Kwanini Zitto Kabwe hakufahamu kama CHADEMA ina mwenyewe?

Kwanini Zitto Kabwe hakufahamu kama CHADEMA ina mwenyewe?

Hiki sio chama bali ni kitega uchumi cha MTEI na wanaukoo wake wote,nia yao ni kukamata Dola tu ili wajibinafsishe migodi yote na visima vote vya gesi,wananchi amkeni,angalia Mbowe alivyoongea,yeye anawaza kukamata Dola tu,sijasikia hata neno moja linalomgusa mtanzania,utleast hata angesema watanzania wana hali mbaya halafu mtu analeta usaliti?,ila yote aliyoongea ni ubinafsi tu.Watanzania amkeni hiki chama hakina nia ya kuwakomboa wananchi.

Hizi zote ni shida za kukariri madesa ya vyuoni. Aongelee watanzania kwenye maada ambayo haihusu hicho kitu, jamani, hivi mmesoma wapi wabongo wenzangu? Kila kitu kina mahala pake na utaratibu wa kukiongelea. Huwezi kwenda kuzindua nyumba ya kulala wageni, afu mwisho wa siku ukaongelea matatizo ya wafanyabiashara sokoni. Utakuwa na matatizo ya ubongo. Jitahidini kufikiri kabla ya kuandika jamani.
 
Komredi MwanaDiwani tatizo kubwa la Zitto alihisi hatonyanyasika kwa wahafidhina wa Chadema kwa vile alivyojituma na kukipigania chama chao.Aliaminishwa kuwa atalipwa kwa mema yake.
Comrade Mingoi,
Kwa hiyo una maana Zitto Kabwe ametapeliwa?

Ndiyo maana ninapatwa na wasiwasi na fikra za Zitto katika msingi wa mafunuo.
 
Waraka wa kumngo'a zitto kabwe ImageUploadedByJamiiForums1426524350.612212.jpg
 
umesoma post yangu lakini?? sijazungumzia ccm kukomaa, nimesema wewe ukomae na chama chako
Ndugu,
Nimekujibu hivyo kwa sababu mimi ni mwanaCCM.

Kwani wewe ulidhani chama changu ni kipi?
 
Na wewe uko chini ya nape au lowassa? Unalipwa sh. Ngapi?? Au ndio ww uliempiga mzee wetu warioba??
Ndugu,
Mimi niko chini ya CCM.

Unaniuliza malipo ili yakusaidie nini katika kujenga hoja?

Kwani wewe unalipwa Tsh. Ngapi?

By the way, Kwani Nape na Lowassa wako chini ya nani?
 
Yes, CCM ina wenyewe lakini CHADEMA ina mwenyewe.

Nadhani unaelewa tofauti ya maneno hayo ndiyo maana wanaCCM tunasema kila siku, CCM ina wenyewe na wenyewe ni sisi.
MWANADIWANI,
heshima kuu kwako.
Unanichanganya mno na naomba angalau uelewe kuwa kuna watu makini wanofauatilana maandiko yako wakiamini wewe ni mtu makini,mimi ni mmoja wao!
Kwa nini unaingia katika cheap politics wakati unaonekana ni mtu mkubwa na mwenye mamalaka ndani ya CCM?
Hivi alivofukuzwa Mansour Himid tafsiri yake ni kuwa CCM ina wenyewe?Kwa nini unajitoa fahamu.
Ni kampeni ngapi ambazo ZZK alishiriki katika kukijenga chama?
ZZK alishaonekana kwa kitambo kuwa anajiamini yuko juu ya chama,ni intelligent,influetial kiasi ambacho hata kushiriki na wenzie anaona tabu.
Katiba inaeleza ya kuwa ukishapeleka shauri mahamakani hukumu yake ni xyz,sasa la ajabu lipi?
 
Ndugu,
Nimekujibu hivyo kwa sababu mimi ni mwanaCCM.

