Wana-JF.,
Mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba Zitto ni msaliti wa mabadiliko nchini kwasababu anatumika kuifanya CCM iendelee kuwa madarakani. Nashawishika kuamini kwamba CHADEMA walichelewa sana kuachana na mtu huyu hatari wa mabadiliko nchini. Naomba niwakumbushe tu kwamba, siyo Zitto tu anayetumiwa na CCM, lkn hata Prof. Kitila Mkumbo. Nashawishika kuamini kwamba kuna watu ambao wako ndani ya ACT-Wazalendo kama Mwigamba wakidhani wapo kwa ajili ya demokrasia lkn hawajui nini hasa malengo ya kuanzishwa kwa ACT. Hili naamini hata mwenyekiti Anna pamoja na viongozi wengine na wanachama asilimia kubwa wa ACT hawajui kilicho nyuma ya pazia.
Kwa ufupi ni kwamba ACT ni chama chenye mkono wa CCM ili kupambana na Upinzani hasa CHADEMA na UKAWA hapa nchini ili CCM iendelee kuwa madarakani. Wote mnatambua iliyokuwa nafasi ya Kitila Mkumbo kabala ya kufukuzwa CHADEMA. Lkn, pamoja na Kitila kujihusisha na Siasa akiwa mfanyakazi UDSM, tena chini ya Prof. Mukandala ambaye ni mshahuri wa Rais katika mabo ya kisiasa, bado Kitila Mkumbo aliendelea na kazi yake pale UDSM na alipandishwa cheo hadi kuwa Dean wa School mojawapo pale DUCE. Hili tu kwa mtu mwenye kufikiri linatosha kukupa picha kwamba ni kwanini wengine waliachishwa kazi lkn Mkumbo yeye alizidi kupandishwa vyeo??
Jambo lingine ni kauli ya Zitto hasa alipotembelea Mwananchi wiki iliyopita. Zitto alisema kwamba alishiriki kuanzisha ACT. Sasa jiulize, ni lini ACT ilianzishwa na kupata usajili wa kudumu na lini Zitto aliondolewa CHADEMA? Je, wale wanaojifanya vipofu na kusema CHADEMA ilimuonea Zitto mbona hata hawajiulizi swali kwamba, je, ni chama gani cha siasa kinachoweza kumvumilia msaliti anayeanzisha chama huku bado ana uanachama wa chama kingine achilia mbali nafasi za uongozi?
Jambo lingine la kushangaza ni kwamba, Zitto amesema hadharani kwamba mbunge yeyote atakayetaka kwenda bungeni kutokea mkoa wa Kigoma ni lazima agombee kupitia ACT, kwani atakayeshindwa kufanya hivyo basi asahau ubunge. Sababu kuu Zitto alisema, ACT ina mikakati ya kuwa na chanzo katika MKoa wa Kigoma. Hili nalo neno, hasa inapotolewa na mtu kama Zitto aliyekuwa akilalamika kwamba CHADEMA ni ya wachaga kwasababu tu Mwenyekiti wake ni Mchaga. Sasa swali hapa ni kwanini ACT iwe na kitovu Kigoma? au kwasababu Kiongozi wake mkuu ni Muha????? nini sasa ulichokuwa unakipigia kelele ukiwa CHADEMA? Swali lingine ni hili, hivi Zitto ana hati miliki ya Mkoa Kigoma na watu wake hadi yeye ndiyo awe na uamuzi wa nani aende Bungeni? hivi wale wabunge wa mkoa Kigoma na watu wa Kigoma hawana nguvu kiasi kwamba wanatii kila kitu kutoka kwa Zitto? Baada ya Zitto kutoa hiyo kauli nilibakinajiuliza swali 1, je, Kitila na Mwigamba nao walikuwa na taarifa toka mwanzo kwamba ACT inatakiwa kuwa na kitovu Kigoma? au hili nalo limewashangaza kama ilivyotushangaza wengi.
Jambo lingine la usaliti wa Zitto dhidi ya mabadiliko nchini ni yanayoendelea humu JF kutoka kwa wafuasi wa ACT na Zitto kuhusu CHADEMA. Kila siku hawa watu wanaanzisha thread za KIPUUZI dhidi ya CHADEMA. Naziita za KIPUUZI, kwani hazina mantiki na zinapoteza hadhi ya JF. Hawa watu wana uelewa na exposure mdogo sana kuhusu mabao ya kisiasa na hata kijamii. Zitto alisema alishawaelekeza nini cha kufanya na hasa kutopambana na vyama vya Upinzani, lkn yanayotokea hapa JF kila mtu ni shahidi. Kila siku kuna thread kuanzia 5 za kipuuzi dhidi ya upinzani zinaanzishwa na wafuasi wa ACT. Sasa kauli ya Zitto iko wapi????
Narudia tena, Zitto Zuberi Kabwe, ni Msaliti na mwenye tamaa mbaya sana ya madaraka pamoja na pesa. Na kwa wafuasi wa ACT, kama mnadhani mko kwenye meli 1 na Zitto na Mkumbo, basi mnapoteza muda wenu. Hawa wawili (Zitto na Mkumbo) wanawatumia tu ili kuendelea kufanya kazi ya mtawala. Kazi iliyowashinda wakiwa ndani, na sasa wanatafuta namna ya kuendelea kuifanya.
