Kwanini zamani Dagaa wakipikwa wanaondolewa vichwa ila Siku hizi hapana.

Mi mkazi wa mwanza. Enzi za kukata vicha dagaa bei ilikuwa sh hamsini. Sasa ni miatano. Hebu fikiria ukiwakata kichwa ni kama unabakiza 1/3. Sasa hapo si wanakuwa mameisha.

Na pia improvement za mapish nazo zimesaidia
 
Kwa sababu ya Mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Ndo maana zamani dada zetu mlikua mnavaa underskirt na machupi kama kaptula ila sikuhizi ni mwendo wa Bikini na nyuzi tu kiunoni.
 
Mambo yanabadilika sana kwanini zamani kabla ya kupika dagaa walikua wanakatwa vichwa ila siku hizi hawaondolewi vile vichwa na bado wanakua watamu tu

Nini lengo la kuondoa vile vichwa?
ukiondoa vichwa utapunguza mboga usawa wenyewe huu wa magu.!
 
Ndo maana watu wanaoishi DSM wana akili za dagaa
Huku mikoani tunatoa vichwa
 
Zamani dagaa walikuwa wanaanikwa chini kwenye mchanga hivyo hupelekea dagaa wale kuwa na mchanga mwingi kichwan hivyo Wakati wa kupika inabidi uviondoe vile vichwa kwa sababu ya mchanga
Ila kwa sasa wanaanikwa juu kwenye vichanja hivyo si rahisi dagaa kuwa na michanga na ndio maana kwa sasa wanapikwa bila kutoa vichwa
 
Jibu lako lina ukweli mwingi sana.
 
Back
Top Bottom