakufanikiwa baada ya mfilisi kuahirisha na wabia kuuza vema hisa zao.
3 mkono advocate ana chuki kukosa tenda za kuiwakilisha Tanesco katika k kesi feki
Mh Prof Mhongo kumshtukia wakamtumia Zitto
5.Mengine mengi.yaja zitto kwishney
 
Wana-JF.,
Mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba Zitto ni msaliti wa mabadiliko nchini kwasababu anatumika kuifanya CCM iendelee kuwa madarakani. Nashawishika kuamini kwamba CHADEMA walichelewa sana kuachana na mtu huyu hatari wa mabadiliko nchini. Naomba niwakumbushe tu kwamba, siyo Zitto tu anayetumiwa na CCM, lkn hata Prof. Kitila Mkumbo. Nashawishika kuamini kwamba kuna watu ambao wako ndani ya ACT-Wazalendo kama Mwigamba wakidhani wapo kwa ajili ya demokrasia lkn hawajui nini hasa malengo ya kuanzishwa kwa ACT. Hili naamini hata mwenyekiti Anna pamoja na viongozi wengine na wanachama asilimia kubwa wa ACT hawajui kilicho nyuma ya pazia.

Kwa ufupi ni kwamba ACT ni chama chenye mkono wa CCM ili kupambana na Upinzani hasa CHADEMA na UKAWA hapa nchini ili CCM iendelee kuwa madarakani. Wote mnatambua iliyokuwa nafasi ya Kitila Mkumbo kabala ya kufukuzwa CHADEMA. Lkn, pamoja na Kitila kujihusisha na Siasa akiwa mfanyakazi UDSM, tena chini ya Prof. Mukandala ambaye ni mshahuri wa Rais katika mabo ya kisiasa, bado Kitila Mkumbo aliendelea na kazi yake pale UDSM na alipandishwa cheo hadi kuwa Dean wa School mojawapo pale DUCE. Hili tu kwa mtu mwenye kufikiri linatosha kukupa picha kwamba ni kwanini wengine waliachishwa kazi lkn Mkumbo yeye alizidi kupandishwa vyeo??

Jambo lingine ni kauli ya Zitto hasa alipotembelea Mwananchi wiki iliyopita. Zitto alisema kwamba alishiriki kuanzisha ACT. Sasa jiulize, ni lini ACT ilianzishwa na kupata usajili wa kudumu na lini Zitto aliondolewa CHADEMA? Je, wale wanaojifanya vipofu na kusema CHADEMA ilimuonea Zitto mbona hata hawajiulizi swali kwamba, je, ni chama gani cha siasa kinachoweza kumvumilia msaliti anayeanzisha chama huku bado ana uanachama wa chama kingine achilia mbali nafasi za uongozi?

Jambo lingine la kushangaza ni kwamba, Zitto amesema hadharani kwamba mbunge yeyote atakayetaka kwenda bungeni kutokea mkoa wa Kigoma ni lazima agombee kupitia ACT, kwani atakayeshindwa kufanya hivyo basi asahau ubunge. Sababu kuu Zitto alisema, ACT ina mikakati ya kuwa na chanzo katika MKoa wa Kigoma. Hili nalo neno, hasa inapotolewa na mtu kama Zitto aliyekuwa akilalamika kwamba CHADEMA ni ya wachaga kwasababu tu Mwenyekiti wake ni Mchaga. Sasa swali hapa ni kwanini ACT iwe na kitovu Kigoma? au kwasababu Kiongozi wake mkuu ni Muha????? nini sasa ulichokuwa unakipigia kelele ukiwa CHADEMA? Swali lingine ni hili, hivi Zitto ana hati miliki ya Mkoa Kigoma na watu wake hadi yeye ndiyo awe na uamuzi wa nani aende Bungeni? hivi wale wabunge wa mkoa Kigoma na watu wa Kigoma hawana nguvu kiasi kwamba wanatii kila kitu kutoka kwa Zitto? Baada ya Zitto kutoa hiyo kauli nilibakinajiuliza swali 1, je, Kitila na Mwigamba nao walikuwa na taarifa toka mwanzo kwamba ACT inatakiwa kuwa na kitovu Kigoma? au hili nalo limewashangaza kama ilivyotushangaza wengi.

Jambo lingine la usaliti wa Zitto dhidi ya mabadiliko nchini ni yanayoendelea humu JF kutoka kwa wafuasi wa ACT na Zitto kuhusu CHADEMA. Kila siku hawa watu wanaanzisha thread za KIPUUZI dhidi ya CHADEMA. Naziita za KIPUUZI, kwani hazina mantiki na zinapoteza hadhi ya JF. Hawa watu wana uelewa na exposure mdogo sana kuhusu mabao ya kisiasa na hata kijamii. Zitto alisema alishawaelekeza nini cha kufanya na hasa kutopambana na vyama vya Upinzani, lkn yanayotokea hapa JF kila mtu ni shahidi. Kila siku kuna thread kuanzia 5 za kipuuzi dhidi ya upinzani zinaanzishwa na wafuasi wa ACT. Sasa kauli ya Zitto iko wapi????

Narudia tena, Zitto Zuberi Kabwe, ni Msaliti na mwenye tamaa mbaya sana ya madaraka pamoja na pesa. Na kwa wafuasi wa ACT, kama mnadhani mko kwenye meli 1 na Zitto na Mkumbo, basi mnapoteza muda wenu. Hawa wawili (Zitto na Mkumbo) wanawatumia tu ili kuendelea kufanya kazi ya mtawala. Kazi iliyowashinda wakiwa ndani, na sasa wanatafuta namna ya kuendelea kuifanya.

Ni mimi tu kukuletea ukweli.
JATELO.
 
Back
Top Bottom