Ni mimi tu kukuletea ukweli.
JATELO.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Utabiri kinzani na mchanganyiko:
NAVAA VIATU VYA "SHEIKH YAHYA" KWA MUDA.!
Apumzike kwa amani huko alipo mnajimu mkuu, ustaadh, mtaalamu wa nyota na anga za mbali, bingwa wa kusoma alama za nyakati, mtaalamu wa kuita na kufukuza majini marehemu Sheikh Yahya Hussein. Miaka kadhaa baada ya kifo chake leo naomba kurithi kazi yake japo kwa dadika chache.
Nimesoma interview ya leo ya ZZK na gazeti la JamboLeo ameeleza juu ya umakini wa usalama wa taifa. Amesema wanaopuuza usalama wa taifa ni watu ambao hawafikiri vizuri.
Kauli hii ya ZZK imenifanya nijaribu kuunganisha dots na hivyo kuweza kufanya utabiri wangu vzr.
Dot ya kwanza. Siku chache zilizopita maafisa wa juu wa Usalama wa taifa waliripotiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Ndg.Edward Lowassa na kuwa wanamuunga mkono kwny mbio zake za Urais. Usalama wanaodaiwa kumuunga mkono Lowassa ndio haohao ZZK anawasifia leo kuwa wako makini.
Dot ya pili. ZZK wakati anafukuzwa CHADEMA alisema ipo siku atakuwa kiongozi mkubwa nchini na eti chadema watamheshimu kwa hilo.
Dot ya tatu. Fedha nyingi na nguvu kubwa inayotumika kukitangaza chama cha ACT inatoka wapi?
UTABIRI.!
Mpango wa ZZK kuanzisha chama cha ACT wakati akiwa bado mwanachama wa CHADEMA ni mpango ulioratibiwa vizuri na usalama wa taifa wanaomuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa.
Lowassa is very strategic person. Anajua kuwa hawezi kupitishwa na CCM kugombea Urais. So ametafuta chama mbadala. Chama ambacho kitamfanya ashinde kirahisi.
Lowassa anajua kuwa akijiunga CHADEMA hatapokelewa na hata akipokelewa hawezi kupewa nafasi ya kugombea Urais. So ndoto yake itakuwa imekufa. Sasa afanyeje ili agombee nje ya CCM na kushinda?
Mbinu aliyotumia ni kuanzisha chama ambacho kitapata support CCM na upinzani. Na chama hicho ni ACT.
Alichofanya Lowassa ni kutafuta mtu mwenye ushawishi ndani ya CHADEMA ambaye akiondoka anaweza kuhama na wafuasi wengi. Na mtu huyo ni ZZK.
So ZZK kazi yake kubwa ni kuibomoa CHADEMA. Aondoke na wafuasi wengi wa CHADEMA kwa kadri iwezekanavyo. Ndio maana hadi sasa hatujasikia mtu kutoka TLP, UDP au PPT Maendeleo, kajiunga na ACT. Wengi tunaowasikia wametoka CHADEMA. Hiyo ndiyo kazi aliyopewa ZZK. Kuibomoa CHADEMA.!
Na wapo wabunge kadhaa wa CHADEMA watakaojiunga na ACT baada ya bunge kuvunjwa (baadhi majina tunayo). Wamehofia kujiunga sasa hivi kwa sababu watapoteza "kiinua mgongo" chao kama ilivyokua kwa Fredy Mpendazoe mwaka 2010. So baada ya bunge kuvunjwa mwezi July kuna utitiri wa wabunge wa CHADEMA watajiunga ACT.
Baada ya hapo Lowassa mwenyewe atajiunga ACT akifuatwa na mamia ya wabunge wa CCM na mawaziri lukuki. Wapo wafuasi na viongozi wa vyama vingine vya upinzani ambao nao watajuinga ACT. Kufikia hapo ACT kitakuwa chama tishio kwa CCM na upinzani maana kina wafuasi kutoka chama tawala na upinzani.
Wakati CCM na CHADEMA wakiwa kwenye taharuki ya mpasuko kwenye vyama vyao, ACT watatumia fursa hiyo kujinasibu na kujitafutia uhalali kwa wananchi. Ushawishi wa Lowassa na ZZK utawafanya watu wengi wajiunge na ACT kutokea CCM na Upinzani hasa CHADEMA.
Wakati wa uchaguzi ACT itapata kura nyingi kutoka kwa waliokua supporters wa CHADEMA na waliokua supporters wa CCM na vyama vingine vya upinzani. So ACT itapunguza kura za CCM na za CHADEMA kisha watachanganya pamoja na kudeclare ushindi.
Baada ya hapo Edward Lowassa atatangazwa Rais kupitia ACT na ndipo atamteua ZZK kuwa Waziri mkuu. Na hapo ndipo litakapotimia lile neno la ZZK kuwa "ipo siku nitakuwa kiongozi mkubwa nchini na CHADEMA wataniheshimu"
Mkakati huu unadaiwa kupangwa kwa ustadi mkubwa na Usalama wa taifa ndio maana ZZK amediriki kusema "wanaobeza usalama wa taifa hawajui kazi yake".
‪#‎MWISHO WA UTABIRI‬.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Copy and paste...👆👆