sijulikani
Member
- May 15, 2014
- 52
- 89
Zamani kulikuwa na msemoa baba au mama ni baraka. Ukihusiana na baba au mama yako au ndugu zako ni baraka.
Lakini ukweli nilioutathmini katika maisha ni tofauti. Utakubaliana na mimi kwamba watu ambao wameendesha maisha yao huku wakiwa karibu sana na wazazi wao maisha yamewapiga na wengi wao hawajafaulu.
Wamejikita katika umasikini wa kutupwa. Hata kama si umasikini hawafiki kiwango cha maisha mazuri tunayoyaita "kutoboa".
Kinyume chake ni kwamba wale ambao ama waligombana na wazazi na wakaachana nao, au waligombana na ndugu kisha wakaachana nao, ndiyo wengi wamefaulu maisha. Wanakula vizuri, wanasomesha watoto wao vizuri, wanasafiri kwa magari yao vizuri na mambo kama hayo.
Hebu tutafakari na tujadili kwa undani tatizo hili, maana kuna tiatizo zito kwenye jamii yetu tunalificha kw apropoganda potofu. Bahati nzuri ni tatizo linamkuta kila mmoja wetu.
Huenda wazazi wetu na ndugu zetu asili yao ni ukorofi. Nahisi ukorofi wao usingekuwa tatizo kama jamii ingekuwa haiwaungi mkono wanapoonekana wamekorofisha. Lakini jamii nayo inajidanganya kuwaunga mkono na ndiyo maana mtu anapoamua kuwatupilia mbali wazazi na ndugu anajikuta maendeleo yake yanapanda wakati yule aliyebaki anawakumbatia anaishia kuporomoka kimaisha.
Mimi nadhani anaporomoka kimaisha kwa sababu aliishia kufurahisha jamii na kutozingatia ukwlei kwamba ndugu na wazazi ni wakorofi na wadumazaji wa maendeleo.
Naomba tujadili hili, naamini ni kansa iliyoko kwenye jamii inaogopa kujadiliwa.