Kwani wewe ulidhani chama changu ni kipi?
kumbe hujaelewa, nilimaanisha ukomae na chama (CCM) haya ya wengine waachie wenyewe, wewe ukaja na jibu la kwamba ccm imekomaa - mie nilifocus kwako kama mwanadiwani, but you shifted focus to ccm instead
 
Hizi zote ni shida za kukariri madesa ya vyuoni. Aongelee watanzania kwenye maada ambayo haihusu hicho kitu, jamani, hivi mmesoma wapi wabongo wenzangu? Kila kitu kina mahala pake na utaratibu wa kukiongelea. Huwezi kwenda kuzindua nyumba ya kulala wageni, afu mwisho wa siku ukaongelea matatizo ya wafanyabiashara sokoni. Utakuwa na matatizo ya ubongo. Jitahidini kufikiri kabla ya kuandika jamani.
Alitakiwa awaweke watanzania kwanza,alitakiwa aonyeshe jinsi anavyoumia mtu kukisaliti chama ni kuwasaliti Watanzania,yeye yeye kajiweka mbele kabla ya watanzania kasema kuwa Anajiandaa kukamata dola halafu Zitto anamsaliti,wewe akili yako imeshidwa kung'amua kuwa MBowe anachotaka ni kukamata nchi tu na wala sio kutatua matatizo ya watanzania
 
Zitto bado haamini kwa kilichomtokea Chadema kwa kuwa alikipenda sana chama.Ndio sawa na kukataliwa na mwanamke unaempenda.

Zitto ndio mwanachama pekee ambae hakuwahi kuwa chama kingine, lema alikuwa tlp, mbowe alikuwa ccm, slaa alikuwa ccm, mgonjwa wa akili tundu.lisu nae alikuwa ccm
 
Last edited by a moderator:
Hiki chama lazima kife
Lazima kife,namkumbuka sana Wangwe,huyu Mbowe anajifanya yeye yupo juu ya kila kitu,mtu akitaka kugombea uenyekiti tu anaitwa msaliti,anzia Kabouru,Wangwe na sasa Zitto.Hata huyu Tundu Lissu siku akionyesha nia ya kugombea uenyekiti na yeye ataitwa msaliti
 
Alitakiwa awaweke watanzania kwanza,alitakiwa aonyeshe jinsi anavyoumia mtu kukisaliti chama ni kuwasaliti Watanzania,yeye yeye kajiweka mbele kabla ya watanzania kasema kuwa Anajiandaa kukamata dola halafu Zitto anamsaliti,wewe akili yako imeshidwa kung'amua kuwa MBowe anachotaka ni kukamata nchi tu na wala sio kutatua matatizo ya watanzania

Mbowe anampiga fitina dr. Slaa ili agombee urais october, Slaa hana chake atabaki mshauri wa chama
 
Lazima kife,namkumbuka sana Wangwe,huyu Mbowe anajifanya yeye yupo juu ya kila kitu,mtu akitaka kugombea uenyekiti tu anaitwa msaliti,anzia Kabouru,Wangwe na sasa Zitto.Hata huyu Tundu Lissu siku akionyesha nia ya kugombea uenyekiti na yeye ataitwa msaliti

Tundu.lisu ametulizwa baada ya dada yake kuzawadiwa ubunge wa viti maalum ndio maana anamnyenyekea sana Mbowe
 
Mbowe anampiga fitina dr. Slaa ili agombee urais october, Slaa hana chake atabaki mshauri wa chama
Anaona kuwa dalili zinaonyesha kuwa upinzani unaweza kushinda,hawa UKAWA /CHADEMA lazima wafarakane kabla ya uchaguzi,yaani hawa kila mtu anautaka urais.
 
Huyu anaitwa mwanadiwani sijui kama huwa anatumia akili leo hii labda hajui uwezo wa watanzania kuchanganua mambo umekuwa mkubwa hivyo hawamezi chochote wanachoambiwa. Zitto anajua fitina na hujuma alizokuwa anafanya chadema sasa anatafuta huruma ya watanzania ohhooo sikujua kama chadema ina mwenyewe basi huyu si kiongozi anayefahaa kwenye jamii maana anaweza kuingia hata sehemu ambayo ana uhakika nayo. Akipewa nafasi ya juu si atasaini mikataba mibovu aje atuambie alikuwa hawajui wawekezaji. Huyu anatofauti gani na mkulu aliyesema hajui kwa nini tz ni maskini si unaona anayoyafanya ina maana nae aliingia kwenye urais akiwa hajui kwenye urais kuna nini. Type za kina zitto wako wengi wanataka madaraka kesho wakiaribu utasikia hata nilikuwa sijui nani mwenye taasisi. Zitto kilichokuua unakijua ni UNAFIKI basi haya mengine unatafuta huruma kwa umma ambao wengi kwa sasa wanakufahamu unafiki wako kwenye rushwa nyingi humo wakati huo huo tena wewe ni mpiga vita rushwa zamani ilikuwa raisi kuwadanganya wananchi leo anayefikiri atadumu kwa njia hiyo anajidanganya mwenyewe. Zitto ukweli anaujua na wengi tunaujua hivyo kujisemesha vijimaneno anapoteza muda bure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom