Kwanini Zitto Kabwe hakufahamu kama CHADEMA ina mwenyewe?

Kwanini Zitto Kabwe hakufahamu kama CHADEMA ina mwenyewe?

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
Wakati akihojiwa na gazeti la Mtanzania, Zitto kabwe pamoja na mambo mengine, ameonyesha kama hakufahamu kuwa CHADEMA ina mwenyewe na kwa msingi huo, aliingia CHADEMA bila kufahamu mlango wa kutokea na sasa anahangaika kutafuta mlango wa kutokea wakati wenye CHADEMA wameisha mfukuza.

Siwezi kusema Zitto Kabwe ni mjinga lakini ninaweza kusema, upumbavu wake ulimfanya kudhani kama yeye pia ni mmliki wa CHADEMA na kwa msingi huo, alitoa nguvu na akili yake yote itumike ndani ya CHADEMA akidhani anachokifanya ni sehemu ya maisha yake wakati wenye mradi wakimtazama kama mjinga asiyetambua anachokifanya.

Kwa upumbavu wake, hata pale walipomwambia kutogusa vitu na viti fulani vya CHADEMA kwa sababu vimewekwa maalum ili wakae na kuvitumia wenye CHADEMA, hakutaka kusikia na kuacha kuvigusa.

Freeman Mbowe amekaliliwa kwenye kikao cha ndani ya CHADEMA akisema,

''Sasa mtu akisema tuna mgogoro na Zitto Kabwe, magazeti yanaandika, kwa hiyo tukae na Zitto tuongee naye, Tuongee naye nini?. Usaliti ndani ya chama hiki hatuuvumilii kwa gharama yoyote. Period.

Usaliti ni treason, wewe uko na wenzako hapa tunajipanga namna ya kukamata dola, mnalala usiku na mchana, mnamkuta mwenzenu asubuhi anatoka na kwenda usalama wa taifa kupeleka information zenu. Halafu unaniambia tuongee kuhusu Zitto.

Zitto anaunda chama yuko ndani ya chama. Tumvumilie tu, Kamanda tafadhari eeh.

Hatuna chuki na mtu binafsi lakini nawaambieni hatuta entertain ujinga huo, this is the war.

Mtu yoyote anayefanya kazi ya kutuuza na siyo Zitto tu. Wako wengine wengi tukiwakamata. Yule jamaa pale alisema sijui lakini mimi sijasema''.


Zitto kwa upande wake anajitetea baada ya kuulizwa swali hili na mwandishi wa gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha habari kinachosema,''Zitto: Kipengele kilichotumika kunifukuza Chadema kilitungwa kwa ajili yangu''.
Swali: Baada ya Mahakama kutoa uamuzi wake na Mwansheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu kutangaza kuwa umefukuzwa uanachama kwa kuwa kukishitaki chama ni kujifukuza katika chama moja kwa moja, tangu ukiwa kiongozi wa chama uliwahi kukitilia shaka kifungu hicho kwa kuwa hivi sasa umeonekana kukilalamikia.

Jibu: Hiki kifungu kipo kwenye kanuni na wala siyo Katiba, kilitungwa mwaka 2013. Mwaka huo kuna mabadiliko fulani fulani yalifanywa. Mabadiliko yale yalikuwa na malengo fulanifulani ikiwamo kulenga watu fulanifulani.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, mamlaka ya kutoa haki iko kwenye chombo kimoja tu nacho ni Mahakama, kila raia ana haki ya kwenda mahakamani kudai haki, unaposema mwananchama wa Chadema akienda mahakamni amejivua uanachama ina maana wewe huitambui Katiba ya Jamuhuri.

Hii ina maana kama mwanachama amekipangisha chama, na chama kikashindwa kulipa kodi, yule mwanachama akienda mahakamani amejivua mwenyewe uanachama kwa kuwa haruhusiwi kwenda mahakamani.

Hicho ni kipengele ambacho hakikupaswa kuwap, Wanachama wa Chadema waende mahakamani kushtaki kipengele hicho ili kitangazwe kuwa siyo halali.
Chama kinachopambana kushika dola hakipaswi kuwa na vipengele kama hivi. Ila yote kwa yote hiki kipengele kimewekwa mwaka 2013 na mwaka 2015 kikatumika kwangu, ni wazi kilitungwa kwa ajili yangu.

Swali: Baada ya kufukuzwa Chadema, ni nini hatma yako kisiasa?

