CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,958
- 9,518
Mkuu ni kweli Tanzania kuna wafanya kazi wakulima. Hiyo iko Bongo halafu tuwaze kushindana na wakulima wa South Africa au Kenya ambao wana export hadi USA?ni kweli kabisa.
Mkuu ni kweli Tanzania kuna wafanya kazi wakulima. Hiyo iko Bongo halafu tuwaze kushindana na wakulima wa South Africa au Kenya ambao wana export hadi USA?ni kweli kabisa.
haiwezekani kabisa..ndo hivo tusipobadilika tutaishia kulaumu kilimo.Mkuu ni kweli Tanzania kuna wafanya kazi wakulima. Hiyo iko Bongo halafu tuwaze kushindana na wakulima wa South Africa au Kenya ambao wana export hadi USA?
hautakiwi kukimbia biashara au kilimo kwa sababu umepata hasara..ila usipojua kwanini umepata hasara huenda ukawa unapata hasara za mara kwa mara ambazo huenda zikakuvunja moyo kuendelea.Kila Biashara zina faida na hasara!Ni Kwa vile huwa watu hawasemi.Hata big corporations zinapata hasara;ila zinabebwa na wingi wa shareholders.Mbona mashrika mengi ya Ndege ni hasara ila yanapewa ruzuku!
With time watu wanajifunza,punde watapata faida.Kufanya makosa na kupata hasara no Kitu cha kawaida,unahitaji kujifunza kwenye makosa.Mtu Anayejua makosa mengi kwenye Biashara na akajifunza siku moja atafanikiwa.Kosa ni kukimbia Biashara Kwa loss moja!!Utakimbia hadi lini?
pole sana mkuu,,kilimo ni biashara inayohitaji usimamizi wenye mzuri na msimamizi makini na usikubali kuanza mradi wa kilimo kama huna muda wa kutosha kulembelea shamba lako mara kwa mara na pia licha ya msimamizi lazima kuwepo mtaalamu atakayekuwa anamshauri na kumfundisha msimamizi wako(kama mradi ni mkubwa).Asante kwa kutukumbusha! Namba 3 na 4 vimenigharimu mno, kiasi kwamba sina hamu tena na kilimo cha aina yoyote.
asante.Ahsante kwa kuleta Maarifa
Kilimo kimekuwa kikinadiwa na kupigiwa upatu na wahamasishaji wa aina mbalimbali hususani wale wanaosisitiza kulima kibiashara na kuwapa watu matumaini bila kuwadokeza vitu mhimu ambayo vitawasaidia kuepukana na hasara zinazoweza kuepukika.
Baadhi ya mambo ambayo huweza kusababisha hasara ni kama yafuatayo:
1.UFAHAMU DUNI JUU YA ZAO ANALOLIMA.
Mara nyingi wengi wetu hutaka kuanza kufanya kilimo bila kuwa na uelewa juu ya namna ya kulima,changamoto za magonjwa na wadudu na utatuzi wake na hivyo wengi hujikuta wanafika kati ya uhalibifu na utatuzi hakuna.
SULUHISHO.
Tafuta ufahamu kabla hujaanza ili angalau hata usiibiwe na wasimamizi.
2.UFAHAMU DUNI WA MASOKO.
Hapa wengi hukurupuka kwa sababu ya bei ya mwaka jana.Wengi wamepata hasara pia kwa kusikia zao flani linalipa na hata bila kufanya uchunguzi wa kina wanaishia kuambulia madeni ya mikopo na hasara za kupoteza nyumba zao.Lakini kama angetulia na kutafuta habari za kina juu ya soko la bidhaa hiyoo,huenda asingelima au kulima zao stahiki katika eneo husika.
3.USIMAMIZI MBOVU.
Usimamizi ndio kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya kuwa imara sana,lakini imekuwa tofauti kwa watu wengi wanaoingia kwenye kilimo na hivyo kuambulia hasara au kupata mazao chini ya kiwango.Wengi wamekuwa wakiweka wasimamizi ambao kimsingi hawana utaalamu wala uzoefu wowote juu kilimo na hata kutopata utaalamu wa kilimo na hivyo madawa kupigwa under dosage na usimamizi mwingine wa chini ya kiwango na matokeo ni kuambulia hasara.
SULUHISHO.
msimamizi awe anauzoefu au uelewa juu ya kilimo na awe na uchungu na kazi yako vinginevyo utavuna mabua.
4.KILIMO CHA WHATSAAP.
Wengi wa wanaojiigiza kwenye kilimo wamekuwa wavivu kutembelea mashamba yao na hivyo kuishia kuagiza na kutumiwa picha za maendeleo ya zao kwa picha za whatsap.Hili limewaghalimu wengi na wamepata hasara kubwa sana,kwani wasimamizi huweza kutuma picha za mashamba ya watu wengine yenye hali nzuri na hivyo unapata moyo na kutuma pesa ambapo mwisho wa siku unaambulia majonzi.
SULUHISHO.
Kama huna muda wakutosha au msimamizi atayefanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa basi ni vema ukaahilisha.
5.KUTOTATHMINI GHARAMA ZA UENDESHAJI.
Hii pia ni ukurupufu unaopelekea hasara isiyo kifani kwani mtu anamtaji mdogo anataka kulima eneo kubwa na mwisho wa siku anashindwa kugharamia baadhi ya mahitaji kama madawa,mbolea na usimazimizi mwingine na matokeo yake ni kupata mazao ambayo hayarudishi hata mtaji wako.
SULUHISHO.
Kabla hujaanza kulima tafadhali hakikisha unapata taarifa za gharama kwa kina na kutoka kwa watu wanaoaminika.
KAMA KUNA MENGINE WAWEZA ONGEZA.
Hahaaa unaongelea jwa upande wa Dini? vipi kwa wenzetu kule wanapigana na still wana mashamba makubwa na wana export?Kilimo hakiwalipi kwa sababu hawajaikomboa hiyo ardhi kwa Damu ya Yesu kristo, maana hujui kabla ya wewe kuanza kulima hapo ni wakina nani walikuwa wanalima na je ni mambo gan yasiyo faa wamefanya juu ya hiyo ardhi? Ni nini kimetamkwa juu ya hiyo ardhi mpaka isiweze kutoa mazao inavyotakiwa? Maana ardhi pia inaongea kwa mujibu wa maandiko. Cha msingi ni kujua historia ya hilo eneo kabla hujanunua ili uweze kujipanga kwa kuondoa mamlaka iliyopo katika hiyo ardhi na kusimika mamlaka unayoamini kuwa utafanikiwa ukilima mahal hapo: kwa wale wa Imani naamin watakuwa wanaelewa ninamaanisha nini lkn ukiingia kichwa kichwa na mkopo wako wa benk kwenye kilimo bas utaishia kuuziwa nyumba yako kwa kushindwa kulipa deni maana aridhi ikikukataa hakuna utakacho vuna.
wengi wanaopata hasara hufanya ambayo huwa ni off season mf.kilimo cha tikiti...msingi mkubwa ni usimamizi na utaalamu.Off season production ndo siri ya kilimo chenye tija..
ok!Asante sana mkuu