Nebart Chalaji
Senior Member
- Feb 15, 2013
- 143
- 192
Kilimo kimekuwa kikinadiwa na kupigiwa upatu na wahamasishaji wa aina mbalimbali hususani wale wanaosisitiza kulima kibiashara na kuwapa watu matumaini bila kuwadokeza vitu mhimu ambayo vitawasaidia kuepukana na hasara zinazoweza kuepukika.
Baadhi ya mambo ambayo huweza kusababisha hasara ni kama yafuatayo:
1.UFAHAMU DUNI JUU YA ZAO ANALOLIMA.
Mara nyingi wengi wetu hutaka kuanza kufanya kilimo bila kuwa na uelewa juu ya namna ya kulima,changamoto za magonjwa na wadudu na utatuzi wake na hivyo wengi hujikuta wanafika kati ya uhalibifu na utatuzi hakuna.
SULUHISHO.
Tafuta ufahamu kabla hujaanza ili angalau hata usiibiwe na wasimamizi.
2.UFAHAMU DUNI WA MASOKO.
Hapa wengi hukurupuka kwa sababu ya bei ya mwaka jana.Wengi wamepata hasara pia kwa kusikia zao flani linalipa na hata bila kufanya uchunguzi wa kina wanaishia kuambulia madeni ya mikopo na hasara za kupoteza nyumba zao.Lakini kama angetulia na kutafuta habari za kina juu ya soko la bidhaa hiyoo,huenda asingelima au kulima zao stahiki katika eneo husika.
3.USIMAMIZI MBOVU.
Usimamizi ndio kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya kuwa imara sana,lakini imekuwa tofauti kwa watu wengi wanaoingia kwenye kilimo na hivyo kuambulia hasara au kupata mazao chini ya kiwango.Wengi wamekuwa wakiweka wasimamizi ambao kimsingi hawana utaalamu wala uzoefu wowote juu kilimo na hata kutopata utaalamu wa kilimo na hivyo madawa kupigwa under dosage na usimamizi mwingine wa chini ya kiwango na matokeo ni kuambulia hasara.
SULUHISHO.
msimamizi awe anauzoefu au uelewa juu ya kilimo na awe na uchungu na kazi yako vinginevyo utavuna mabua.
4.KILIMO CHA WHATSAAP.
Wengi wa wanaojiigiza kwenye kilimo wamekuwa wavivu kutembelea mashamba yao na hivyo kuishia kuagiza na kutumiwa picha za maendeleo ya zao kwa picha za whatsap.Hili limewaghalimu wengi na wamepata hasara kubwa sana,kwani wasimamizi huweza kutuma picha za mashamba ya watu wengine yenye hali nzuri na hivyo unapata moyo na kutuma pesa ambapo mwisho wa siku unaambulia majonzi.
SULUHISHO.
Kama huna muda wakutosha au msimamizi atayefanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa basi ni vema ukaahilisha.
5.KUTOTATHMINI GHARAMA ZA UENDESHAJI.
Hii pia ni ukurupufu unaopelekea hasara isiyo kifani kwani mtu anamtaji mdogo anataka kulima eneo kubwa na mwisho wa siku anashindwa kugharamia baadhi ya mahitaji kama madawa,mbolea na usimazimizi mwingine na matokeo yake ni kupata mazao ambayo hayarudishi hata mtaji wako.
SULUHISHO.
Kabla hujaanza kulima tafadhali hakikisha unapata taarifa za gharama kwa kina na kutoka kwa watu wanaoaminika.
KAMA KUNA MENGINE WAWEZA ONGEZA.