Jibu: Nina ziara ya kuzunguka na wananchi wa jimbo langu kuangalia jinsi ya kuwatumikia, leo (jana) nawaaga rasmi kwamba sintakuwa nao baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, lakini ni nini kinachokuja baadaye ya hapo tutakijua vizuri wiki ijayo (wiki hii).
Hatujajua kama Chadema wameandika barua kwa Spika ili kunitangaza kuwa jimbo liko wazi, kama ndivyo tutakaa kujua ni nini cha kufanya.
Ilipaswa baada ya kesi kwisha taratibu zifuatwe, mpaka sasa sijapata taarifa zozote za kufukuzwa ndiyo maana nasema mpaka wiki kesho iishe tutajua, nitakuwa na nia ya kuendelea kutumikia kwenye jimbo lolote Oktoba.

Swali: Una mpango wa kujiunga na ACT?

Jibu: Tusijaribu kuvuka mto kabla hatujafika pa kuvukia.
 
Mkuu unahangaika sana na ZItto kabwe... Komaa na chama chako ya wengine wachie wenyewe
 
Mkuu unahangaika sana na ZItto kabwe... Komaa na chama chako ya wengine wachie wenyewe
Ndugu,
Umeisoma mada yangu yote na kuielewa?

CCM kwa sasa haihitaji mtu ili kuikomaza kwa sababu imeishavuka kiwango cha kukomazwa.
 
Endelea kujipaka wanja kwenye mdogo.


swissme
 
Hata ccm ina wenyewe,mguse chenge na mzee wa manvi uone cheche
 
Mbona ccm wenyewe ni wakina chenge lowasa
Tibaijuka a.k.a milioni kumi hela yamboga. Chadema wenyewe ni wananchi.
cA
 
Hata ccm ina wenyewe,mguse chenge na mzee wa manvi uone cheche
Ndugu;
Majibu utayapata hapa,
Habari yenyewe ni hii,
Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi imewasimamisha Andrew Chenge, William Ngeleja na Prof Anna Tibaijuka ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa, NEC.

Chenge, Ngeleja na Prof Anna Tibaijuka wanahojiwa tume ya maadili kufuatia tuhuma za kupokea hongo kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira.

Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi inakutana mjini Dodoma kujadili mambo mbalimbali ikiwamo hatma ya wanachama sita walioanza kampeni za urais kabla ya muda ndani ya chama hicho
Mzee wa manvi ndiyo nani?

Nieleweshe.
 
yes, ccm ina wenyewe lakini chadema ina mwenyewe.

Nadhani unaelewa tofauti ya maneno hayo ndiyo maana wanaccm tunasema kila siku, ccm ina wenyewe na wenyewe ni sisi.

act haina mwenye nayo ni ya umma...! Jokes make mtakavoporomoka kama mafuriko....
 
Hiki sio chama bali ni kitega uchumi cha MTEI na wanaukoo wake wote,nia yao ni kukamata Dola tu ili wajibinafsishe migodi yote na visima vote vya gesi,wananchi amkeni,angalia Mbowe alivyoongea,yeye anawaza kukamata Dola tu,sijasikia hata neno moja linalomgusa mtanzania,utleast hata angesema watanzania wana hali mbaya halafu mtu analeta usaliti?,ila yote aliyoongea ni ubinafsi tu.Watanzania amkeni hiki chama hakina nia ya kuwakomboa wananchi.
 
Ndugu,
Umeisoma mada yangu yote na kuielewa?

CCM kwa sasa haihitaji mtu ili kuikomaza kwa sababu imeishavuka kiwango cha kukomazwa.
umesoma post yangu lakini?? sijazungumzia ccm kukomaa, nimesema wewe ukomae na chama chako
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Komredi MwanaDiwani tatizo kubwa la Zitto alihisi hatonyanyasika kwa wahafidhina wa Chadema kwa vile alivyojituma na kukipigania chama chao.Aliaminishwa kuwa atalipwa kwa mema yake.
 
Last edited by a moderator:
Zitto bado haamini kwa kilichomtokea Chadema kwa kuwa alikipenda sana chama.Ndio sawa na kukataliwa na mwanamke unaempenda.
 
Last edited by a moderator:
Hiki sio chama bali ni kitega uchumi cha MTEI na wanaukoo wake wote,nia yao ni kukamata Dola tu ili wajibinafsishe migodi yote na visima vote vya gesi,wananchi amkeni,angalia Mbowe alivyoongea,yeye anawaza kukamata Dola tu,sijasikia hata neno moja linalomgusa mtanzania,utleast hata angesema watanzania wana hali mbaya halafu mtu analeta usaliti?,ila yote aliyoongea ni ubinafsi tu.Watanzania amkeni hiki chama hakina nia ya kuwakomboa wananchi.
Eti anajiandaa kuchukua dola. Hivi huyu Mbowe anafahamu hata maana ya dola?

Mbowe anajipanga kuchukua dola inayotumia wana usalama wa taifa zaidi ya 20 kupanga mbinu ya kumuua Dkt. Slaa!

Anyway, Wonders never cease!
 
Back
Top Bottom